Wanafunzi wa zaidi 1000 vyuo vikuu wajiunga na CCM

Hapa JF kuna unafiki wa hali ya juu kabisa. .....

Haya mambo ya kupondea JF yatakushinda. Unafiki kama upo hata wewe unao kwa vile ni mwana JF. hakuna unafiki wala nini ila hii mbinu yako ya kupondea JF kwa ujumla utachemsha. JF is here to stay so jiandae for a long bitter journey hapa.
 
Hapa JF kuna unafiki wa hali ya juu kabisa. Kila leo watu mnasisitiza uhuru wa kujieleza / kutoa maoni nakadhalika. Leo vijana wameamua kujiunga na CCM, mnawasema vibaya kana kwamba nyie ndiyo mlioshika funguo za uhuru wao. Kwenda CCM siyo njaa ni matumizi ya uhuru wao kama vile nyie mnavyotumia uhuru wenu wa kujieleza.

Mkuu punda kunani kuipondea JF kila mtundiko wako?
Kwanza ulianza kwa kuhoji credibility yetu, leo unahoji unafiki, kulikoni? Watu tuna fikira anuwai hapa.
Huo uhuru wa kutoa na/ama kupokea mawazo/maoni unaousema hapo juu ndio huo wanaoutumia hao wanaowashangaa wanafunzi wa vyuo kujiunga na sisiemu, sasa kosa lao lipi? Wanasema yale yaliyo moyoni mwao bila kificho. Kama wana mtazamo tofauti na unavyofikiri wewe basi ni halali yao, JF inaruhusu, na kama haitoshi katiba ya nchi inaruhusu jambo hilo! Wewe unaishi dunia ipi mkuu?Ndio jambo forums ilivyo, ina watu wa kila namna.
Hebu soma vizuri masharti ya kujiunga na JF pale ukurasa wa mbele, huenda ukaelimika na kuelewa hiki ninachokiandika hapa, kwa sababu wamefafanua kwa undani sana.
Tuendelee kulumbana!
 
nidhanivyo mimi ni kuwa Mzumbe university ina zaidi ya wanafunzi 3000, sua zaidi ya 3000, na dodoma kama 2000, hapo hujaweka vyuo vingine anbavyo idadi yake haijulikani.

sasa hiyo idadi ya wanafunzi 1000 ni ndogo sana ukizingatia kuwa sasa hivi kuna mwamko wa kujua kitu gsni kinaendelea.

ila basi tukiweza tuwe na wawakilishi kwa kula chuo wa JF ili tuone kama hawa wanafunzi wanaweza kujua nchi inavyoendeshwa.
 
Mkuu punda kunani kuipondea JF kila mtundiko wako?
Kwanza ulianza kwa kuhoji credibility yetu, leo unahoji unafiki, kulikoni? Watu tuna fikira anuwai hapa.
Huo uhuru wa kutoa na/ama kupokea mawazo/maoni unaousema hapo juu ndio huo wanaoutumia hao wanaowashangaa wanafunzi wa vyuo kujiunga na sisiemu, sasa kosa lao lipi? Wanasema yale yaliyo moyoni mwao bila kificho. Kama wana mtazamo tofauti na unavyofikiri wewe basi ni halali yao, JF inaruhusu, na kama haitoshi katiba ya nchi inaruhusu jambo hilo! Wewe unaishi dunia ipi mkuu?Ndio jambo forums ilivyo, ina watu wa kila namna.
Hebu soma vizuri masharti ya kujiunga na JF pale ukurasa wa mbele, huenda ukaelimika na kuelewa hiki ninachokiandika hapa, kwa sababu wamefafanua kwa undani sana.
Tuendelee kulumbana!

Mpashe huyu bwana, naona ameivalia njugu JF sana badala ya ku-deal na hoja za members, kwa msemo wa dada yetu mwafrika wa kike-"yatamshinda"!
 
(Kada smells the air)...then
sniffs, mhm,then he says !
I smell some MIPASHO HUMU NDANI !
 
Kama ni kweli alishindwaje kuwasaidia wanafunzi waliokuwa Ukraine tayari na walianza kusoma baada ya mwaka moja akawatelekeza. AIBU HIYO JK, WEWE ULISOMESHWA KWA PESA YA WALIPA KODI.

JK ndio kawaambia wahamie ccm ?
kamahajasema, basi acha vijana wafanye ile kitu roho inapenda !
 
Wangekuwa wamehamia upinzani hapo ingekuwa news au?

Anyway, wanafunzi wa vyuo vikuu huwa sielewi kabisa mambo yao.
Walivaa kijani na njano Diamond baada ya kufatwa na magari kutoka vyuoni, wakachukua kadi za ccm kibao, wiki iliyofuata walewale wakaandamana kwenda jangwani na kashfa kibao dhidi ya serikali kwa kushindwa kutekeleza habari yao ya mikopo.

Leo tena wanasifia na hapohapo anapouliza mtu asiyeridhishwa na mwenendo wa mikopo anashangiliwa, hiyo inatoa picha gani?

Na wao wameamua kuleta ushkaji na serikali ya kishkaji?

Mnyika, mbona kasomeshwa na ccm, na alikuwa ccm lakini kinyemela kahamia upinzani na haijawa big news, sio ndio hapo !!
 
Acheni jamani wajiamulie.

