Wanafunzi wahoji uhalali tume Bodi ya Mikopo

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Wanafunzi wahoji uhalali tume Bodi ya Mikopo


Na Tumaini Makene

WAKATI baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu wakihoji utaratibu uliotumika kuwapata wajumbe wa tume ya kuipitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa
Elimu ya Juu (HESLB), wengine wametoa tamko juu ya sababu za migogoro vyuoni na kusuasua kwa mwelekeo wa elimu nchini.

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (CKD) ambao hawakutaka majina yao yaandikwe gazetini, wamehoji uhalali wa wajumbe wa tume ya wataalamu 11 iliyoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kufanya mapitio ya mfumo wa uendeshaji wa Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (HESLB).

Wasiwasi wa wanafunzi hao juu ya ufanisi wa tume hiyo unatokana na madai kuwa baadhi ya wajumbe kuwa katika Bodi ya Wakurugenzi HESLB, hivyo kuwepo kwa mazingira ya mgongano wa maslahi.

"Prof. Wilbert Abel, ambaye ni Mkurugenzi Elimu ya Juu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ni mjumbe wa bodi ya wakurugenzi bodi ya mikopo, Prof. Makenya Maboko naye halikadhalika, wamemuweka pia Deo, ambaye alikuwa rais hapa UDSM na amekuwa akituhumiwa kwa kushiriki vikao kuridhia kupanda kwa karo chuoni."

"Sasa hii ina tofauti gani na ule msemo wa kiswahili, kuwa kesi ya Ngedere unaipeleka kwa nyani, unategemea kutakuwa na utendekaji wa haki hapo kweli," alihoji mmoja wa wanafunzi hao, walipokuwa wakizungumza na Majira.

Katika hatua nyingine, Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Kanda ya Kati ambao ni wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wametoa tamko wakisema kuwa bodi hiyo haipaswi kubebeshwa lawama zote huku upande wa pili wa serikali na uongozi wa vyuo vikuu, ukijivua kuhusika na migogoro vyuoni.

Katika tamko lao hilo walilotuma kwa vyombo vya habari, wanafunzi hao wamechambua matatizo ya mfumo wa ufadhili wa elimu ya juu, vyanzo vya migogoro ya wanafunzi na wahadhiri na utatuzi wa masuala hayo.

Wamesema serikali inapaswa kuweka bayana kuwa kuwaelimisha wananchi wake ni wajibu na haki yao ya kikatiba, huku wakitoa wito kwa Watanzania wote, bila kujali tofauti za kiitikadi kujua hilo na kulipigania, ili watoto wa watu maskini, wakulima na wafanyakazi nchini wapate elimu.

"Katika siku za karibuni kumekuwa na mifululizo ya migomo katika taasisi za elimu ya juu ambapo lawama nyingi zimeelekezwa kwa bodi ya mikopo ya elimu ya juu. Sisi vijana wa CHADEMA ambao ni wanafunzi wa vyuo vikuu kanda ya kati tumeonelea kuwa si vema tukakaa kimya na kushindwa kuchangia kuelezea walau kile tunachokifamau ili kuboresha mazingira ya elimu kwa Tanzania.

"Kwa mtizamo wetu sisi, tunaona kuwa tatizo hili lina mzizi wa udhaifu katika maeneo matatu. La kwanza ni bodi yenyewe, la pili ni la serikali yenyewe na mwisho ni tawala za vyuo husika.

Pamoja na suala hili la migogoro katika elimu ya juu, pia tumetoa tamko kuhusu matokeo ya kidato cha nne 2010 na unyanyasaji wa watoto," ilisema sehemu ya tamko hilo.

Wakizungumzia matatizo ya elimu ya juu nchini, kwa kuanzia na bodi ya mikopo, wanafunzi hao walisema kuwa matatizo ndani ya taasisi hiyo yamejengeka katika sehemu kuu tatu, wakizitaja kuwa ni;

Utambuzi wa uwezo wa familia ya mwanafunzi mhitaji mkopo, ucheleweshaji usiokuwa na maelezo mazuri (kama vile kupotea fomu au kukosewa majina) na kuwanyima mikopo wanafunzi wanaorudia mwaka au masomo.

Waliongeza kuwa mfumo wa utambuzi wa wanafunzi wahitaji, haujaweza kufanyika kwa namna iliyo sahihi, wakidai kuwa kuna wakati watu kutoka familia moja, waliotumia vigezo vya aina moja kuomba mkopo, wamekuwa wakipewa mikopo kwa viwango vya asilimia tofauti;

Huku pia wakitoa madai kuwa baadhi ya wanafunzi kutoka katika familia zenye uwezo wamekuwa wakipata mikopo kwa asilimia 100, wakati wale wanaotoka familia zisizokuwa na uwezo wakiambulia asilimia ndogo, kiasi cha kutoweza kumalizia

"Ucheleshwaji usiokuwa na maelezo mazuri labda kutokana na kupotea kwa fomu au kukosewa majina...Kumnyima mtu ambaye ana anarudia mitihani au anayerudia mwaka. Kupata supplementary au kurudia mwaka ni ajali ya kitaaluma ambayo haistahili adhabu yoyote," ilisema sehemu ya tamko hilo la vijana wa chama hicho, huku ikiongeza;

"Mfumo wa means test ni mbovu na haufai. Maendeleo
yanajionyesha kuwa umeshindwa kufanya kazi kwa ufanisi. Tunashauri uvunjwe kwani haufai na ni wa kibaguzi. Ni vema kuwa kama kuna mtu asiye na haja na mkopo atoe taarifa ili asipewe kabisa kwani kulipa mkopo ni wajibu.

