Wanafunzi wawili wa kike watelekezwa 'guest'

charger

JF-Expert Member
Nov 21, 2010
2,320
1,369
Habari zenu wana JF,
hivi kizazi hiki kinaelekea wapi jamani ?nimekutana na habari hii nikaona niwape mtafakari na nyie.

WANAFUNZI wawili wa kike wa kidato cha pili katika sekondari ya Enyeitu mkoani Arusha, wametelekezwa katika nyumba ya kulala wageni Dar es Salaam kwa mwezi mmoja sasa.

Wasichana hao wakazi wa Mianziani, Arusha, walifika Dar es Salaam Juni 4 wakifuatana na mwanamume anayejulikana kwa jina la Rwaka au Swai.

Mwanamume huyo aliwafikisha katika nyumba hiyo ya Flamingo iliyopo Nzasa A Mbagala katika wilayani Temeke.

Wanafunzi hao Neema Abel (17) anayedai anaishi na mjomba wake, Amos Michael na Tatu Salim (16) aanayeishi na dada yake Aisha Salim, walifika katika nyumba hiyo siku hiyo saa nane usiku na kupokewa na mhudumu Zainabu Abdallah.

Mwandishi wa habari hizi alifika katika nyumba hiyo ya kulala wageni juzi na kuwakuta wanafunzi hao wamekaa nje kama wapo nyumbani tena wakicheza bao na baadaye akazungumza nao.

Awali, mhudumu huyo alidai kuwa mwanamume huyo aliwaandika katika daftari la wageni wanafunzi hao kuwa ni Aisha Salim (Tatu) na Angela Amos (Neema) ambaye alidai mwanamume huyo ni baba yao mdogo na walifika naye jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutembea.

Alisema, baba huyo alikuwa akifika kila siku katika nyumba hiyo na kuwapa fedha za chakula na kulipia gharama ya chumba namba nane walichokuwa wakiishi kwa wiki tatu.

Zainabu alisema, baadaye walishangaa kutomwona huyo mtu na hivyo wasichana hao wakashindwa kulipia chumba na chakula ndipo wakafichua kuwa hakuwa baba yao na amewatelekeza na wanadaiwa Sh 35,000 za chumba.

Mabinti hao wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, walidai kuwa, mwanamume huyo ambaye ni mtu wa makamo, alikutana nao Arusha na kuwa marafiki wa kawaida.

Tatu alisema, baada ya kufunga shule, baba huyo aliwaambia waje Dar es Salaam kuona mji, ndipo naye akamtafuta rafiki yake, Neema, ambaye wanasoma wote shule moja na kutorokea Dar es Salaam.

Alisema, walipofika jijini, mwanamume huyo aliwaambia waseme kuwa ni baba yao mdogo na kuwaacha kwenye nyumba hiyo naye akaenda kwa mkewe, na akawa akifika mara kwa mara akiwa na rafiki yake na kuwaachia matumizi.

Alisema, siku moja alifika na kumtaka kimapenzi alipokataa, ndipo alikawaambia kuanzia siku hiyo watajua wenyewe watalala wapi, kula wapi na hata nauli ya kurudi Arusha.

Alisema, kuanzia siku hiyo wamekuwa wakipika chakula pamoja na wahudumu wa nyumba hiyo, huku bado wakiwa na deni la Sh 35,000 na bila kusema fedha wanazochanga kwa ajili ya chakula wanazipata wapi.

Angela alisema, wanachohitaji sasa ni nauli ya kuwarudisha Arusha, ili kuendelea na masomo, kwa kuwa shule wanayosoma ilifunguliwa jana na wamejifunza kutokana na makosa waliyofanya.

Baadhi ya wafanyakazi wa nyumba hiyo, walidai wasichana hao walisitishiwa huduma baada ya mwanamume huyo kuwakuta wakiwa na vijana wadogo na baada ya kusitishiwa huduma, wamekuwa wakitoka usiku na kwenda kwenye kumbi za starehe ili kupata fedha za kujikimu.

Source:Habari leo 11th JULY 2011

 
1.Hawa wanamiaka chini ya 18 ni watoto
2. Ni wanafunzi
Huyu baba akamatwe kwa kuwalaghai watoto na kuwatelekeza
Ashitakiwe kwa mujibu wa sheria za TZ
 
Hawa watoto ni viwembe, kuna mengi wanafanya na hilo Fataki lao bt wanaficha! Tamaa mbaya!
 
Watoto wa siku hizi wana tamaa sana. Hii ni dalili kuwa maadili yetu yanakufa maana Wazee ambao ndio wanatakiwa kuwaongoza wanakuwa ndio waaribifu wakubwa wa hao watoto.
 
