WANAHARAKATI, Ulimboka MNAFANYA KAZI YA KANISA

kiogopeni

Member
Jun 26, 2012
31
7
Ulimboka ana damu tofuti na Waislamu waliouliwa Mwembechai?

Sehemu ya mazungumo ya Mheshimiwa Kitwana Kondo (MB) mbele ya waandishi wa habari Mei 27, mwaka huu

JUZI tarehe 21 ya mwezi huu, niliwaambia ya kwamba mimi ni mwanachama wa CCM, na kiongozi wa CCM, na nina wajibu mimi wa kufuata maagizo na maelekezo yote ya CCM. Niliwaambia pia ya kwamba nina wajibu mimi wa kutetea maamuzi ya serikali ya Chama Cha Mapinduzi.
Lakini nilisema pia kwamba pia nina wajibu wa kuishauri serikali yangu pale ninapoona inafanya makosa. Wajibu huu mie ninao.
Nililolisema na ninalisema tena leo ni kwamba serikali imekuwa Insensitive kwa mambo yanayowahusu Waislamu na mambo mengine. Na kwa kuwa serikali inakuwa insensitive Waislamu wanatafsiri ile insensivity ya serikali kuwa bila shaka serikali haiwapendi.
Siku ile nilitoa mfano wa kuingia Msikitini Polisi wa serikali walikuwa hawana sababu ya kuingia Msikitini. Lakini lile limetokea na ghasia ambazo serikali yenyewe ili contribute (ilichangia). Kabla ya siku ile polisi wamekuwa wakiwakamata Masheikh majumbani kwao kimya kimya. Kama serikali ingekuwa inataka kumkamata Magezi wangeweza kumkamata Magezi nyumbani kwake.
Lakini serikali katika busara zake iliona Magezi imkamate Msikitini baada ya swala ya Alasiri pale mahala pamejaa watu. Huku ikijua kwamba Magezi ana wafuasi wake. Kwanini isimkamate Magezi asubuhi nyumbani kwake? Kwanini isimkamate Magezi usiku nyumbani kwake?
Wakaamua kumkamata pale. Kitendo kile ndicho kilicholeta rabsha ya tarehe 12.
Watu walipozidiwa nguvu wakakimbilia ndani ya Msikiti. Msikiti ule una wanawake ambao hawakuwahi kutoka. Sasa mimi bado narudia kwamba kama serikali ingetaka ingeweza kuuzingira ule Msikiti wale wangetoka tu. Ni insensitivity yao ya kusema potelea mbali (kwanza) kwanini wangoje mpaka saa nane za usiku, wakavunja
mlango ambao mpaka leo haujatengenezwa wakaingia ndani. Walishawakatia umeme na nini. Wakavunja Msikiti wakaingia ndani. Na si hivyo tu, wakawakamata, wakawapiga wale wanawake wakawapiga. Na wakawamwagia unga ambao unawasha. Mimi nilizungumza na wale wanawake wanaeleza mambo hayo. Sasa mimi nasema hilo linaonyesha insensivity ya serikali.
Na imefanya kosa kuwashitaki wale Waislamu wa Mwembechai kwa kusema Yesu si Mungu. Au kusema Yesu si mwana wa Mungu au kusema Yesu hakusulubiwa. Imefanya kosa kubwa kuwashitaki wale. Kwa kusema maneno ambayo ndiyo anayoyaamini miaka yote. Kila mahali palipo na Uislamu maneno hayo yapo. Sasa naambiwa habari ya mahakama. Mimi sisemi habari ya mahakama. Nasema habari ya serikali. Mahakama inapelekewa kesi. Sasa kesi ya kusema Yesu si Mungu haikutoka kwenye mahakama.
Haya yametoka nje, polisi ndio waliomshitaki mtu huyu kwa kusema Yesu si Mungu. Serikali ambayo haina dini!