"Bodi ya mikopo ipewe ushirikiano wa kutosha na usiosababisha lawama na serikali. Bodi hii ingepaswa ijengewe uwezo wa kufanya shughuli zake kwa ufanisi. Pia ipewe ushirikiano na tawala za vyuo katika kuhakikisha mawasiliano na wanafunzi yanaboreshwa.

"Bodi ipewe mawasiliano sahihi na vyuo husika. Mfano wa hili
ni upandaji wa ada na gharama zozote za masomo. Bodi ya mikopo imejitahidi sana na isibebeshwe lawama zote wakati ambapo serikali na tawala za vyuo zikijivua kuhusika na migogoro vyuoni.

Wakizungumzia juu ya matatizo ya serikali katika migogoro ya wanafunzi elimu ya juu na utoaji wa mikopo, wanafunzi hao walisema kuwa imekuwa ikiechelewesha kutoa fedha kwa bodi husika, kwa muda stahili na hivyo kuvuruga maendeleo ya kitaaluma ya wanafunzi, wakidai kuwa hiyo ni dalili ya kutoipatia kipaumbele elimu kwa ujumla wake.

Pia walisema kuwa serikali imejivua jukumu la kusomesha raia wake, wakisema kuwa hata sababu ya kuanzisha bodi ya mikopo inaonekana ni dalili za kujivua huko, huku pia wakidai kuwa serikali imekuwa ikiitumia bodi hiyo kisiasa.

"Serikali imeitumia bodi ya mikopo kama jimbo la uchaguzi. Serikali kwa sababu inazozijua ilikataa kutoa fedha mapema mnamo mwaka jana (2010). Kutokana na hilo taaluma imeathirika sana kwani tumepaswa kufanya masomo usiku na mchana kufidia muda uliopotea.

Kwa upande wa uongozi wa vyuo, wanafunzi hao walisema kuwa vyuo vingi vimekuwa vikichelewesha majina ya wanafunzi wapya na wanaoenda kwenye mafunzo ya vitendo kwenye bodi hivyo kuchelewesha mikopo. Pia kumekuwepo na ucheleweshaji wa matokeo ya wanafunzi bodi ya mikopo, hali inayosababisha fedha kutopelekwa mapema.

Vijana hao walipendekeza kuwa serikali inawajibika kuweka mazingira rafiki kwa watoto wa maskini wa Tanzania, ili waweze kupata elimu ya juu kwa ufanisi unaotakiwa.

"Haiingii akilini kuwa kuvunja bodi ya mikopo ndani ya serikali ile ile, utawala ule ule, na viongozi wale wale kutaleta tija katika mazingira yale yale. Tusipokuwa makini inawezekana kabisa kuwa kipya tunachokitarajia kikaleta kuleta shida zaidi kuliko kile cha zamani.

 
PHP:
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (CKD) ambao hawakutaka majina yao yaandikwe gazetini, wamehoji uhalali wa wajumbe wa tume ya wataalamu 11 iliyoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kufanya mapitio ya mfumo wa uendeshaji wa Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (HESLB).
 
Wasiwasi wa wanafunzi hao juu ya ufanisi wa tume hiyo unatokana na madai kuwa baadhi ya wajumbe kuwa katika Bodi ya Wakurugenzi HESLB, hivyo kuwepo kwa mazingira ya mgongano wa maslahi.
 
"Prof. Wilbert Abel, ambaye ni Mkurugenzi Elimu ya Juu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ni mjumbe wa bodi ya wakurugenzi bodi ya mikopo, Prof. Makenya Maboko naye halikadhalika, wamemuweka pia Deo, ambaye alikuwa rais hapa UDSM na amekuwa akituhumiwa kwa kushiriki vikao kuridhia kupanda kwa karo chuoni."
 
"Sasa hii ina tofauti gani na ule msemo wa kiswahili, kuwa kesi ya Ngedere unaipeleka kwa nyani, unategemea kutakuwa na utendekaji wa haki hapo kweli," alihoji mmoja wa wanafunzi hao, walipokuwa wakizungumza na Majira.

Hii inanikumbusha juu ya JK alivyoahidi kuteua tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya..............alidai atateua mwenyekiti wa tume hiyo ambaye amebobea kwenye sheria kama vile tatizo la tume za awali ilikuwa siyo kubobea kwenye taaluma hiyo..............

Bila ya kutoa fursa sawa kwa wote katika ajira zozote za umme tutaendelea kulia na tatizo la uongozi mbovu.................kwa sababu wateuzi hutanguliza masilahi binafsi..................................
 
Back
Top Bottom