Wanafunzi zaidi ya 50 UDSM wafukuzwa moja kwa moja!

Lazima mfanye maamuzi magumu.UDSM hamjawahi kushindwa,hili pia mtashinda.tutawaunga mkono kwa namna yeyote,anzisheni spesho thread humu tuwe tunapata maendeleo ya kuwakomboa wenzenu.
 
waliofukuzwa walijitoa kwaajili yenu,msiwatupe kipindi hiki! Tumieni vizuri facebook kupanga mikakati mpaka wenzenu warudishwe! Tumieni teknolojia kumobilize wanafunzi wote.
 
The government is insecure and has decided to be oppressive in response. I wonder why the annually Human Rights report done by LHRC are not taken into consideration.

Oops. Does the gavoo listen anyway? Poleni sana

Adhabu za tatu na ya nne hakika zimekaa kiuonezi sana na ni kinyume cha sheria na Katiba.

It is high time wanaharakati walipinge hilo kwa kila hali.
 
Kuna thread imeandikwa hata jana iliyokuwa na kichwa "nguvu ya umma ya shinda". Inazungumza tofauti kabisa na hii stori. Sasa sijui ukweli ni upi. Na kama kuna uongo, ni kwasababu gani? Tena kwa wasomi!?

Ngachoka kapsaa!
 
Ni muda mfupi ulio pita,wana UDSM tukiwa tunafurahia pesa kutolewa maarufu kama boom,chuo kimetoa maamuzi ya kuwafukuza chuo moja kwa moja wanafunzi wote waliohusika na kuhamasisha mgomo.
Ni takribani wiki tatu sasa,hali ya UDSM imekuwa tete,baada ya wenzetu kusimamishwa masomo kwa kosa la kudai mikopo kwa mwaka wa kwanza walio kosa!
Nawapa ushauri wa bure vijana mnaosoma UDSM nilitegemea mkidumishe chuo kuwa center of exellence kwanza kwa kusoma kwa bidii sana baada ya kugundua kuwa serikali haina mpango na ninyi hata kidogo na pia wakufunzi wenu wamekatishwa tamaa na masilahi kidogo sana wanayopata na kuamua kuishia kwenye consultance na siasa ili mpate elimu yenye kiwango cha juu mwende zenu ugwaibuni kufanya kazi maana mpango wa serikali ni kuwachanganya muwache kusoma ili wale watoto wao wanaosoma ngambo wakirudi mshindwe kukabiliana nao kwenye interview. mimi wakati wangu wa elimu ya juu nilihakikisha hakuna mtu anayegoma. tulitumia kila ushawishi kuzuia migomo .baada yamasomo tukasepa tukaenda kufanya kazi kwa wale waliokuwa wanahitaji wataalamu - naomba tujaribu kuielewa serikali yetu na tuchukue hatua za kujisaidia wenyewe jamani.
 
hayo siyo maamuzi magumu,ni maamuzi ya kukomoana,kwa polisi kulinda hizo sehemu ni kawaida hata wale wanaosoma nje ya Tz utayaona hayo,polisi ndio wanaofanya kazi ya ulinzi ktk mazingira ya chuo hakuna mambo ya urinzi wa kimasai na magari ya polisi huzunguka mda wote vyuoni
 
hao walotoa maamuzi wana fikra fupi kama mkia wa sungura!
ngoja miaka 3 ipite watavuna walichopanda!
 
sasa hapo chuo si kinaanzisha mgogoro mwingine? maana watagoma tena mpaka wenzao warudishwe
 
Tatizo nyie wadogo zetu siku hizi mnadhalilisha sana Chuo chetu. Migomo yenu haina nguvu kabisa na ndiyo maana watawala wa Chuo wanafanya haya. Juzi juzi tu nimepita nikakuta mara wengine wapo kwenye Kunji, wengine wapo kule SR (Semina Rooms), wengine library, Wengine Hill Park wanalewa, nk. Katika hali kama hii ya kugawanyika ni vigumu sana mkawashinda hao watawala. Nendeni mkawachape bakora wote wanaowasaliti popote pale walipo ili chuo kisitawalike!. Lakini nawaambieni hakuna Watawala wa Chuo waoga kama wa UDSM. Mkipiga Kunji la nguvu siku 3 mfululizo lazima wawasikilize.
 
