Wanaharakati, CDM, wanafunzi vyuoni toeni muda sawa kufanikisha maandamano nchi nzima

M-pesa

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
602
151
Kwa kuwa wadau wasioridhishwa na mwenendo wa serikali ni wengi na wapo karibia kila kona ya nchi yetu. Kwa uchache tu ni pamoja na wananchi wote kwa ujumla wao, wanafunzi vyuoni, wanaharakati, chadema na wafuasi wake maelfu elfu, wafanyakazi n.k
Na kwa kuwa kikundi cha watu wachache wanaoghilibu wananchi na kuamua kuitunga katiba kwa manufaa yao, huku wakiendelea kupata upinzani mkali nje na ndani ya nchi bila kukubali.

Njia pekee ya kufanikisha maandamano makubwa nchi nzima ni kuungana na wadau wote wanaokerwa na haya mambo ya kishenzi yanayofanywa na serikali ya CCM.

Kuungana kwenyewe ni kupanga kwa kutoa tamko la tarehe moja ya maandamano bila kikomo kwa kila kundi nchi nzima.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom