Wanaharakati: Ziachieni simu za VodaCom!

This just makes the whole 'war against ufusadi' thing sound rather moronic.. This could never be effective therefore there is no point in even wasting time debating it..

Inashangaza pamoja na thread kufika mpaka page zaidi ya 10, kuna mediocre-thinking individuals bado wameshindwa ku-decipher the thread mpaka usawa huu..lol
 
Nasikia Marekani wanapitisha tena mbiu ya - BUY AMERICAN, yaani inawahamasisha wananchi kununua vitu ambavyo vimetengenezwa Marekani tu.. Je hiii kitu haifanani ya hiyo ya MMJ..
 
Nani huwa anarekodi hiyo makitu?Mengi nini??Hilo la mafumbo hata mie nimelisikia sasa na hawapokei kabisa simu ambazo hawazijui..Yote haya yanasababishwa na Mengi..

Anawafuata fuata sana watu wa Jedwali la RA

Gembe,
Kuwa mwangalifu mkuu, mimi nilimtaja huyo Mengi nikafungiwa. Lakini ukimchana-chana RA kama inavyoendelea hivi sasa vifungu maalumu havitumiki.
 
Fallacious argument at its best. Hakuna masika yaso na mbu, ni either tunakubali mabadiliko kwa manufaa ya wengi au tunaendelea kupigika kwa manufaa ya wachache, the options are in front of us.

Unganisheni dots: Abdulhalim...(?)
 
Inashangaza pamoja na thread kufika mpaka page zaidi ya 10, kuna mediocre-thinking individuals bado wameshindwa ku-decipher the thread mpaka usawa huu..lol

Je, wewe unataka kutuambia kuwa ni Mwanakijiji lakini unatumia jina tofauti?
 
MODs, kuna uhalali wowote wa mada hii kuendelea kuwepo?

Ni vema tukawa na standards zinazoapply kwa all JF members. Kama habari/mada ipo 'empty' na inamwelekeo wa kuathiri biashara/masahi ya watu (RA si pekee mmiliki wa Vodacom, Vodacom SA wana 65% shareholding!) ni vema ikawa na supporting evidence/facts za kutosha kabla haijaqualify kuwekwa hapa JF (or at least kwenye jukwaa hili!)

Kwa sababu ni habari inayoweza kuathiri maslahi ya kibiashara ya vodacom ama ya 'usalama' wa wanaharakati, kama ina ukweli wowote basi ni vema ukweli huo mtoa mada akau substantiate, vinginevyo nawaomba MODs waifute (With due respect kwa Mzee Mwanakijiji).We better stick to our motto: JF, Where We Dare to Talk Openly!

Kwa sababu ya mapungufu yake, hii mada naona inaleta malumbano yasiyo na msingi. Kama, mtoa mada mpaka sasa hajajibu (au kufafanua) maswali ya wanajamvi, binafsi sioni uhalali wa mada hii kuendelea kuwepo hapa.

Mods,

Ninaungana na SMU katika kuhakikisha kuwa kwa mujibu wa rules za JF hii thread inatakiwa kufungwa.

Please do the needful.
 
counting.. joto linapanda, joto linashuka.. kijasho chembamba.. Kama hauko katika mapambano dhidi ya ufisadi endelea na Vodacom. Hili si gumu. Mada imeanza na "wanaharakati". Kama wewe siyo (hili ni mwenyewe unajifahamu).. carry on with your life, waalike ndugu zako na jamaa zako kutumia simu za vodacom. Kama ni Mwanaharakati na hauko tayari kusalimu amri.. do the needful...

MM
 
Labda ifungwe kwa kuwa mtoa mada kaingia mitini? Vinginevyo tahadhari yake ni nzuri tu kwa walengwa. Vita na wenye nazo si lelemama.
 
Wewe kama unapinga ufisadi unakula vitu vya mafisadi........huna haja ya kuja kubwatuka hapa nadhani ndilo lengo maalum la hii mada ..........kwa maana hiyo labda nikusaidie pundaseven;rostam ana share kubwa tu vodacom;mramba ana share kubwa tu vodacom .....kuna haja gani ya kuja kuwabwatukia hapa kama mnakula matunda ya mafisadi....na hii inaa maanisha wanatakiwa wajue hatuhitaji mali za kifisadi ili tuishi....
 
Je, wewe unataka kutuambia kuwa ni Mwanakijiji lakini unatumia jina tofauti?

Sikutegemea swali substd kutoka mtu kama wewe. Nway, sijui swali lako lina mchango gani ktk hii thread au ktk larger picture.

