Wanahabari mpo? niwekeni sawa na katika hili,,

WJN

Member
Nov 6, 2010
54
0
Ni matumaini yangu m-wazima wana jf! Leo naomba fahamu tofauti iliyopo kati ya 'REUTERS' na 'BBC',
 
Ni matumaini yangu m-wazima wana jf! Leo naomba fahamu tofauti iliyopo kati ya 'REUTERS' na 'BBC',

Du mkuu kama kweli umeweza kuwa member wa JF na hujui tofauti kati ya BBC na Reuters ni kitu cha ajabu sana. Kama kweli huelewi basi inabidi nizna kwa kuelewesha kwa mfano rahisi kabisa.

BBC ni shirika la Utangazaji ambao hapa kwetu ni sawa kidogo na TBC au RTD ya zamani. Lakini inafanana zaidi na TBC yapo haziko sawa.

Rueters ni shirika la habari amabalo kazi yake ni kuuza habari (video, text, sauti etc) Naweza kuifananisha kidogo na ile tuliyokuwa tunaiita shihata, lakini tofauti ni kuwa Shihata ilikuwa ya serikali na ilikuwa haifanyi biashara.
 
Bongolander,

Acha kejeli bwana, kwani kuna mtihani kujiunga na JF? Hapa kuna watu wa kada mbali mbali na taaluma mbali mbali. Sio kila mtu anajua mambo ya sekta ya habari, na hakuna kigezo cha kwamba ujue vitu fulani fulani kabla ya kujiunga na JF.

Ila ni vizuri kwamba mwisho wa siku umetoa jibu ambalo naamini muuliza swali litamfaa.
 
Back
Top Bottom