Wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma vs Binafsi

generalization yako sio sahihi mkubwa na ningependa uangalie vyuo binafsi kwa umakini kabla ya kutoa maoni humu JF. Mfano ukiangalia vyuo vingi vya umma ndio vinaongoza kwa wanachuo wake kufanya mafunzo ya vitendo mfano pale ardhi kila mwisho wa muhula wanachuo wote wanafanya field na ni kwa mda wa siku 80,ukienda udsm pia courses nyingi ukiondoa za CASS na UDBS(kwa mwaka wa kwanza hawana mafunzo ya vitendo) ila collages zingine wanafanya haya mafunzo.

Ukija kwenye vyuo binafsi huko ni mwendo wa projects yani wanachuo mpaka wanahitimu hawajawahi fanya haya mafunzo sasa kwa hali ya kawaida tu unatarajia ufanisi kutoka kwa muhitimu huyo? Maana wengi wao mpaka wakae sawa inabidi ofisi itumie nguvu ya ziada ili akae sawa katika hiyo taaluma ambayo kwa ofisi zinazo-recruit vizuri hawezi kupata nafasi muhitimu wa hivyo vyuo binafsi.
Upo sahihi mkuu, labda inategemea pia na aina ya kozi ambayo mtoa hoja anajaribu kuziungumzia..kwa ujumla ukienda vyuo vingi vya umma vinajitosheleza kwa kiasi kikubwa na ufuatiliaji wa mitaala.
 
Mod jamani mbona husikii kilio cha watuuuuu!!! tuliashasema thread zinazohusu ubora wa vyuo ziondolewe.

Kwani nkazi ya jukwaaa lka Elimu ni nini???? wewe utakuwa ni mtanzania wa aina gani usiyetaka changamoto???
 
vyuo vya kibongo vyote uozo mtupu na ubabaishaji......tunasoma kwa nadharia ila practical hamna kitu kama unabisha mtafute mtu anayesoma it au computer science mpe kazi ya kitendo ......yaani utacheka anachokifanya

Umenifurahisha saana: nimewahi kufanya kazi last year na m2 mwenye degree ya comp science, 1 day akawa ananiuliza 'hiv bootable CD ndio nini?'
 
Umenifurahisha saana: nimewahi kufanya kazi last year na m2 mwenye degree ya comp science, 1 day akawa ananiuliza 'hiv bootable CD ndio nini?'

huyo atakua degree holder wa vijichuo uchwara,ukienda mavyuo ya umma hapa TZ yote yamejaa majembe na ukija kwenye ishu za taaluma ndio toka watoto wako fiti,inaonesha hiyo ofisi ni kijibanda tu ka mtaani maana kama ni ofisi ya maana huwezi kuajiri KILAZA kama huyo.
 
vyuo vip bora kati ya vya umma na binafsi kwa sasa kawaulizeni ma afisa uwajili watawambia hivyo vya umma vinatoa nini na vya binafsi vinatoa nini tuache mawazo ya kiujumla na jambo la mwaka 2000 usilizungumzie leo mwaka 2011 ulimwengu umebadilika sasa tunaangalia uwezo wa mtu si chuo gani watoto wa vyuo vya umma na binafsi wote majibu ya assigment zao wanadesa google sasa sijui mnaongea nini
 
Umenifurahisha saana: nimewahi kufanya kazi last year na m2 mwenye degree ya comp science, 1 day akawa ananiuliza 'hiv bootable CD ndio nini?'

sasa mpaka chuo kama tumain nao eti wanatoa degree ya IT,unategemea nin hapo?
 
Back
Top Bottom