Labda Mwanakjj atakusaidia kukujibu.
 
hili swala la kususia huduma za mafisadi ni jema sana,
tusiwape nafasi wanatucheka.
 
We all know VODACOM are too expensive, but what we can do? Ourself we want everything whatever is cheap or expensive.
 
Juzi juzi tu niliona post inayotaka watu kususia bidhaa za duka la Mlimani Game, sikuona mtu yeyote iliyesema kuwa hiyo post ifutwe!Mbona hii ya Vodacom kuna baadhi ya watu imewaudhi sana? Nimeshiriki sana katika kususia bidhaa na vitu mbalimbali, na kwa kumbukumbu zangu nakumbuka tulshasusia hata bidhaa za Afrika Kusini wakati wa Apartheid, tukafanikiwa. Tumesusia bidhaa zinazotengenezwa Israel, na kuna mafanikio kuwa kususia bidhaa hizo kunasaidia katika harakati. Sasa likija hili swala la kususia Vodacom, hapa nchini kweti, mbona inakuwa shida?? Mimi nitasusia, na nitaendeleza kusambaza neno kwa watu wengi nitakavyoweza, kuwa kutumia bidhaa kutoka kwa watu wanaohujumu uchumi wetu ni sawa na kujiweka kitanzi mwenyewe. Wewe unayetaka kuendelea nayo, endelea tu, hukatazwi. Sisi tutaendelea tu, na uashindi utapatikana tu, maana harakati zetu ni za kihalali. Namnukuu Che Guevara akielezea mapinduzi. Aliwahi kuandika: 'Wherever death may suprise us, it will be wellcomed, provided that, this, our battlecry reaches some receptive ear...' Patria o muerte, venceremos!
 
Juzi juzi tu niliona post inayotaka watu kususia bidhaa za duka la Mlimani Game, sikuona mtu yeyote iliyesema kuwa hiyo post ifutwe!Mbona hii ya Vodacom kuna baadhi ya watu imewaudhi sana? .................. Sasa likija hili swala la kususia Vodacom, hapa nchini kweti, mbona inakuwa shida?? Mimi nitasusia, na nitaendeleza kusambaza neno kwa watu wengi nitakavyoweza, kuwa kutumia bidhaa kutoka kwa watu wanaohujumu uchumi wetu ni sawa na kujiweka kitanzi mwenyewe. Wewe unayetaka kuendelea nayo, endelea tu, hukatazwi.

Mimi pia ni mmoja wa waliopendekeza mada ifutwe/ihamishwe. Si kwamba naunga mkono ufisadi, la khasha! Ila ni kwa sababu post yenyewe haina clear motive (kwa kifupi bado ina lack substance!). Lazima tuwe na standards na kuzifuata.

Mtu mwingine anaweza pia akaibuka na kuweka post kama hiyo lakini kwenye neno Vodacom, akaweka neno Tigo, au Zain, au TTCL au kampuni nyingine yoyote bila kuwa na supporting evidence au angalau sababu. Je moderator watakuwa na basis gani ya kufuta post kama hizo kama hii imeachwa?

Ukifuatilia wachangiaji utaona jinsi watu walivyokuwa wanajaribu kuspeculate sababu za kususia vodacom (kwa mfano kuna waliosema simu zinakuwa monitored na kila unapopiga simu RA anaweza kuisikiliza!). Hizi ni claim za hatari kama hazina ushahidi.

Kwa kiasi wewe umejaribu kuonesha ni kwa nini tususie (see red highlights above). Ukisoma ile mada ya kuepuka bidhaa za Game, haipo empty kama hii.

Hata hivyo naona mwenyewe MM ameshasema walengwa ni wanaharakati (wanajielewa!) na hivyo wasio wanaharakati wasihofu (ingawa hii kwa namna fulani inahitilafiana na sababu uliyoitoa wewe hapo juu).

Together we stand, divided we fall.
 
