Wanagawana roho

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,848
2,669
Hapo Tanga pana makaburi ya misheni yaliyozungushiwa uzio. Nje ya uzio pana mlinzi mzee hivi anayelinda misalaba na mashada. Jirani yake pana shamba la misheni pia la minazi. Vibaka wa2 walifika hapo mida mibaya kuiba nazi. Walipoangua za kutosha wakaziweka juu ya turubai na kuanza kuziburuta kuelekea makaburini kugawana. Nazi 2 zilianguka pale getini ila hawakuzichukua. Bahati yao mlinzi alikuwa anakoroma. Hawakwenda mbali na getini wakaanza, 'hii yangu hii yako...' muda si mrefu mlinzi akagutuka akawa anasikia, 'hii yangu hii yako...' hakuelewa somo hivyo akatoka nduki hadi kwa mchungaji anayeishi mita 150 tu toka pale. Akamweleza hali halisi. Naye mchungaji kwa mawenge ya usingizi akamwambia, bila shaka Mungu na shetani wanagawana roho. Twende!

Walipofika kila mmoja akakaa upande wake wa geti wakawa wanasikiliza. Vibaka walipomaliza, mmoja akamwambia mwenzie, 'kuna zile 2 pale getini. Moja yangu moja yako.' sikujua kilichoendelea
 
This is deadly...nimecheka sana...hahahahahaha....mbio walizozipata nadhan visigino vilikuwa zinagonga visogoni...
Hapo Tanga pana makaburi ya misheni yaliyozungushiwa uzio. Nje ya uzio pana mlinzi mzee hivi anayelinda misalaba na mashada. Jirani yake pana shamba la misheni pia la minazi. Vibaka wa2 walifika hapo mida mibaya kuiba nazi. Walipoangua za kutosha wakaziweka juu ya turubai na kuanza kuziburuta kuelekea makaburini kugawana. Nazi 2 zilianguka pale getini ila hawakuzichukua. Bahati yao mlinzi alikuwa anakoroma. Hawakwenda mbali na getini wakaanza, 'hii yangu hii yako...' muda si mrefu mlinzi akagutuka akawa anasikia, 'hii yangu hii yako...' hakuelewa somo hivyo akatoka nduki hadi kwa mchungaji anayeishi mita 150 tu toka pale. Akamweleza hali halisi. Naye mchungaji kwa mawenge ya usingizi akamwambia, bila shaka Mungu na shetani wanagawana roho. Twende!

Walipofika kila mmoja akakaa upande wake wa geti wakawa wanasikiliza. Vibaka walipomaliza, mmoja akamwambia mwenzie, 'kuna zile 2 pale getini. Moja yangu moja yako.' sikujua kilichoendelea
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom