Wanafunzi wa Vyuo/Sekondari waruhusiwe kufanya kazi kuchangia elimu yao?

mwanakijiji uko juu sana na kuunga mkono kabisa maana mimi hii nimeifanya pale nilipokuwa SUA mpaka leo hii ninavyo sema niliweza kupata kiwanja na kuanza kujenga nyumba kwa biashara ya kuchoma tofali lakini tatizo wanafunzi wengi hawataki kuhangaika ila wanategemea wazazi wao na mbaya sana nipale wanawake wanapofanya uchangudoa mapaka hata huku ughaibuni wanatuzalilisha sana yani wanakosa akili za nini wafanye ilikujipatia kipata kwa ajili ya starehe. tuzidi kuwasaidia hawa dada zetu maana hawajui kama HIV ipo hata ughaibuni wanajipa matumaini hakuna HIV huku bali Afrika. sijui kama kuna ukweli wowote.
 
Mkuu mwanakijiji hoja yako ni nzuri ila ni impractical kwa Tanzania. Zamani miaka ya 80 kurudi nyuma wanafunzi wengi wa chuo kikuu, nikiongelea chuo kikuu kwa wakati huo unanielewa (yaani UDSM) walikuwa wana muda wa kufanya kazi za ziada na baadhi yao walikuwa wanafanya kazi. Kilichokuja kuharibu ni baada ya migomo na watawala kutukanwa. Ikaonekana kuwa wanafunzi wa chuo kikuu wana muda mwingi wa ziada ndiyo unaowafanya kufanya mambo ya kipuuzi kama migomo, n.k. Mkakati ukawa dawa ni kuwa keep busy na shule, wataalam wa mitaala wakaanzisha kitu kinachomuweza busy mwanafunzi kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa mbili usiku. Anachofikiria ni chakula na darasani tu kama yupo serious na elimu.

wakaanzisha mfumo wa semester kutoka term system, wakaongeza idadi ya kozi, unakuta mtu ana kozi mpaka nane kwa semester na zote hizo anatakiwa kuhudhuria, lecture, seminar/tutorials, katika course assessment anakuwa na homework plus tests. Hii inamfanya mwanafunzi 24hrs a day kufikiria jinsi ya kupangua issue moja ya elimu baada ya ingine, je saa ngapi atapata muda wa kufanya part time job?.

Kingine ni suala la uchumi, kutokana na hali kuwa ngumu waajiri hawaajiri tena, maana kama kuna mtu kamaliza masomo miaka miwili iliyopita na bado hajapata kazi unatarajia aliyeko shuleni atafanikiwa?. Nakumbuka mimi enzi zetu unakuta mtu bado hajamaliza hata mitihani tayari ana offer tatu au nne za kazi mpaka anachanganyikiwa lakini si sikuhizi, tena kibaya zaidi waajiri wameanzisha mchezo wa kuangalia GPA (Grand Points Average) ili mtu awe shortlisted for an interviews, the higher the GPA the higher the chance of being called for the interviews, sasa mtu akiangalia kufocus katika part time kutampunguzia uwezo wa kutengeneza GPA kubwa.

Kwa ujumla tu katika mazingira ya mfumo wa elimu ya Tanzania wa leo hii, hii mada yako wengi wataiona ni kituko japo there is very important suggestions in it.

Nadhani wewe unaongelea kazi za ofisini au niseme -skilled jobs. Kama nimemwelewa Mwanakijiji vizuri yeye anasema kazi ni kazi ili mradi ni halali; kukata majani, kusafisha vyoo, bartender etc. Nina ndugu wa karibu wanaosoma chuo kikuu na mwaka jana nilitaka kumtwanga mtu ngumi kwa sababu alikuwa nyumbani muda wote wa likizo kubwa ya mwaka. Miezi 3 (maana vyuo vilichelewa kufunguliwa kutokana na uchaguzi).

