Elections 2010 Wanaharakati watoa masaa 72 kwa serikali......

urasa

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
434
2
hili limekaa vizuri,kufuatana na serikali kuendelea kujishebedua na kusuasua juu ya hatma ya wanvyuo kushiriki uchaguzi mkuu,wanaharakati hao wameamua kuipa masaa 72 kinyumme na hapo ni kuwepo kwa maandamano ya amani kushinikiza hilo jambo,lets join this guyz,safari yetu ya uhuru wa kweli tunakaribia
 
Bomba sana wakuu.

Lakini hao wanavyuo wanasemaje kuhusu hilo? Je haki yao hiyo wanaitamani au? Isiwe tunawapigia debe bure ilhali wenyewe hata hawaoneshi dalili ya kuwa wamedhulumiwa kutokupiga kura. Naomba kama kuna wanaJF wanavyuo wajitokeze kwa kuunga mkono wanaharakati, wakijiweka wazi kuwa wao ni waathirika wa kukosa kupiga kura(bila kutaja identiti zao of koz).

Big Up wanaharakati. Tupo pamoja.
 
Kama kweli ni wapiganaji na wanauchungu na nchi basi wangetembea hata kwa miguu hadi vyuoni mwao kupiga kura maeneo waliyojiandikisha kuliko kupiga kelele nyumbani huku wameshika remort control ya tv .. Wakiangalia channel o / big brother / ze comedy .. Wakati wa azimio la arusha wazee wetu walitembea kwa miguu toka tanga mpaka dar.. Ni wakati wa kufanya na sio kubaki kupiga kelele tu.. Tumenyimwa haki zetu
 
ngoja uchaguzi usogezwe hata wiki tu halafu uone hiyo negative impact
 
Nimeipenda hiyo kwani itaendelea kuitia tumbo joto sisiem. Ninawashauri wanaharakati wafanye mobilization ya kutosha ili mahudhurio yaitikise jiji la Dar. Nami kwa upande wangu nimeanza kuwatumia sms rafiki zangu ili siku hiyo tuhudhurie.

wakati wa ukombozi ni sasa siyo kesho.
 
HII NI HAKI YA MUHIMU. DAFTARI LILIPOSAHIHISHWA WALIKUWA VYUONI. KURA WAKO NYUMBANI. TATIZO NI KWAMBA HATA WAKIWA NA NAULI YA KURUDI KUPIGA KURA BADO WATAHITAJI MALAZI WATAKAOPOTEZA HAKI YAO BADO NI WENGI SANA. HIVYO KUFUNGUA CHUO Ndiyo busara kwani hawatahitaji gharama za ziada. Laiti watu wangeandamana kudai tume huru ya UChaguzi. Isiyotokana na utezuzi wa chama cha mgombea yeyote.
 
hili limekaa vizuri,kufuatana na serikali kuendelea kujishebedua na kusuasua juu ya hatma ya wanvyuo kushiriki uchaguzi mkuu,wanaharakati hao wameamua kuipa masaa 72 kinyumme na hapo ni kuwepo kwa maandamano ya amani kushinikiza hilo jambo,lets join this guyz,safari yetu ya uhuru wa kweli tunakaribia

Hao wanachuo ni wasomi kama wana akili nzuri yakufikiria nakuona mbali walitakiwa kuomba ufafanuzi mapema kutoka tume ya uchaguzi kuwa wao itakuwaje maana tarehe ya uchaguzi ilikuwa inajulikana mapema saana tu.asa wanangoja mambo hadi yaharibike ndio waje wajifanye wanataka haki ya kupiga kura?hao wanzuoni wamechemsha bora wakae kimya tuu.limeshapita hilooooooooo no soln zaidi yakutulia na kumgoja 2015.teh teh teh.
 
Kama kweli wako seroius kushiriki uchaguzi hata kama itashindikana watu wajitolee kushare accommodation kwa kuchangishana kwa hizo siku chache hadi vyuo vitakafunguliwa kwani si mbali sana kulinganisha na hasara ya kukosa kupiga kura.
 
Hao wanachuo ni wasomi kama wana akili nzuri yakufikiria nakuona mbali walitakiwa kuomba ufafanuzi mapema kutoka tume ya uchaguzi kuwa wao itakuwaje maana tarehe ya uchaguzi ilikuwa inajulikana mapema saana tu.asa wanangoja mambo hadi yaharibike ndio waje wajifanye wanataka haki ya kupiga kura?hao wanzuoni wamechemsha bora wakae kimya tuu.limeshapita hilooooooooo no soln zaidi yakutulia na kumgoja 2015.teh teh teh.

Joyce

Embu niambie umesoma chuo gani? embu nikumbushe ni lini semister ya Kwanza ilianza mwezi wa kumi na Moja tangu mwaka 2000? kwanini itokee mwaka huu, just reason na sio kuandika vitu usivyovielewa.
 
I will be there kuishinikiza serikali.
waitishe maandamani ya amani tuoneshe mshikamano
 
we msanii unajua kiswahili kweli? maandamani ndiyo nini?..............je ukipewa jukumu la kuongea utaweza kujiexpress kwa maana humu tu unashindwa .
 
we msanii unajua kiswahili kweli? maandamani ndiyo nini?..............je ukipewa jukumu la kuongea utaweza kujiexpress kwa maana humu tu unashindwa .
Nilishapanga kutojibu hoja zako kabisaaa. lakini kwa hili nakujibu kwa kusema thanx mkuu NOVA
 
Ndiyo msanii labda ndiyo kusema umekubali kushindwa kimyakimya hakikisha unajipanga kujibu hoja sio kususa...................ulidhani kila mtu atakubaliana na hoja zako dhaifu?.......au?
 
HII NI HAKI YA MUHIMU. DAFTARI LILIPOSAHIHISHWA WALIKUWA VYUONI. KURA WAKO NYUMBANI. TATIZO NI KWAMBA HATA WAKIWA NA NAULI YA KURUDI KUPIGA KURA BADO WATAHITAJI MALAZI WATAKAOPOTEZA HAKI YAO BADO NI WENGI SANA. HIVYO KUFUNGUA CHUO Ndiyo busara kwani hawatahitaji gharama za ziada. Laiti watu wangeandamana kudai tume huru ya UChaguzi. Isiyotokana na utezuzi wa chama cha mgombea yeyote.

Kama vyuo vikifunguliwa kabla ya uchaguzi, utatatua vipi tena tatizo la wanafunzi wa mwaka wa kwanza (first year) ambao walijiandikisha katika maeneo yao wanayoishi sasa(nyumbani kwao).Hivyo, kufungua vyuo si suluhisho la tatizo hili,kwani bado wanafunzi wa mwaka wa kwanza nao watakosa fursa ya kupiga kura iwapo vyuo vitafunguliwa
 
Ukisema mwaka wa kwanza nao watapata tatizo la kutopiga kula pia wanafunzi walio vyuoni inaonesha dhairi kuwa Tanzania ina utawala mbovu,wanaandaa daftari ikiwa wanajua raia wake hawakai sehemu moja kama majengo, mambo kama haya yalikuwa kwenye nchi ya kusadikika kwa mfalme Juha. Namuomba Rais wa Tano wa JMT akiapishwa atoe Tume/NEC iliyo huru.
 
Back
Top Bottom