Uwendawazimu!Mtoto akinyea nguo unakata makalio... huo ndiyo uamuzi wa kifisadi. Nchi hii inaendeshwa kidikteta hata kama inajitangazia ni nchi ya kidemokrasia. Ni jeshi tu liwezalo kufanya mambo ya namna hiyo kwenye karne hii. Mtaendelea kuwatisha watu wenu mpaka lini hasa pale wanapodai haki zao? Mngekuwa mnafanya hivi kwa mafisadi kusingekuwa na ufisadi hasa wa mikopo. Kauli yangu: Huu ni uonevu wa serikali kwa raia wake. Sijawahi kuona serikali dhalimu namna hii...ukidai haki unaitwa adui, ukiiba, unaitwa mwema. Yana mwisho haya.
 
Hii lazima itakua UDSM.

Ila nafikiri nyinyi hamjui maana ya Kunji. yaani hamuwezi pata haki yenu bila Kunji ka maana.

Nafikiri wewe unaishi nje ya nchi tena kwa muda mrefu sasa - kunji lilikuwa linafanya kazi wakati ule ambapo TZ kulikuwa na vyuo 2 tu UDSM na SUA tuu sasa hivi kuna vyuo mpaka vingine vinaitwa MOM na JORDAN wasipoangalia hicho chuo cha UDSM kinaweza kufungwa kabisa NA najengo yake kukabidhiwa kwa SHOPRITE kupanua biashara ya supermarket na kumbi za starehe!!!!! serikali ya sasa imedata ndugu zangu ..............waswahili wana msemo usemao ukicheza na masaburi yatakupaka mavi ,,, haya wanafunzi tafakarini na mfanye maamuzi yanayowasaidia - nawatakieni kila la heri
 
Nawapa ushauri wa bure vijana mnaosoma UDSM nilitegemea mkidumishe chuo kuwa center of exellence kwanza kwa kusoma kwa bidii sana baada ya kugundua kuwa serikali haina mpango na ninyi hata kidogo na pia wakufunzi wenu wamekatishwa tamaa na masilahi kidogo sana wanayopata na kuamua kuishia kwenye consultance na siasa ili mpate elimu yenye kiwango cha juu mwende zenu ugwaibuni kufanya kazi maana mpango wa serikali ni kuwachanganya muwache kusoma ili wale watoto wao wanaosoma ngambo wakirudi mshindwe kukabiliana nao kwenye interview. mimi wakati wangu wa elimu ya juu nilihakikisha hakuna mtu anayegoma. tulitumia kila ushawishi kuzuia migomo .baada yamasomo tukasepa tukaenda kufanya kazi kwa wale waliokuwa wanahitaji wataalamu - naomba tujaribu kuielewa serikali yetu na tuchukue hatua za kujisaidia wenyewe jamani.

Kabla ya kuandika jaribu kuelewa kinachozungumziwa.

Watasoma vipi ikiwa wamenyimwa mikopo? na wazazi wao hawana uwezo wa kuwalipia? bila shaka unazungumzia wakati ule ukishachaguliwa tu kuingia elimu ya juu una uhakika wa kulipiwa na serikali, ingawa hata kipindi hicho migomo ilikuwepo.

Kwa serikali hii tuliyonayo, inayoona ni busara kuongeza posho za wabunge kwa ajili ya kukaa tu na wengine kwa kusinzia bungeni kuliko kusomesha wananchi wake, migomo tu ndio silaha ya mwisho na inayoifanya isikie.
 
walichokuwa wanakitafuta sasa wamekipata, hivi udsm hamuwezi kukaa na uongozi mkazungumza...?? kwa nini ninyi kama wasomi mumekaRiRishwa njia moja tu ya kutatua matatizo yenu (yaani migomo)...?? hamjajifunza njia zingine za kutatua matatizo yenu..??basi njia mmoja wapo ni mazungumzo

waliofukuzwa chuo tunawakaribisha hapa kijijini kwetu BUSEGA tuendelee na kilimo kwanza, kumbukeni huu ni msimu wa mvua, karibuni sana...
 
Uwendawazimu!Mtoto akinyea nguo unakata makalio... huo ndiyo uamuzi wa kifisadi. Nchi hii inaendeshwa kidikteta hata kama inajitangazia ni nchi ya kidemokrasia. Ni jeshi tu liwezalo kufanya mambo ya namna hiyo kwenye karne hii. Mtaendelea kuwatisha watu wenu mpaka lini hasa pale wanapodai haki zao? Mngekuwa mnafanya hivi kwa mafisadi kusingekuwa na ufisadi hasa wa mikopo. Kauli yangu: Huu ni uonevu wa serikali kwa raia wake. Sijawahi kuona serikali dhalimu namna hii...ukidai haki unaitwa adui, ukiiba, unaitwa mwema. Yana mwisho haya.