Binafsi nilifanya kazi ya kuosha vyombo hotelini huku nasoma (saa 12 jioni mpaka saa 6 usiku asubuhi darasani). Unachoka vilivyo lakini unakubali no pain no gain. Siku hizi vijana wanazuzura kwa miezi mitatu, kila kukicha wanaomba nauli ya daladala kwenda kutembelea rafiki mara mbagalla mara mbezi. Ninavyoondika hapa nimeshampa 'warning' mtu kwamba wakifunga chuo nataka aje na majibu ya atafanya nini kujipatia pocket money! sitaki mtu aniogengee mlango anaomba nauli. Nadhani wazazi na walezi nao inabidi waangalie hili maana tunalea taifa la walalamishi na washika vibakuli.

Hivi ni wapi ulimuona mwanafunzi wa chuo anafanya kazi kwenye 'chip kuku'? wote wanataka kuvaa suti na kuingia ofisini hata kama hajapata hiyo degree! Ukija kwa wadogo zao wa sekondari wale wanalala vilivyo wakiamka wanaomba hela haoooo kwenye internet cafe!
 
Mkuu mwanakijiji hoja yako ni nzuri ila ni impractical kwa Tanzania. Zamani miaka ya 80 kurudi nyuma wanafunzi wengi wa chuo kikuu, nikiongelea chuo kikuu kwa wakati huo unanielewa (yaani UDSM) walikuwa wana muda wa kufanya kazi za ziada na baadhi yao walikuwa wanafanya kazi. Kilichokuja kuharibu ni baada ya migomo na watawala kutukanwa. Ikaonekana kuwa wanafunzi wa chuo kikuu wana muda mwingi wa ziada ndiyo unaowafanya kufanya mambo ya kipuuzi kama migomo, n.k. Mkakati ukawa dawa ni kuwa keep busy na shule, wataalam wa mitaala wakaanzisha kitu kinachomuweza busy mwanafunzi kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa mbili usiku. Anachofikiria ni chakula na darasani tu kama yupo serious na elimu.

wakaanzisha mfumo wa semester kutoka term system, wakaongeza idadi ya kozi, unakuta mtu ana kozi mpaka nane kwa semester na zote hizo anatakiwa kuhudhuria, lecture, seminar/tutorials, katika course assessment anakuwa na homework plus tests. Hii inamfanya mwanafunzi 24hrs a day kufikiria jinsi ya kupangua issue moja ya elimu baada ya ingine, je saa ngapi atapata muda wa kufanya part time job?.

Kingine ni suala la uchumi, kutokana na hali kuwa ngumu waajiri hawaajiri tena, maana kama kuna mtu kamaliza masomo miaka miwili iliyopita na bado hajapata kazi unatarajia aliyeko shuleni atafanikiwa?. Nakumbuka mimi enzi zetu unakuta mtu bado hajamaliza hata mitihani tayari ana offer tatu au nne za kazi mpaka anachanganyikiwa lakini si sikuhizi, tena kibaya zaidi waajiri wameanzisha mchezo wa kuangalia GPA (Grand Points Average) ili mtu awe shortlisted for an interviews, the higher the GPA the higher the chance of being called for the interviews, sasa mtu akiangalia kufocus katika part time kutampunguzia uwezo wa kutengeneza GPA kubwa.

Kwa ujumla tu katika mazingira ya mfumo wa elimu ya Tanzania wa leo hii, hii mada yako wengi wataiona ni kituko japo there is very important suggestions in it.

Hapana, hoja hii ni ya msingi sana.

Hasa katika zama hizi waajiri wataangaliai zaidi wanafunzi kwa kuzingatia kuwa malipo yao ni madogo(kima cha msharhara wa mwanafunzi) kama ilivyo kwa sasa wanavyokimbilia kuajiri vibarua (casual nworkers) kwenye viwanda vingi vya watu binafsi ambapo kuna vibarua mpaka wa miaka sita na vibarua wana-constitute 70% or more ya entire workforce.

Nimependa hilo wazo.
 
Mwanakijiji, hoja yako imekuja wakati mzuri tena mapema ili watu waijadili kwa kina kabla hatujabadili chama tawala! Hii itawasaidia wanafunzi sana hata kusoma pia. Mwanafunzi akipata part time job, itasaidia kuongeza hata pato la taifa kwa kuongeza uzalishaji. Chukulia mimi nifungue kiwanda maeneo ya ubungo karibu na UDSM pale say cha kutengeneza juice. Nikiajili wanafunzi wa part time ( naweza kuweka limit fulani hivi kama kwa kila 200 bottles of processed juice namlipa mwanafunzi kiasi fulani cha pesa) then its good for me, my company and for the student.

Nipo ughaibuni, wanafunzi wengi hapa wanajisomesha! wapo wanaopata scholarships lakini si wote kwa hiyo wengi wanapiga part-time jobs na wengi wanategemewa na makampuni katika kuweka mambo sawa. So, its makes the students not rely too much on their family, government and other crazy business.
 
Hapana, hoja hii ni ya msingi sana.

Hasa katika zama hizi waajiri wataangalia zaidi wanafunzi kwa kuzingatia kuwa malipo yao ni madogo(kima cha msharhara wa mwanafunzi) kama ilivyo kwa sasa wanavyokimbilia kuajiri vibarua (casual nworkers) kwenye viwanda vingi vya watu binafsi ambapo kuna vibarua mpaka wa miaka sita na vibarua wana-constitute 70% or more ya entire workforce.

Nimependa hilo wazo.

Hilo liende sambamba na ku-review mtaala wa vyuo vikuu ili kutoa muda wa hawa watanzania kuweza kushiriki katika ujenzi wa taifa kwa kutoa kuliko wakati huu ambapo wanapokea tu.
 
Kuna kundi kubwa la watu ambao wanasubiri serikali iwapatie fedha za masomo n.k na wazazi wao wakati wana uwezo wa kufanya kazi. Kwa muda mrefu mfumo ulioundwa na serikali ya CCM unazuia na kufanya iwe ngumu sana kwa wanafunzi kufanya kazi. Matokeo yake, walinzi kwenye vyuo wanaajiriwa nje, wasafisha madarasa na vyoo ni watu wa nje, wakata majani ni watu wa nje wakati kuna nguvu kazi ambayo ipo tu.

Tumetengeneza mfumo wa kundi tegemezi ambalo linachukua tu kutoka kwenye jamii lakini halirudishi. Wengi wa hawa wanapata nafasi ya kufanya kazi kidogo kama sehemu ya kutimizwa matakwa ya elimu yao (research, internships n.k). Je, umefika wakati wa kutengeneza mfumo wa wanafunzi kuchangia elimu kwa kuwapatia nafasi za kazi humo humo mashuleni na kuweka kiwango cha chini cha mishahara ya wanafunzi (iwe tofauti na kima cha chini cha mtu wa kawaida).

Kwa mfano, badala ya kuwapatia posho bila kufanyia kazi kwanini posho za wanafunzi nchini zisiingizwe kama sehemu ya mapato yao wanayofanyia kazi?

je wanafunzi watakuwa tayari kusafisha vyoo, kufagia, kukata majani, kulisha wanyama, kufanya kazi za uwaiter/bartender n.k ili wajipatie kipato cha matumizi?

Je, tunaweza kuweka utaratibu hata wanafunzi wa sekondari nao waruhusiwe kufanya kazi na kujipatia kipato badala ya kutegemea fedha za posho toka kwa familia, wadau na wapambe?

mwanakjj huu mfumo unawezekana kabisa na unahitaji umakini mkubwa sana , na chini ya ccm hautawezekana kwa sababu unahitaji watu makini sana, kwa ccm kila kitu kwao ni dili la kula na kuiba pesa
 