Jamani watoto wasikuizi hawana uwoga hata kidogo,na huyobabu mtu mzima fisadi anataka kuwafisidi watoto loh,
 
Ewe Mungu walinde wadogo,watoto wetu ni nini hichi jamani?waeza kuta wala hawana shida yoyote wamesikia kuja kutembezwa jijini wakachanganyikiwa.
 
Ok, hii habari niliisikia pia but mimi nawalaumu hawa watoto kwa kupenda vitu vya cheee, well najua mwaweza kuni-challenge but I have been teaching, I know wanafunzi walivyo, huwa nashangaa hata serikali ikipiga makelele eti walimu wanawapachika mimba wanafunzi......hebu imagine unafundisha mtoto wa kike kakukalia uchi, maziwa nje! Narudia kusema kwamaba naongea kitu ambacho nimekuwa nikikishuhudia kwa macho yangu, well najua wanafunzi wangu watakua wananimisi baada ya kauchana na Ualimu (kuasi taaluma) maaana binti akinikalia uchi nilikua namwambia kabisa kwamba fulani naomba ufunge duka lako.....yes, I did it. Sasa akitokea mtu mwingine ataona ndio nafasi ya kuvitafuna maana katoto ni kazuri mbaya halafu kanakufuata eti kanaomba nauli au umsaidie swali wakati mko wawili tu halafu angalia kanavyrembua na mapozi ya ajabu ajabu.....Namkumbuka sana Baba yangu siku moja alisema hivi: Tusimlaumu Chui peke yake, tumlaumu na Mchunga mbuzi pia.
Any comment? nipo tayari kutoa ufafanuzi na experience binafsi kuhusu wanafunzi hasa hawa wa Mjini....challenge me then
 
Yaani mi nashindwa hata nisemeje jamani, sio siri imenisikitisha sana. 16, 17 yrs of age.....binti anajiuza!! Kweli mi namlaumu huyo baba, bora hata angewarudisha au angewataarifu ndugu zao sio lazima kujitaja kuwa ye ndo amewarubuni basi tu taarifa ingewasaidia.
 
Vischana vingi kuanzia miaka 14,15 na kuendelea viko moto chini kutwa kwenye mitandao na simu kutafuta mafataki na kwa kuwa vyakula vya siku hizi mafuta mengi na dawa za wachina kungeza maumbile vimenenepeana utafikiri watu wazima
 
Watoto wadogo wanajiaibisha. Wazee wazima nao mishipa ya aibu ishakatika.
 
Ok, hii habari niliisikia pia but mimi nawalaumu hawa watoto kwa kupenda vitu vya cheee, well najua mwaweza kuni-challenge but I have been teaching, I know wanafunzi walivyo, huwa nashangaa hata serikali ikipiga makelele eti walimu wanawapachika mimba wanafunzi......hebu imagine unafundisha mtoto wa kike kakukalia uchi, maziwa nje! Narudia kusema kwamaba naongea kitu ambacho nimekuwa nikikishuhudia kwa macho yangu, well najua wanafunzi wangu watakua wananimisi baada ya kauchana na Ualimu (kuasi taaluma) maaana binti akinikalia uchi nilikua namwambia kabisa kwamba fulani naomba ufunge duka lako.....yes, I did it. Sasa akitokea mtu mwingine ataona ndio nafasi ya kuvitafuna maana katoto ni kazuri mbaya halafu kanakufuata eti kanaomba nauli au umsaidie swali wakati mko wawili tu halafu angalia kanavyrembua na mapozi ya ajabu ajabu.....Namkumbuka sana Baba yangu siku moja alisema hivi: Tusimlaumu Chui peke yake, tumlaumu na Mchunga mbuzi pia.
Any comment? nipo tayari kutoa ufafanuzi na experience binafsi kuhusu wanafunzi hasa hawa wa Mjini....challenge me then

Kama mwalim uliye matured ni bora ukaelewa kuwa watoto wanapofikiaumri fulani wanakuwa na mambo mengi ya kuashiria ngono.
Na si vizuri wewe ukajichukulia hiyo nafasi kwa kutokuelewa kwao.
Wengi ni wadogo hawana uwezo wa kupambanua bado wao wanaona dunia tamabalale .

Umri walionao ni mbaya wakudanganyana, kuiga na kujaribu kila jambo.
Eh MUNGU OKOA HILI KIZAZI KISIANGAMIE Maana watoto wengi cku hizi ni yatima wamekosa malezi bora
 
Inasikitisha sana! But funny enough kama wanaweza kuchangia hela ya chakula kwa nini hiyo hela wasingefanye ni nauli? kama mwamndishi wa habari hizi asingewagundua wangekaa kimya hadi lini? Na watapokelewa tena shuleni kweli?
 
Back
Top Bottom