Last edited:
Juzi juzi tu niliona post inayotaka watu kususia bidhaa za duka la Mlimani Game, sikuona mtu yeyote iliyesema kuwa hiyo post ifutwe!Mbona hii ya Vodacom kuna baadhi ya watu imewaudhi sana? Nimeshiriki sana katika kususia bidhaa na vitu mbalimbali, na kwa kumbukumbu zangu nakumbuka tulshasusia hata bidhaa za Afrika Kusini wakati wa Apartheid, tukafanikiwa. Tumesusia bidhaa zinazotengenezwa Israel, na kuna mafanikio kuwa kususia bidhaa hizo kunasaidia katika harakati. Sasa likija hili swala la kususia Vodacom, hapa nchini kweti, mbona inakuwa shida?? Mimi nitasusia, na nitaendeleza kusambaza neno kwa watu wengi nitakavyoweza, kuwa kutumia bidhaa kutoka kwa watu wanaohujumu uchumi wetu ni sawa na kujiweka kitanzi mwenyewe. Wewe unayetaka kuendelea nayo, endelea tu, hukatazwi. Sisi tutaendelea tu, na uashindi utapatikana tu, maana harakati zetu ni za kihalali. Namnukuu Che Guevara akielezea mapinduzi. Aliwahi kuandika: 'Wherever death may suprise us, it will be wellcomed, provided that, this, our battlecry reaches some receptive ear...' Patria o muerte, venceremos!

We ndugu uko nchi gani? Tunaomba usituletee udini hapa. Tanzania si taifa la kiislamu kususia bidhaa za Israel. Be carefull usituletee laana katika taifa letu.
 
counting.. joto linapanda, joto linashuka.. kijasho chembamba.. Kama hauko katika mapambano dhidi ya ufisadi endelea na Vodacom. Hili si gumu. Mada imeanza na "wanaharakati". Kama wewe siyo (hili ni mwenyewe unajifahamu).. carry on with your life, waalike ndugu zako na jamaa zako kutumia simu za vodacom. Kama ni Mwanaharakati na hauko tayari kusalimu amri.. do the needful...

MM

Mwanakijiji,
Tumekuomba utupe maelezo zaidi lakini bado naona unaendelea kutuacha kwenye mataa tu. Kwani wanaharakati wamekewa label gani? Wanaharakati tuko wengi kuanzia wale wa high rank mpaka wale wa low rank. Ungetuambia namna tutakavyoathirika kwa kuendelea kutumia network ya Vodacom, nafikiri haya malumbano yanayoendelea hapa na watu mpaka wanatoleana maneno makali na yasiyofaa yangekoma. Lakini bado unaucha mjadala uendelee kila mtu akitoa maoni kwa kadiri nafsi yake inavyomtuma. Mwanakijii, please weka wazi suala hili ili mjadala uishe.
 
Mwanakijiji unafikiri matatizo yetu yataisha kwa kususia mtandao wa Vodacom ,hao jamaa wanaweza kununua share kwenye kampuni yeyote kwa hiyo tutakuwa hatujafanya lolote

Mkuu Belo, swali lako ni la msingi sana.

Nimekuwa nikijaribu kutafakari tangu nilipoiona thread hii mara ya kwanza (jana), kwa lengo la kutaka kuona ni kiasi gani ususiaji wa Vodacom unaweza kusaidia katika kuleta ufanisi wa mapambano dhidi ya ufisadi. Nataka kusema ninapoandika leo kujaribu kuchangia, ninakuwa nimejiridhisha kabisa kuwa naelewa mantiki nzima ya madhara v/s faida ya kususia Vodacom (hasa kwa lengo la kumkomoa mtu mmoja au wawili) kwa sababu zozote tunazoweza kubuni.

Kwa manufaa ya mjadala, ningependa kubainisha madhara machache halafu tuyalinganishe na sababu zilizotolewa na baadhi ya watu kuhalalisha kususia Vodacom.