Unanikumbusha enzi zile za "Education for self reliance" ambapo shuleni tulizalisha mboga,kuku wa nyama na mayai, mihogo n.k. mwishoni tuliweza kufaidi matunda yake moja kwa moja licha ya kujifunza kilimo na ufugaji pia umhimu wa kazi. Siku hizi ukitaja hilo unatafuta ugomvi, kazi kwa vijana wetu sio jambo la kujivunia. Wanataka mafanikio kwa kamali (jirushe, vuta mkwanja, tajirika, hamisi manoti,jishindie mamilioni na simu ya blackberry.......). Vijana wanataka wakae kujisomea tu bila bughudha....... chakushangaza kusoma kwenyewe nitaabu kwao wanataka "madesa" na kwahiyo hata maarifa(knowledge) hawana. Juhudi kubwa inawekwa kupata vyeti nasio taaluma. Elimu yetu imepoteza malengo kama "Education for self reliance" ilivyo potea.
 
Hoja ni nzuri sana ila sisi tumechangia zaidi kwenye ajira za "kisomi". Ukimwambia mwanafunzi wa chuo kikuu TZ kufanya kazi ya kufyeka au kufagia choo (Japo waliopo nje ya nchi wanaweza). Utaonekana kama unamtukana matusi ya nguoni. Tuna tatizo kubwa la kuchagua kazi, sio kwamba ajira hamna! Nina rafiki yangu aliishi kwa mjomba wake Dar kwa zaidi ya mwaka mmoja, kisa alikuwa haridhiki na kazi anazopata, ila kwa sababu ya kuwa alikuwa anakula na kulala bure haikuwa vigumu kusubiri.
 
Mkuu hongera kwa kuzama katika mawazo na kuibuka na hoja nzito. naona hata michango yote ni mizito sijaona aliyechafua hewa mpaka sasa.

1. Kimsingi ni wazo zuri sana la kimapinduzi. cha kwanza kama walivyosema wengine, ni kubadili falsafa ya mitaala yetu. hii habari ya kumrundikia mtu masomo kibao haitusaidii chochote. watu waweke mkazo katika masomo yanayohusiana, kuwe na specialization mapema zaidi. hii ina faida nyingi. pamoja na kutoa nafasi kwa mwanafunzi kufanya kazi za ziada, itampa pia nafasi ya kusoma na kuelewa badala ya kusoma ili kufaulu mtihani.

2. lakini la msingi zaidi, tatizo kubwa lililoko katika taasisi zetu ni kwamba watu wanapenda kushughulika na makampuni ili wapate commission. sasa kama wanafunzi watakuwa wanapata offer hizi, maana hapo unapunguza "ulaji" wa wakuu fulani, kwa hiyo wanaweza kuiwekea breki hii.

3. Sidhani kwamba kwa kuwa tu wanafunzi wetu wengi wanashabikia maisha ya kifahari na anasa, na kuwa aliyefanikiwa ni yule asiyefanya "kazi za kifala-****", sidhani kama hilo litakuwa tatizo kwa muda mrefu. ukishaweka tu utaratibu huo ukafanya kazi, utaona mabadiliko katika fikra, kutoka kwenye kuchagua kazi za kifala, kwenda kwenye msimamo wa "inaniweka chuoni". mabadiliko haya katika mtazamo huwa yanachukua muda kidogo lakini ndivyo itakavyokuwa. heshima itakuja tu mradi watu wanalipwa na kufanikisha mambo yao.

4. hii itatusaidia pia kurejesha heshima ya kazi. kuna kipindi mwanafunzi alifanya kazi kama adhabu, na kuona kabisa vitu kama kuchimba choo, shimo la taka, kulima na kufyeka kama ni adhabu. lakini sasa mtu atafanya kazi za mikono zinazofanana na hizo na kujipatia kipato. itakuwa namna fulani ya JKT hivi. imetulia sana.

5. Lakini ipo willingness ya kufanikisha hilo? tunahitaji ushirikiano wa sekta kadhaa hapa. kwa watu wenye lengo la kujenga nchi na taifa, ni wazo la msingi na la kufanyiwa kazi. lakini je, viongozi wetu wanatumia muda wao mwingi kufikiria namna ya kumsaidia mwananchi? kama will haipo, tutafute namna ya kuchagiza hili
 
Hii inawezekana kabisa lakini kazi zenyewe ziko wapi?
Halafu hawa vjana wetu 'MASHAROBARO' kazi nyingine hawapendi kuzifanya. Laiti kama wangepitia JKT labda hili wazo lingewezekana.

