Wanafunzi Wavamia Tume ya Vyuo Vikuu - TCU

SuperNgekewa

Member
May 10, 2010
49
3
WANAFUNZI WAVAMIA TUME YA VYUO VIKUU



Baadhi wa wanafunzi wakiwa nje ya jengo hilo.

KUNDI la wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kujiunga na vyuo mbalimbali vya serikali na kupata alama za juu leo wamefurika nje ya Jengo la Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) lililopo Mikocheni jijini Dar es Salaam wakipinga uamuzi wa wenzao waliopata alama ndogo kupatiwa nafasi za kujiunga na vyuo vya serikali na wao kukosa nafasi na kudai uamuzi huo ni wa kuwaonea.




Askari wa jengo hilo akiinyoosha mkono kuwataka wanafunzi hao kukaa mbali na eneo hilo, amri waliyokataa kuitii.​





Muuza "lamba-lamba" (ice cream) akiwa kwenye mkusanyiko huo kukata kiu ya ‘madenti' hao.​




PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY
 
Nchi hii watu wanapata shida zingine kwa sababu watu wachache hawataki kufanya kazi zao inavyotakiwa. Its so sad kuona mtu kahangaika toka chini huko gizani anafika huku ndo wanamchanganya kwa kitu kidogo ambacho ni kumwelewesha mambo yanakuwa safi.
 
Jana na leo nimekuta vijana wengi hapo Tume ya Vyuo Vikuu. Hivi wanafanya nini hapo. Niliona kama vile wanafuatilia kitu. Sidhani kama ni mgomo tu ndio umewaleta hapo. Naomba ni fahamishwe zaidi.
 
Back
Top Bottom