Acha upumbavu mdau aliye kuambia watoto wa serikali wapo UDSM ni nani??? kama ni watoto basi ni watoto wa kambo ambao huwa wanakula makombo siku zote ...... mimi nafikiri watoto wa ndoa wa serikali yetu ambao daima watakula hata kile ambacho sii haki yao ni vyama vya siasa na ruzuku zao za kila mwezi na waheshimiwa wabunge na posho zao zinazoongezwa kwa nguvu kila mara hata kama hawazitaki.
 
Kuna thread imeandikwa hata jana iliyokuwa na kichwa "nguvu ya umma ya shinda". Inazungumza tofauti kabisa na hii stori. Sasa sijui ukweli ni upi. Na kama kuna uongo, ni kwasababu gani? Tena kwa wasomi!?

Ngachoka kapsaa!

Hata mie naona hapa jf panataka kuwa kama facebook,jana uzi wa kwanza ulikuwa wamekinukisha,baadaye nguvu ya umma imeshinda sasa hivi tena sad news!?!
 
unaandika kama umetoka kupata uhuru jana. Au haujui tz kuna vyuo vingi

mkuu hili suala ni toka juzi na watu walishatupia sana humu kwaiyo mimi nilichokifanya nikutoa update ya leo.. wakati tamko la VC lajuzi baada yakugoma na kuzuia UTAWALA alitoa tamko lakuwarudisha wale 35 na kuwasuspend wale 8, vijana walizidi kushinikiza mgomo wakitaka hata wale 8 warudi.. ilivyofika saa mbili usiku VC akatoa tamko lakurudisha hata wale 8, kumbe ilikuwa changa la macho akitafuta pakutokea na USIKU wa jana ndo inatoka sad newz kama nilivyopost..na sijarudia kuhusu mgomo maana ni mgomo wa tar 11/11 nikiamini kila mmoja anajua juu ya wale waliokamatwa na tatizo lilikuwa ni nini(KUTETEA WATOTO MASKINI 1st WALIOSHINDWA KUENDELEA NA MASOMO KWASABABU YA "NO LOAN" wakati mke wa LIZIWAN KIKWETE akiwa na 100% UDOM) mgomo ulikuwa wa amani kabisa sema ndo vile
 
sad newz...
utawala wa chuo umefanya maamuz ya kutisha!!!!
1.wanafunz 8 waliokuwa-suspended wamefukuzwa chuo kabisa....
2.wanafunzi 35 wenye kesi mahakamani wamefukuzwa chuo kabisa...
3.wanafunz waliofukuzwa chuo kutodahiliwa chuo chochote cha umma na kunyimwa mkopo maishan mwao mwote....
4.maeneo muhimu ya chuo kama vile cafeteria,lecture rooms,library nk kulindwa na polisi.....
je tutafika???????

Hapa watakuwa wamekandamiza haki za binaadamu na hata kuvunja katiba. Tushukuru Mungu kuwa wakati huu angalau kuna vyuo vya private.

Hii adha ya kuwazuia watu kusoma ilitumika sana na Nyerere dhidhi ya kabila fulani la kaskazini. Wakati ule watu wa kabila hilo walipewa quota ndogo sana ya viti vya sekondari. Kwa sababu serikali ilikuwa imetaifisha shule zote, hawa wahanga hawakuwa na alternative yoyote bali kutafuta maisha vingine. Wengine walibadilisha majina na kuhamia mikoa ya pembezoni warudie shule, wengine walichukua ajira zilizo nje ya taratibu zinazokubalika na wengine wengi kuhamia Kenya.

Lakini pamoja na yote, hauwezi ukakandamiza utashi wa binaadamu. Hili kabila lilikuja kuongoza kujenga shule za private na hata kabla ya watawala kuleta dhana ya shule za kata, huo mkoa ulikuwa na shule kadhaa katika kila kata - tena za maana, zinazofaulisha. Leo hii, watu wenye kuona mbalia, wanawatoa watoto wao kwenye shule kubwa za serikali na kuwahamishia kwenye hizi shule.
 
Back
Top Bottom