"Fikiri nje ya sanduku" ndugu! Kazi mbona ziko nyingi kuanzia majumbani, mabarabarani, sehemu za biashara nk au lazima upate kazi ofisini?

Hizo hizo kazini nyingine unazozidhania hazipendwi na masharobaro huko Ughaibuni ndizo hufanywa na watu wenye hata PHD! MRADI KIPATO KINAPATIKANA.
 
Hoja ni nzuri sana ila sisi tumechangia zaidi kwenye ajira za "kisomi". Ukimwambia mwanafunzi wa chuo kikuu TZ kufanya kazi ya kufyeka au kufagia choo (Japo waliopo nje ya nchi wanaweza). Utaonekana kama unamtukana matusi ya nguoni. Tuna tatizo kubwa la kuchagua kazi, sio kwamba ajira hamna! Nina rafiki yangu aliishi kwa mjomba wake Dar kwa zaidi ya mwaka mmoja, kisa alikuwa haridhiki na kazi anazopata, ila kwa sababu ya kuwa alikuwa anakula na kulala bure haikuwa vigumu kusubiri.

Kwenye bold - nadhani kuna kitu pia kinajitokeza hapa nacho ni ustaarabu! Tanzania sehemu nyingi matumizi ya facilities kama vyoo nk ni mtihani mkubwa sana.Ustaarabu hakuna utashangaa hata majumbani mwa watu huu ustaarabu ni haba! Sishangai kama wanafunzi na watu wengine wakikataa au kunyanyapaa kufagia vyoo! Sijui kama kuna mtu atanipinga nikisema kuwa kazi nazo ziendane na ustaarabu ili zivutie watu kuzifanya.Sijui tufanyeje ili kujenga ustaarabu utakaochochea kupenda kazi za iana yoyote. Ughaibuni watu wanajua au kujifunza ustaarabu wa kutumia vyoo na hata huduma nyingine. Tanzania na nchi nyingine za ulimwengu wa tatu bado tuko nyuma sana na utakapojaribu kuibua hili kama tatizo basi unaweza kuangaliwa vinaya kama mtu mwenye majivuno! TUNA KAZI KUBWA SANA KAMA TUNATAKA KUBADILI MIFUMO NA TARATIBU ZA MAISHA!
 
Mzee mwanakijiji sitaki kuunga mkono hoja yako japo kwa mbali inaonekana ina maana fulani, Kwanza kabla ya kuanza kwa mfumo huo lazima ujue kwa nini mfumo wa zamani ulikufa kwa mfano nikiwa primary school na baadae secondary school tulikuwa tuna mashamba ya shule ambayo tulikuwa tunalima na kisha mazao yapatikanayo yalikuwa yanasaidia shule kwa namna moja au nyingine, sijui utaratibu huo ulikufa vipi mwanzoni mwa miaka ya 2000, na tulikuwa hatupewi hata 100 ila amri ndio ilikuwa inatekelezwa.

kwenye suala la usafi wa maeneo ya shule haya bado yanafanyika hususani kwa shule za goverment sina uhakika na shule binafsi, ila kwenye vyuo mambo hayo hayapo labda vyuo vya ualimu especially diploma sina uhakika DUCE na MKWAWA.

Kwenye ulinzi hilo sitokubaliana nawe kabisa kwani ulinzi unambinu zake sasa siamini kama wanafunzi hao watakuwa na mbinu za kukabiliana na wezi pindi linapotokea suala la uvamizi, suala sio kuwaajiri ila kama watakuwa wanatoa admission kwa watu waliopitiaa mgambo then ni sahihi wakawaajili kama walinzi, rejea chanzo cha mgomo wa Secondary ya Mazengo kati ya 2002 au 2003, chanzo kilikuwa ni kuchunga ng'ombe wa shule na suala la ulinzi
 
Back
Top Bottom