CCM hoyeee! CCM juu juu juu zaidi!

si ndio hapo ! jamaa vijana wana mawazo mazuri sana na wakaamua kufanya wanachoprefer, ccm in that sense !

wapinzani pia si wana wasomi wao, mnyika, na wengineo. halafu wanafanya bi dili wakati seif sharif hamad mwenyewe alikuwa ccm na kuhamia upinzania haikuwa ishu wala, ccm walikaa kimya ! lakini sasa akihama kiongozi toka upinzani kwenda ccm, basi watu wanasema kanunuliwa, inakuwaje hapa wakuu ? mie sielewi elewi !
 
bad news. we need a new technique to make these guys aware of themselves.

unataka kuniambia vijana wa chuo kikuu are not aware of themselves ???? wanaenda kufanya nini huko chuoni sasa ?

ohh, no nakataa, they are very much aware of themselves ndio maana wakaamua kujiunga na CCM !

CCM OYEEEEEEEEEEEEEEEEE !!
 
Hapa JF kuna unafiki wa hali ya juu kabisa. Kila leo watu mnasisitiza uhuru wa kujieleza / kutoa maoni nakadhalika. Leo vijana wameamua kujiunga na CCM, mnawasema vibaya kana kwamba nyie ndiyo mlioshika funguo za uhuru wao. Kwenda CCM siyo njaa ni matumizi ya uhuru wao kama vile nyie mnavyotumia uhuru wenu wa kujieleza.

babu unajua unachosema ni kweli usiopingika na kama mtu atakuwa against na wewe FINE ndio uhuru wa mawazo na vita vya fikra hivyo, UNAJUA HATA KUNA KIPINDI HAPA JF MEMBERS WA CCM WALIKUWA WANAONA AIBU KUJIONYESHA WAZI KWAMBA WAO NI CCM, SIMPLY BECAUSE WATAANZA KUNYOOSHEWA VIDOLE, lakini after we worked things out, sasa tupo kwenye LIMELIGHT !!

vijana wa chuo kikuu kama wamefanya decision ya kujiunga na ccm wanapaswa kupongezwa kwa maana wanajua nini sera za chama, nini chama kinasimamia, na hivyo kuendeleza libeneke watakalotuachia akina mzee malecela, kingunge na wengine !

kama mtasema JK aone aibu, pia vile vile mnapaswa kusema JK NYERERE aone aibu, maana nae alimtuma MSEKWA kutafuta vijana watakaojiunga na CCM kwa hiari yao, ndipo walipopatikana akina JK KIKWETE, NA EL !! mnaopinga vijana kujiunga ccm, mpo hapo ?
 
Jamani tulieni kidogo, hivi mtu akiamua kujiunga na chama anachokipenda ni kwa sababu ya njaa?!!! mbona huko CCM wapo maprofessa wengi wamepelekwa na njaa? Je Professa Wangwe ana njaa yoyote?...

Wametimiza haki zao jamani, tuwaache hao!!! naona FD amefurahi... sibiri sunami 2010,,, Mnyika atakuwa Prof. Tayari

si 1000 tu,,, wengine sijui 50,000 si wako upinzani? sasa tatizo nini?

baab kubwa ! great eksiplenesheni ! excelente !
 
Unajua mkuu, kinachobishaniwa hapa ni kwamba, ni hivi majuzi tu hapa wanafunzi hawa hawa walikuwa wanaandamana kupinga serikali ya kishikaji na chama chake, ambavyo vimewasahau kwa kutowapa mikopo ambayo raisi aliahidi,leo ndio hao hao tena wanapokea kadi za chama ambacho walikiponda pamoja na serikali yake.Mgongano wa hoja na mawazo ndio unakuja hapa haswa. Kwamba, iweje hawahawa ndio waliponda chama majuzi na leo wanapokea kadi kwa chama hicho hicho? Nini kimewabadilisha mawazo ghafla?
Ugumu wa kufikiri unakuja hapa haswa mkuu.
Tuendelee kulumbana.

una uhakika wanafunzi wote waliprotest siku hiyo au ni baadhi ya wanafunzi ? unajuaje kama wanafunzi waliojiunga na ccm waliprotest ?
 
una uhakika wanafunzi wote waliprotest siku hiyo au ni baadhi ya wanafunzi ? unajuaje kama wanafunzi waliojiunga na ccm waliprotest ?

Hata kama sio wote walishiriki maandamano, lakini ni wote walisimamishwa masomo kwa kutokuingia darasani. Kwa hiyo basi, athari za wachache zinawakumba na wasiokuwemo.
 
Nadhani ushauri kwenye Network yangu unafanya kazi.
Nimewaagiza vijana wasicheze mbali na system naona agizo langu linatekelezwa kwa vitendo.
Strategy za kupambana ni nyingi sana ndiyo maana ndani ya CIA kuna KGB na ndani ya KGB kuna CIA.
 
heheee, wewe kweli upo yu-es-ei !
 
Hata kama sio wote walishiriki maandamano, lakini ni wote walisimamishwa masomo kwa kutokuingia darasani. Kwa hiyo basi, athari za wachache zinawakumba na wasiokuwemo.

lakini hapa sikumaanisha chochote juu ya WALIOSIMAMISHWA masomo, nilikuwa nikiongelea WALE WALIOJIUNGA NA CHAMA CHA MAPINDUZI !!
 
lakini hapa sikumaanisha chochote juu ya WALIOSIMAMISHWA masomo, nilikuwa nikiongelea WALE WALIOJIUNGA NA CHAMA CHA MAPINDUZI !!

KM,
Naona unajibu mmoja baada ya mwingine.....hakuna hoja au swali bila kuwa na jibu lake 'sahihi'. Wewe kweli kada, nimekubali!!!.
 
if they keep beating you, why not join them?

Mzee MMJ,

I like this kuhusiana na hii ishu, maana inaweza kuwa na maana nyingi sana, ikiwa ni pamoja na kujiunga na wenye hoja kama huna hoja, badala ya kuleta viroja!

Nimesema mara niyngi kuhusu hawa wanafunzi, si majuzi tu walikuwa wakisifiwa kuhusiana na Zitto, "kuzuiliwa" huko mashuleni kwao au?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom