wanafunzi watano wa chuo........!

Hapana,
najua hauwez tunga jambo la uwongo pasipo kujipanga.
Ni lazima walijipanga tu.

ngumu Madame B,
kumbuka waongo wengi wanakamatwa kwa kipengele kidogo sana
ukibisha nakuchapa FIMBO ya makalioni
 
Last edited by a moderator:
kama ni mimi nazuka na uongo mpya hapo hapo fasta.nawapa ishara wenzangu tumwambie lecturer kuwa macho yetu yameacha gafla kuona vizuri, halafu wakati wa kutoka chumbani tunajifanya kupapasa mlango!
 
Wanafunzi watano wa chuo kikuu kimoja
hapa nchini walikuwa wanatakiwa
wafanye mtihani siku ifuatayo. Wale
wanafunzi wakanywa pombe mpaka saa
nane usiku. Siku ya mtihani wote wakawa na uchovu
wa hangover,hivyo wakashindwa kwenda
kufanya mtihani. Wakatunga uongo wa kuenda
kumwambia Lecturer wa somo
husika.Wakaenda kumdanganya Lecturer
kuwa walishindwa kufanya mtihani kwa
sababu jana walienda harusini na wakati
wanarudi gari lao likapata pancha na wakavamiwa na majambazi wakawapiga
na kuwaibia. Yule Lecturer akakubali na akawapa siku
tatu za kujiandaa kwa Special exam. Siku ya mtihani special,Lecturer aliwapa
ma paper na kuwasimamia mwenyewe.
Mwongozo wa mtihani ulikuwa kama
ufuatavyo; 1.Mtihani huu ni kwa wanafunzi watano. 2.Majibu yao yote yafaa yawe
sawa...yakiwa tofauti watapata zero na
kufeli. 3.Mtihani huu una maswali matano na
yote lazima yajibiwe. Maswali ya mtihani yalikuwa hivi: 1.Harusi ilifanyika sehemu gani?
2.Gari mliotumia mpaka mkapata pancha
inaitwaje?
3.Ajali ilitokea eneo gani?
4.Nani alikuwa dereva?
5.Tairi ipi ilipata pancha...ya mbele au
nyuma? NAWATAKIA MTIHANI MWEMA.
Mimi nlikua mmojawapo ya hao wanafunzi na hili ndilo lilikua jibu langu.
"ile pancha ilitoa mlio Mkubwa sana nikazimia kwa mshtuko, nikajikuta home"
 
Back
Top Bottom