Wanafunzi wa vyuo vikuu vya iringa waunda shirikisho la wanachadema-iringa

PAMBANA

Member
Oct 21, 2010
73
21
Kweli chama cha CHADEMA kinazidi kujiwekea hazina ya wasomi hapa nchini na kinakubalika kwa asilimia kubwa sana kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.

Hivi karibuni wanafunzi wanachama na wakereketwa wa vyuo vikuu vya hapa mjini Iringa kwa maana ya Chuo cha Tumaini,Mkwawa na RUCO waliunda shirikisho la wanafunzi wanachama na wakereketwa wa CHADEMA.

Shirikisho hili linaitwa IRINGA UNIVERSITIES AND COLLEGES CHADEMA NETWORK lipo chini ya uongozi wa CDM wilaya ya Iringa Mjini. Wana mikakati mingi kukuza na kukijenga chama hapa Iringa kwa kueneza sera na kuwaelimisha vijana wenzao.

Pia wanataka kuhakikisha wanashirikiana na mbunge Mh.P.Msigwa kukieneza chama na kufungua matawi vijijini.Hivi karibuni kutakuwa wataandaa kongamano la katiba ambalo litaambatana na kulizindua rasmi shirikisho hili ambapo watawaalika viongozi wa chama wa kitaifa kwa ajili ya kongamano hilo.

Tafadhali naomba kuwafahamisha wana CDM walioko humu ambao mlikuwa hana taarifa hizi.

CHADEMA INAJIVUNIA NGUVU YA UMMA :rain:
 
Ni habari njema kwani wasomi wanawajibika kuwa chachu ya mageuzi, demokrasia na maendeleo katika jamii
 
Safi sana na safari njema ya demokrasia ya kweli Tanzania na pia tuna Imani kubwa sana ya CHADEMa Tanzania nakuona jinsi gani tunaweza kufanya siasa za ushindani Imara Tanzania
 
Exllent! Inatia moyo na hamasa zaid, Tumain university Arusha nas tunaenda kuanzisha!
GUD wana CDM wasomi, mnafaa kuwa chachu ya mabadiliko, we ni the real changes!
 
vizuri sana, siasa yatakiwa mjifunze mkiwa vyuoni ili mkitoka tu, mnatekeleza coz mtakuwa mmekomaa. Vijana tuungane pia tuwe makin na viongozi mamluki!
 
makaburu wa Tanzania ni wale wanaojiita wazawa, wenye uchungu na nchi hii, wanaopendekeza jembe la shilingi 2500 kwa mkulima ilihali wakimiliki magari ya anasa! Wakati wa mabadiliko ndio huu!
 
Hongereni sana wanafunzi wa Vyuo Vikuu hasa wa huko Mkoani Iringa kwa kuwa juhudi zenu katika muitiko wa kuleta mabadiliko ya kweli nchini yametambulika!!!

Hakika ni wakati mwafaka wanafunzi wote wa vyuo vikuu nchini kunyanyuka kusimama mstari wa mbele kuhesabiwa kuwa ni sehemu muhimu sana katika kundi linalopanuka kila kukicha TUKIJIANDAA VILIVYO KULINYIMA PUMSI GENGE LA FISADI NCHINI hivi karibuni.
 
I won't be surprised to hear Kikwete or one of his surrogates condemning those student's involvement in politics as they are very quick to forget that for decades CCM has been having party branches in colleges and it was only last year Kikwete boasted of UDOM students sponsoring his campaigns to Presidency.

With such moves from the elite, victory from CCM hegemony is assured. Bravo our youths, the genuine pride of our nation.
 
Exllent! Inatia moyo na hamasa zaid, Tumain university Arusha nas tunaenda kuanzisha!
GUD wana CDM wasomi, mnafaa kuwa chachu ya mabadiliko, we ni the real changes!
Nitafuatilia kwa hamu zaidi hizi ahadi za wanavyuo wachukia UFISADI mlioko huko makao makuu ya mabadiliko nchini - jiji la Arusha kwa machaliii na aina ya mikakati bunifu mtakazojitokeza nazo kama wale wenzenu wa Iringa kuliangamiza kabisa hili genge sugu mafisadi nchini kwa kuwaamsha Watanzania kila pembe ya chi kusema 'MAFISADI ONDOKENI NYOTE LEO'!!!

Japo ahadi ni deni, muziki wa Mkoa wa Arusha siku zote usipime, ni muziki munene ya uhakika hakuna mfano wake!!!
 
CCM KIANZA CHOKOCHOKO JUU YA CHADEMA NA VYOMBO VYA DOLA KUTEKELEZA
AZMA YENU NA BASI SISI WANANCHI TUTAMALIZIA KWA
UFASAHA ZAIDI PICHA NZIMA HIVI KARIBUNI


Mheshimiwa Kikwete kidogo kachanganya mada hapa: kati ya Chama (CCM) kilichoshiriki, kupanga na kutekeleza njama za kuwapora wananchi HAKI YA KUCHAGUA viongozi wanaowapenda , upande mmoja, na kwa upande kuna chama (CHADEMA) kinachotekeleza wajibu wake wa kikatiba kushiriki kwenye kupiga mayowe kwa njia ya maandamano ya amani kote nchini kwa kudai kwa uchungu mkali kwamba Watanzania TUMEPORWA HAKI YETU YA MSINGI kikatiba; mpaka hapo ni chama gani kinastahili kufutwa usajili na kuchukuliwa hatua zote na vyombo vya dola???

Mbele ya 'Nguvu ya Umma' hakuna cha John Tendwa na ukada wake kwa CCM, Mrema na fadhila yake kwa uenyekiti wa kamati ya bunge, wala hakuna cha Maswahiba kama Said Mwema wala nani. Tunawasubirini kwa hamu muanze mchezo mzima ili mtakapoandika moja sisi tutaandika kumi na kuendelea.

Chonde msikose kutekeleza amri na busara za Kanali Kikwete, Kapteni Chiligati na Luteni Kanali Makamba maana hiyo ni HARUSI AMBAYO tumekua tukiisubiri kwa muda mrefu sana mpaka hivi sasa sisi Vijana Nguvu kamili ya Umma.
 
Kweli chama cha CHADEMA kinazidi kujiwekea hazina ya wasomi hapa nchini na kinakubalika kwa asilimia kubwa sana kwa wanafunzi wa vyuo vikuu. Hivi karibuni wanafunzi wanachama na wakereketwa wa vyuo vikuu vya hapa mjini Iringa kwa maana ya Chuo cha Tumaini,Mkwawa na RUCO waliunda shirikisho la wanafunzi wanachama na wakereketwa wa CHADEMA.Shirikisho hili linaitwa IRINGA UNIVERSITIES AND COLLEGES CHADEMA NETWORK lipo chini ya uongozi wa CDM wilaya ya Iringa Mjini.Wana mikakati mingi kukuza na kukijenga chama hapa Iringa kwa kueneza sera na kuwaelimisha vijana wenzao.Pia wanataka kuhakikisha wanashirikiana na mbunge Mh.P.Msigwa kukieneza chama na kufungua matawi vijijini.Hivi karibuni kutakuwa wataandaa kongamano la katiba ambalo litaambatana na kulizindua rasmi shirikisho hili ambapo watawaalika viongozi wa chama wa kitaifa kwa ajili ya kongamano hilo.

Tafadhali naomba kuwafahamisha wana CDM walioko humu ambao mlikuwa hana taarifa hizi.

CHADEMA INAJIVUNIA NGUVU YA UMMA :rain:

who cares?
 
Back
Top Bottom