Mwaka 1996 walimamatwa vijana wawili Lushoto. Walikuwa Msikitini wanatoa mawaidha wakasema Yesu si Mungu. Wakangojewa nje walipokuwa wanakwenda sokoni wakakamatwa. Wakashitakiwa kwa kosa, kwa kashfa ya dini nyingine. Dini gani nyingine?
Kashfa yenyewe ni nini wamesema Yesu si Mungu. Na hivi juzi juzi, mambo ndio hayo hayo. Sasa mimi nasema serikali inafanya kosa kubwa, serikali isiyokuwa na dini inafanya kosa kuwashitaki watu kwa sababu ya imani yao.
Hivi karibuni Muadhama Kadinali Pengo amesema kwenye Kiti Moto ya kwamba kwa Muislamu kusema Yesu si Mungu si kashfa. Kwasababu ndio imani yake. Na amesema mimi yaani yeye Kadinali Pengo naamini ya kwamba Mtume Muhammad si Mtume wa mwisho. Hivyo ndivyo imani yangu. Si kashfa kwa dini yoyote.
Si hivyo tu, juzi kwenye gazeti la Dar Leo ... kuna maneno Maaskofu wamuunga mkono K.K. Hawa ni Maaskofu wa Kanisa la Protestant, na wao wanasema kwa Muislamu kusema Yesu si Mungu si kashfa. Na kwa Mkristo kusema Yesu Mungu si kashfa.
Haya ni maneno ambayo yamesemwa na Mabishops, sasa ikiwa dini yenyewe inayosemwa ni kashfa ni dini ya Kikristo, Wakristo wenyewe wanasema si kashfa. Sasa serikali inasema kashfa kwa dini nyingine, dini gani?
Sasa mimi nilichowaomba mnisaidie siku ile ni kuiomba serikali ifute count hii. Serikali kusema lakini kesi iko
mahakamani si kweli. Serikali bado ina uwezo wa kwenda mahakamani na kusema tunafuta count hii. Kuwashitaki kwa sababu wanasema maneno yaliyoko ndani ya Qur’an ndio kusema serikali inaona Qur’an ni kitabu cha uchochezi.
Unapomshitaki mtu mahakamani kwa uchochezi kwa kusema maneno yaliyo ndani ya Qur’an, lazima useme na kitabu chenyewe ni kitabu cha uchochezi.
Sasa ninachosema mimi kwa bahati mbaya hawa kina Bwana walioshtakiwa kwa count hii moja wamepata conviction maana yake, mahakama itakuwa inasema kitabu hiki ni kitabu cha uchochezi.
Swali langu mimi, serikali itaifungia Qur’an? Serikali wataifungia dini ya Kiislamu? Huo ndio woga wangu mimi ... hiki kitabu ni kitabu cha uchochezi inabidi kifungiwe. Hawawezi kuwaambia Waislamu semeni yote lakini haya Yesi si Mungu msiseme. Sasa hii ndio hatari ninayoiona mimi.
Kesi ikiwa mahakamani , pale mwenye uwezo ni hakimu. Lakini hakimu anapima ushahidi uliokuwa pale. Hawa
watu wasema wanastahili kupata dhamana. Hawa watu wanaumwa, wagonjwa. Jana gazeti moja limesema Magezi kadhoofu kabisa. Yule Bwana Kamishna amesema Magezi anatibiwa jela. Na wengine.
Kuna mzee moja Musa Katembo ana umri wa miaka themanini. Basi hata nyie watu wa magazeti hamna huruma, mtu wa miaka themanini! Siku hizi mahakama inasema hata mtu aliyeshitakiwa kwa kuua anaweza kupata dhamana. Itakuwa huyu mzee wa miaka themanini, atafanya nini huyu akipata dhamana.
Sasa mie kuishauri serikali kwamba jamani hawa watu wamekaa zaidi ya miezi mitatu ndani. Ndani kule kuna adha wamekuwa wagonjwa. Mmoja kesha kufa.
