Wanaharakati, CCK wataka polisi wawajibishwe

Kalunguine

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
2,543
134
Na Nasra Abdallah na Asha Bani

MTANDAO wa Mashirika ya Haki za Binadamu Kusini mwa Afrika (SAHRiNGON), umemtaka Rais Jakaya Kikwete, kuwawajibisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na Kamanda wa Polisi mkoani humo, kutokana na mauaji ya raia wanne waliopigwa risasi na polisi wakiwa katika maandamano yaliyofanyika juzi.

Wakati mtandao huo ukitoa shinikizo hilo, Chama Cha Kijamii (CCK), kimesema kuwa kimeanza kukusanya taarifa mbalimbali kutoka kwa wananchi mjini Songea ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kulishitaki Jeshi la Polisi kwa mauaji hayo.

Akizungumza na waandishi jana jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Taifa wa mtandao huo, Martina Kabisama, alisema viongozi hao wanapaswa kuwajibishwa kutokana na kuzembea kuchukua hatua tangu mauaji ya kikatili yalipoanza Novemba mwaka jana hadi kusababisha maandamano hayo yaliyogharimu maisha ya wananchi wasio na hatia.

Pia mtandao huo ulitaka watendaji wengine wanaohusika kama vile mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wa mkoa na watendaji wakuu wa manispaa hiyo kuchukuliwa hatua ikiwezekana kushtakiwa kutokana na uzembe huo na waathirika wote wa tukio hilo walipwe fidia kutokana na madhahara waliyoyapata.

Kabisama alisema SAHRiNGON, wanalaani kitendo cha polisi kutumia mabavu kuzuia maandamano hayo ya amani, jambo lililosababisha vifo vya watu hao na wengine kujeruhiwa kwani kwa kufanya hivyo serikali imewanyima raia hao haki zao za kikatiba.

Aliongeza kuwa tabia ya serikali kuchukua hatua baada ya maandamano au migomo ambayo huwa inasababisha vifo vya watu na majeruhi kutokea, ndiyo imekuwa ikifanya vitendo hivyo kujirudia.

Naye wakili wa mtandao huo, Arnardo Swenya, alisema katika tukio la Songea polisi hawakupaswa kutumia nguvu kuwatawanya wananachi na badala yake wao ndio wangetakiwa wawe walinzi mpaka kuhakikisha wanafikisha ujumbe kwa mkuu wa mkoa kama walivyokusudia.

Hata hivyo, Swenya alisema kwa sasa imekuwa tatizo kwa polisi kutoa vibali vya maandamano jambo linalochangia vurugu kama hizo na kuongeza kuwa tume zinazoundwa katika kuchunguza baadhi ya matukio kama haya zimekuwa kwa ajili ya kuwanyamazisha watu tu pasipo kufanyiwa utekelezaji.

Nao CCK kupitia taarifa ya Mwenyekiti wake, Constantine Akitanda, ilisema wamefikia hatua hiyo kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na jeshi hilo mara kwa mara.

"Tumesikitishwa na kushtushwa na habari za kuuawa kwa wananchi wenzetu kwa risasi na polisi wakiwa katika mazingira ya kudai haki yao ya msingi yaani haki ya kuishi kutokana na kukerwa na kile ambacho wameamini ni kushindwa kazi kwa Jeshi la polisi," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa kilichotakiwa kufanyika ni uongozi huo kuweka utaratibu wa kusikiliza maoni na kilio cha wananchi hao na si kuwaua kama jeshi lilivyofanya.

CCK pia imeutaka uongozi wa jeshi hilo kuchunguza kauli ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Michael Kamuhanda, za kwamba wananchi walitaka kuvamia Ikulu na kituo cha polisi.[/SIZE][/COLOR]

Source: Tanzania Daima

TAMKO LA CCK:

24-02-2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


MAUAJI YA RAIA YANAYODAIWA KUFANYWA NA POLISI HUKO SONGEA KWA KILE KINACHODAIWA KUWA NI MAZINGIRA YA KISIASA

Chama Cha Kijamii (CCK) kimeanza kukusanya taarifa mbalimbali kutoka kwa wananchi mjini Songea, mkoani Ruvuma, ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kulishitaki jeshi la polisi kwa mauaji ya watu wane yaliyotokea Jumatona wiki hii.

