SolarPower
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 223
- 27
Kutokana na uwezo wa kifedha walionao vijana wetu wa Elimu ya Juu, nawashauri wakusanye nguvu zao pamoja na kuanzisha Benki yao. Ushauri ni kuwa kila Mwanafunzi wa Elimu ya Juu awekeze angalau shilingi 500 kila siku kwa kununua hisa za Benki watakayoianzisha. Kwa utaratibu huu kwa mwaka mmoja tu, watakuwa na uwezo wa kukusanya mtaji usiopungua shilingi bilioni 27. Baada ya miaka 10 naamini watakuwa na tawi la hiyo benki yao katika kila mkoa kama sio katika kila wilaya hapa chini. Kupitia Benki hii vijana wetu wengi wapata fursa nzuri ya kuweza kujiajiri na kutimiza ndoto zao katika katika maisha yao.