Wanafunzi wahofia kukosa mitihani

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WANAFUNZI wa kidato cha sita, katika Shule ya Sekondari, Tosamaganga, mkoani Iringa, wamekubwa na hofu ya kushindwa kufanya mtihani wao baada ya shule hiyo, kukosa Sh13 milioni, kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya maabara na kemikali.

Wakizungumza na Mwananchi, wanafunzi hao wanaosoma masomo ya sayansi, walisema bila vifaa hivyo, haitakuiwa rahisi kwao kufanya mtihani huo, unaotarajiwa kuanza Februari 7 mwaka huu.

Waliiomba serikali kuwasaidia kama kweli ianatilia mkazo masomo ya sayansi ambayo wanafunzi wengi wamekuwa wakishindwa, kwa sababu ya kukosekana kwa vifaa vya maabara.

source Wanafunzi wahofia kukosa mitihani
 
Back
Top Bottom