CCK imefikia hatua hiyo kutokana na kukithiri kwa vitondo vya ukiukwaji wa haki za kibinadamu unaofanywa na jeshi hilo kwa muda mrefuhuku mamlaka zote zikiwa zimekaa kimya. Kwa sisi kama chama tumesikitishwa na kushtushwa na habari za kuuawa kwa Watanzania wenzetu kwa risasi na polisi wakiwa katika mazingira ya kudai haki yao ya msingi yaani haki ya kuishi. Wananchi hao wa mjini Songea walikerwa na kile ambacho wananchi hao wameamini ni kushindwa kwa jeshi la polisi kufuatilia mauaji ambayo yamedaiwa kuwa yamekuwa yakitokea kwa muda sasa mjini hapo yakihusishwa na ushirikina.

Wananchi hao kwa umoja wao na bila kutumia alama za kisiasa na wakitumia haki yao ya kikatiba ya kutoa maoni waliamua kukusanyika pamoja ili kwenda kutoa sauti yao mbele ya viongozi wa kisiasa na wale wa polisi wa mkoa wa Ruvuma. Hata hivyo, badala ya uongozi huo kuweka utaratibu wa kusikiliza maoni na kilio cha wananchi hao, jeshi la polisi liliamua kuwatawanya kwa kutumia nguvu. Ni katika mazingira hayo taarifa za awali zinaonesha watu wawili walifyatuliwa risasi na kufa papohapo na mwingine mmoja kufa baada ya kuanguka katika pikipiki akiwakimbia polisi.

Hii si mara ya kwanza kwa askari wetu kuwa wepesi wa vidole kutumia risasi kushambulia wananchi wasio na silaha ambao nguvu yao kubwa ni sauti na kelele.

Kamisheni ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ina mifano ya kutosha ya jinsi jeshi hili lilivyokosa mafunzo ya kuelewa dhana ya haki za raia na haki za binadamu.

Kinachoonekana mara nyingi ni kuwa jeshi hili linajali zaidi haki ya watawala kutawala bila kubughudhiwa na halijali kabisa manung'uniko ya wananchi juu ya watawala hao. Tumeyaona haya Nyamongo, tumeyaona Mbeya, Arusha, Mwanza, Mwembechai, Pemba na sasa yametokea Songea.

Ni kwa sababu hiyo sisi kama chama cha siasa ambacho kinaongozwa na dhana ya kujali haki za wananchi na za binadamu, pamoja na kuitaka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kuchunguza kadhia nzima hiyo, tumeazimia kulishtaki jeshi la polisi ili lijifunze kuheshimu haki za binadamu.

Tunapendekeza pia uchunguzi huru kuhusu swala hili ufanywe mara moja chini ya tume ya haki za binadamu na utawala bora na kuona ni kwa jinsi gani jeshi la polisi lilishindwa kushughulikia malalamiko na manung'uniko ya wananchi kwa namna ya hekima na weledi likihakikisha maisha ya wananchi yanakuwa salama na mali za umma zina kuwa salama. Ni kwa sababu hiyo tunapendekeza Kamisheni za haki za binadamu iwachunguze:

a. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Michael Kamhanda na kuona ni kwa namnagani ameshughulikia malalamiko ya wananchi na jinsi gani alihusika katika kuwapa askari wa chini ruhusa ya kutumia nguvu kubwa dhidi ya kundi dogo la wananchi wasio na silaha. Vile vile kauli zake mara baada ya tukio hilo zichunguzwe ili kuona ni kwa kiasi gani zilikuwa na ukweli? Je ni kweli wananchi walitaka kuvamia Ikulu na kituo cha polisi?

b. Kama waandamanaji hawa wengi walikuwa kwenye pikipiki ni kwa vipi waliweza kuwa tishio kwa polisi waliokuwa kwenye magari na silaha? Ni wazi – kiakili tu – waliokuwa wanaendesha pikipiki wasingeweza kuwa wameshikilia silaha mikononi wakati huo huo! Je ni kweli walikuwa tishio kwa polisi kiasi cha kutawanywa kwa nguvu za silaha za moto?

c. Kauli za Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Mwambungu zina ukweli kiasi gani kuwa polisi waliwaua wananchi hao walipokuwa wakijaribu kuwatawanya wananchi waliokuwa wanaandamana kuelekea kwenye majengo ya serikali (waandamanaji walikuwa katika pikipiki!)