  1. Vodacom inachangia maendeleo ya nchi kwa kulipa Kodi: Hulipa kodi zote inzotakiwa kulipa (PAYE za wafanyakazi wao, SDL, VAT etc). Kususia kutumia bidhaa zao kutasababisha kodi itokanayo na operation zao kushuka na hata kupotea kabisa kama wataamua kufunga biashara yao kutokana na hasara watakayoipata
  2. Vodacom inaajiri waTanzania: Japokuwa idadi kamili ya wafanyakazi wa Vodacom sinayo, inakadiriwa kuwa imeajiri zaidi ya waTanzania 600 nchi nzima. Wafanyakazi hawa hupata nafasi ya kuendeleza taaluma zao (kupitia training, na on-site experience, exposure to technology etc). Vile vile, hulipwa mafao yao vizuri na kuweza kujikimu wao na familia zao. Kwa kuwa na kipato hicho, wafanyakazi hao pia huchangia jitihada mbalimbali za kijamii wanazokabiliana nazo. Kwa ajira hiyo pia, waTanzania wenzetu hawa wanapata nafuu ya kisaikolojia itokanayo na kupata fursa za kujishughulisha.
  3. Misaada na michango ya jamii: Vodacom kama baadhi ya taasisi nchini, hushiriki katika kuchangia michezo, taaluma, afya, na mambo mengine mengi. Vodacom ikisusiwa, uwezo wake wa kusaidia jamii utapungua na hatimiye kuweza kupotea kabisa.
  4. Wadau wengine: Vodacom hutumia kampuni nyingi ndogo na kubwa za watanzania katika kupata huduma zake mbalimbali. kuna kampuni zinazotumika kuwafungia mitambo, kujaza mafuta (diesel) kwenye generators zilizopo kwenye vituo vyao (BTS sites), kuna wanaosambaza vouchers (wako wengi zaidi), sim Cards, wanaopata kazi za kutangaza biashara zao, kuna wanaofanya usafi kwenye maeneo ambayo hutumiwa na kampuni hiyo, n.k. Idadi ya wadau wanaopata kipato kupitia Vodacom ni kubwa. Vodacom ikisinyaa, nao watasinyaa.
  5. Hudama waitoayo. Pamoja na wengi kubainisha kuwa huduma za Vodacom ni ghali, lakini inaelekea inapata wateja wengi zaidi kuliko kampuni zinazotoza viwango vidogo zaidi. Kwa mtazamo wangu ni kuwa, kinachotakiwa na wateja wa Vodacom si u-ghali wa huduma bali ni ubora wake. Nadhani tutakubaliana wote kuwa huduma za simu za mkononi ni chachu kubwa ya maendeleo ya nchi yetu. Huduma hizi zinasaidia kuharakisha na kurahisisha mawasiliano na kufanikisha matumizi bora ya muda (time management). Vodacom ikishindwa ku-operate, si tu kwamba wananchi wengi watapata shida kwa kukosa huduma hizo katika baadhi ya sehemu walipo, bali pia ushindani wa kibiashara utapungua na hivyo kampuni nyingine kuongeza bei za huduma au kubweteka katika kutoa huduma hizo au kuzorota kwa mambo mengine. Kumbukeni Tritel na mtandao uliokuwa ukiishia Kimara.

Kuna mengi yenye manufaa kwa kuwa na Vodacom. Vodacom kama zilivyo kampuni nyingine nchini, haziwezi kukua/kustawi na kuweza kushiriki katika harakati za kuinua uchumi wetu kama hazitakuwa na mafanikio katika biashara zao. Na mafanikio yao yatatokana na ushirikiano kati yao na wadau wote pamoja na wateja wao popote walipo. Nchi hii haiwezi kukua kwa kususia bidhaa.

Kuisusia Vodacom ni uthibitisho tosha kabisa kwamba tutakuwa tunataka kushindwa kujikwamua kiuchumi na kijamii kwa kudhoofisha mdau muhimu katika kukuza uchumi wetu. Kuisusia Vodacom kutaanzisha hofu kwa kampuni nyingine zote. Na wao wataanza ku-invest kwa uangalifu wakitegemea kususiwa wakati wowote na hivyo kuwaingiza kwenye hasara.

Kususia Vodacom au kampuni nyingine yoyote ya simu hakuwezi asilani kumnyima sana usingizi mwekezaji aliewekeza katika kampuni hiyo. Kwani kadiri atakavyoona trend ya profit inabadilika, atahamisha share zake kwenye operation nyingine inayolipa zaidi na kufunga virago. Wakuu, wawekezaji huwa hawasubiri kula hasara kabla ya kuamua hatua za kuchukua kuokoa rasilimali zao. Na huchukua hatua kwa haraka ajabu
.

Kwa kumalizia tu, nadhani thread hii ni ya hatari sana kwa ustawi wa Taifa letu. Ni thread ya aibu kwa uzaleno wa nchi yetu na inatia hofu kuhusu ukweli wa kuwa tunaitakia mema nchi hii.

Naomba nieleweke tu kwamba niliyoyasema hapo juu ni imani yangu na inaweza kuwa na mapungufu. Ila ileweke pia kuwa sina affiliation ya aina yoyote na Vodacom zaidi ya kuwatakia heri kama ninavyowatakia wawekezaji wengine nchini.
 
:rolleyes::rolleyes:And the warning is very clear it is directed to activists and not to everyone kwenye JF nashangaa watu hawamuelewe Mwanakinjiji.

Kama ndo hivyo basi angewapelekea hao wanaharakati kwenye private mail zao.

Nnavyofahamu ukishabandika thread basi unaalika wanajamii wote waijadili.
 
Back
Top Bottom