Sasa kusema aah alikuja ndani mgonjwa. Sasa kwanini msimpeleke hospitali! Sasa huenda akafa mmoja, mmoja mmoja na dhana ipo. Dhana ipo kwamba serikali inafurahia hivyo; kwamba wafe mmoja mmoja. Sasa dhana can be wrong. Na dhana usiitie kwenye sheria.
Kesi ikiwa mahakamani , pale mwenye uwezo ni hakimu. Lakini hakimu anapima ushahidi uliokuwa pale. Hawa watu wasema wanastahili kupata dhamana. Hawa watu wanaumwa, wagonjwa. Jana gazeti moja limesema Magezi kadhoofu kabisa. Yule Bwana Kamishna amesema Magezi anatibiwa jela. Na wengine. Kuna mzee moja Musa Katembo ana umri wa miaka themanini. Basi hata nyie watu wa magazeti hamna huruma, mtu wa miaka themanini! Siku hizi mahakama inasema hata mtu aliyeshitakiwa kwa kuua anaweza kupata dhamana. Itakuwa huyu mzee wa miaka themanini, atafanya nini huyu akipata dhamana.
Sasa mie kuishauri serikali kwamba jamani hawa watu wamekaa zaidi ya miezi mitatu ndani. Ndani kule kuna adha wamekuwa wagonjwa. Mmoja kesha kufa.
Sasa kusema aah alikuja ndani mgonjwa. Sasa kwanini msimpeleke hospitali! Sasa huenda akafa mmoja, mmoja mmoja na dhana ipo. Dhana ipo kwamba serikali inafurahia hivyo; kwamba wafe mmoja mmoja. Sasa dhana can be wrong. Na dhana usiitie kwenye sheria.
Sasa isisemwe maneno ya kwamba mahakama ndio inayowaweka. Si kweli. Mahakama inaamua baada ya kuambiwa. Waliokuwa wakipinga dhamana siku zote ni serikali. Sasa wakati ule walikuwa wazima afadhali, sasa wagonjwa. Kwahiyo, serikali isibabaishe hapa ikasema oh kesi ipo mahakamani.
Viongozi wangu baadhi wanasema kuwa mimi natafuta umaarufu. Mimi sitafuti umaarufu. Mimi maarufu. Mimi sitafuti umaarufu. Mimi tayari maarufu. Kwahiyo, si kweli kwamba mimi natafuta umaarufu.Mimi nimeanza ubunge 1965. Na tokea nimeanza ubunge sijagombea nafasi yoyote mimi nikashindwa. Yoyote. Sasa umaarufu unakuaje.
Nimegombea ubunge mara nne nimeshinda mara zote nne. Nimegombea udiwani mara tatu nimeshinda mara zote tatu. Nimegombea ubunge juzi juzi, nimeshinda. Nimegombea ujumbe wa kamati ya siasa ya mkoa juzi juzi nimeshinda. Sasa umaarufu unakuwaje. Mie sitafuti umaarufu.
 
Mimi nadhani yale mauaji ya Mwembe Chai kwa kila mpenda amani alitakiwa aishangilie Serikali na kuipongeza, huwezi kufananisha vitu walivyokuwa wanafanya na baadhi ya waliouawa pale Mwembechai na hili Suala la ulimboka. Sana sana tuwaulize Wanaharakati ni kwanini hawakuandamana kuipongeza Serikali kipindi kile hawaoni kwamba wapo Biased? kwasababu Serikali ikifanya jambo jema wanakaa kimya lakini ikifanya kitu kibaya wanaandamana kupinga.
 
ama kweli ukiyastaajabu ya mussa utayaona ya firahuni wewe unaakili timamu kweli wewe ,unajua ulichokiandika wewe,maana kuanzia tittle na msg ni vitu viwili tofauti,nyie ndio prof maji marefu nyie.umetumw na nani ????????????na ukirudia kumtajataja yesu utawekwa jela kabisa
 
Nimejaribu kulinganisha kichwa cha habari na habari yenyewe, sijaona uhusiano wowote kabisaaaa.
 
Back
Top Bottom