d. Kwa vile kamisheni hiyo inazo rekodi za kutosha tu kuhusu kuteswa kwa raia mikononi mwa polisi. Kama ilivyo kwenye ripoti ya mwaka 2007/2008 ambapo tume ilichunguza jinsi mahabusu 17 walivyo kufa kwa kukosa hewa wakiwa mikononi mwa polisi kule Mbeya. Taarifa hiyo na nyingine za baadaye zimeonesha kuwa vipo vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa raia mikononi mwa polisi. Tunapendekeza kamisheni hiyo ifanye ziara ya mara moja ya kukutana na wananchi hawa zaidi ya hamsini ambao wanashikiliwa na polisi ili kuhakikisha haki zao za msingi za kiraia na kibinadamu hazikiukwi au wao wenyewe kutishwa wasiweze kusema ukweli wa kile kilichotokea wakiogopa kulipizwa kisasi.

e. Kamisheni pia imhoji hadharani Kamishna wa Mafunzo wa Jeshi la Polisi Kamishna Paul Chagonja juu ya mafunzo ambayo polisi wetu wanapewa na kumtaka asihusike na uchunguzi wa ndani wa polisi hasa kwa vile tayari ameshatoa hukumu hadharani kuwa mkusanyiko wa wananchi wale mjini Songea ulifanywa na wahuni. Mtu ambaye anaona raia wenye kulalamikia watawala ni wahuni hawezi kuwatendea haki; atapendelea jeshi lake na askari wake badala ya haki za binadamu na raia.

f. Kamisheni imhoji vile vile Inspekta Jenerali wa Polisi Bw. Said Mwema kwani chini ya utawala wake tumeshuhudia mara kadhaa polisi wakiua wananchi na kuvunja haki mbalimbali za raia na kumtaka atoe maelezo au aachie ngazi. Haijalishi kama yeye ni shemeji ya Rais au vinginevyo haki za raia ni za msingi na hazipaswi kuchezewa na mtu yeyote.


Ikumbukwe kwamba wakati huu Taifa letu linapitia kipindi kigumu cha wananchi wetu kuamka kisiasa na kutambua haki zao zaidi na zaidi. Tumeshaona katika nchi nyingine ambapo watawala walidhania risasi na vifungo vinaweza kulazimisha wananchi kupiga magoti na wakajikuta wao ndio wanapigishwa magoti. Tusiache taifa letu litawaliwe kama wakati wa wakoloni ambapo wananchi walikuwa wanaogopa jeshi la polisi na hata kushindwa kulipa ushirikiano na jeshi lilijiona liko juu ya wananchi.

Ni matumaini yetu kuwa hatua hii ya kulipandisha jeshi hili kizimbani litakuwa ni tukio la kihistoria katika kuitikia wito wa kutetea haki za wananchi wetu kabla wananchi wenyewe hawajaamua kutetea haki hizo kwa namna ambayo hatujawahi kuiona katika taifa letu.


Constantine Akitanda
Mwenyekiti Taifa
Chama cha Kijamii
 
Download hapa taarifa ya Cha Cha Kijamii kwa vyombo vya habari kuhusiana na mauaji ya watu wasio na hatia.
 

Attachments

  • TAMKO CCK.doc
    66.5 KB · Views: 82
Nachukia sana pale wanasiasa wanapobaka maudhui ya wananchi na kujifanya ni ya kwao! Tabia hii ya kujitafutia umaarufu wa kisiasa yanadunisha upatikanaji wa haki za wananchi. sson litakua jambo la CCM na upinzani na hapo ndo haki za waliouliwa zitakapopotea.
 
vipolisi vya tz sijui wanamaisha gan mazuri kiasi cha kunyanyasa raia kiasi hiki utazan wamemaliza kil kitu kumbe wamejaa dhiki was*** ka nin!

NAONA CCK WAMEPATA MAHALI PA KUJITANGAZA NDIO WACHANGAMKIE SASA.
 
Kwa kweli ni kauli kali na ya kuunga mkono kutolewa na wanaharakati na CCK; natumaini kweli watafungua kesi dhidi ya Jeshi la Polisi kwa mauaji haya.
 
Back
Top Bottom