Wanafunzi vyuo vikuu waandamane kupinga malipo ya Wabunge?

Wabongo bado sana,i said it before!inasikitisha sana kwasababu kuna watakaokata tamaa na hii nchi, kuna ambao wameshafanya hivyo,wengine wanakula na vipofu...Subiri uone kama kuna watakaokataa hayo malipo yenye kukufuru ama kama wanafunzi/wananchi wataandamana.

Chief Observer wa EU EOM David Martin wakati anakabidhi report ya uchaguzi alisema “……I would like to be clear that in doing so we in no way call into question the validity of the election result. I said the last time I was in the country that the ultimate test of an election is did the people get the government they voted for? In Tanzania, they did…”

Haina maana kuwa Tanzania wamepata the government they needed or they deserved. Kwa hiyo mnaopiga kelele na ubovu au upungufu wa priorities za nchi, mkumbuke kuwa watu wamepata serikali walioichagua.

Wabunge na Dowans ni lazima walipwe (Bil 94 Dowans, Bil 34 magari ya Wabunge). Wanafunzi, wagonjwa, Wazee wa Jumuia, nyongeza za mishahara ya walimu, ukosefu wa umeme, barabara mbovu, n.k. hivyo vyote visubiri kwani serikali haina hela.
 
haya fanyeni hima wabunge wa upinzani kupeleka hoja binafsi kupinga malipo ya mil 90 kwa ajili ya matumbo yenu ,kama kweli mnalitakia mema taifa hili lenye asilimia 80 ya watu wanaoishi chini ya dola moja, ukosefu mkubwa wa ajira na huduma mbaya za kijamii kama afya, elimu, maji,umeme na miundo mbinu mibovu.
 
Baba sasa anakunywa uji wa mtoto.
Siamini;
au ni mbinu ya siasa ili jk akemee hilo angalau asave face. lakini hilo nalo siamini.
Ombi;
Wabunge wote wazalendo bila kujali chama, wapokee pesa hizo kisha ipelekwe kwenye kuhudumia elimu.
NB Iundwe kamati ya wabunge,wanaharakati, viongozi wa dini ili wasimamie pesa hiyo itakayo rudishwa na wabunge itumike kwa malengo ya kuboresha elimu tu. Ikibidi ianzishwe bank au Acc kwa madhumuni hayo.
pesa yetu irudi.
 
Badala ya kuandamana kudai ng'ombe atoe maziwa zaidi kwanini wasiandamane kutaka ng'ombe alishwe zaidi ili atoe maziwa zaidi? Au kwanini wasiandamane kupinga maziwa ya ng'ombe kupewa watu wachache zaidi huku wengi wakijitahidi kumlisha ng'ombe huyo?

Wanafunzi wa Vyuo vikuu na wananchi wengine wana haki ya kupinga malipo ya kifisadi ambayo yanafanyika kwa jina la "ubunge"; kwanza siyo tu wakatwe posho na mishahara ya wabunge wote isitishwe kuongezeka kwa miaka miwili ijayo. n.k n.k n.k Au wanafikiri hizo posho na malipo ya wabunge zinatoka wapi kama siyo katika kodi za watoka jasho wa Tanzania?

Haya ndiyo matatizo. Tunadhani kundi fulani ndilo lenye jukumu la kuondoa matatizo yetu.Kwanza hatulalamikii kile au hiki, halafu tuishie kwenye kuandamana tu.Ni lazima tuelewe tatizo letu.Tatizo sio CCM au Kikwete,tatizo ni la kimfumo.Ili tuweze kuung'oa mfumo huu uliopo, ni lazima tushirikiane wote.Hili sio jukumu la wanachuo tu au kundi fulani la watu.
 
Unafikiri haya maandamano tuyafanye lini? Mimi nipo tayari.
Badala ya kuandamana kudai ng'ombe atoe maziwa zaidi kwanini wasiandamane kutaka ng'ombe alishwe zaidi ili atoe maziwa zaidi? Au kwanini wasiandamane kupinga maziwa ya ng'ombe kupewa watu wachache zaidi huku wengi wakijitahidi kumlisha ng'ombe huyo?

Wanafunzi wa Vyuo vikuu na wananchi wengine wana haki ya kupinga malipo ya kifisadi ambayo yanafanyika kwa jina la "ubunge"; kwanza siyo tu wakatwe posho na mishahara ya wabunge wote isitishwe kuongezeka kwa miaka miwili ijayo. n.k n.k n.k Au wanafikiri hizo posho na malipo ya wabunge zinatoka wapi kama siyo katika kodi za watoka jasho wa Tanzania?
 
Mods naomba msinifungie maana nitakachoandika hapa kitawaudhi. Tafadhali niwie radhi. Ni hivi hawa wabunge wa vyama vyote tuliwatuma waende wakalilie haki yetu au tuliwatuma waende kujirusha? Hivi kweli hata haya hamna nina maana ya wabunge wote iwe ni chadema ccm tlp na vingine mimi sifahamu majina ya vyama vingine.... hospitali hazina dawa shule hazina madawati halafu ninyi mnajilimbikizia mali mimi naona dawa sasa ni kuwasha moto kieleweke huu ni upumbavu uliozidi mipaka. Ole wenu wabunge ole wenu mkiwageuzia macho na mgongo wale waliowapigia kura. Haya Mbowe, Regia, Mnyika, Zitto tuelezeni mnachukua hayo magari au kuna tamko mtatoa??????mtujibu haraka maana sisi ndio tuliowachagua

wangunge 45 wa chadema(sina hakika) x Tshs. 25 000 000 = Tshs. 1 125 000 000

wabunge wetu onesheni mfano. changisheneni kila mbunge m25. tafuteni mahala penye uhitaji mtoe mchango wenu. ama mubuni mradi endelevu wenye manufaa ya moja kwa moja kwa jamii.
 
Unafikiri haya maandamano tuyafanye lini? Mimi nipo tayari.
Du hapo ndio maneno sasa hata mm nitakuwepo sio hao majoga wanadai kuwapa mashangingi ni sababu ya kumchagua Rais asiyemtaka.
Kinachozungumzwa hapa ni
Wanafunzi wa Vyuo vikuu na wananchi wengine wana haki ya kupinga malipo ya kifisadi ambayo yanafanyika kwa jina la "ubunge"; kwanza siyo tu wakatwe posho na mishahara ya wabunge wote isitishwe kuongezeka kwa miaka miwili ijayo. n.k n.k n.k Au wanafikiri hizo posho na malipo ya wabunge zinatoka wapi kama siyo katika kodi za watoka jasho wa Tanzania?
 
Bado tuna safari ndefu kwa kweli.
Mkuu Mwanakijiji Kama kuna kitu ninafeel strongly ni matumizi ya rasilimali zetu na kodi zetu na nina uhakika kama wananchi wote wangejua mpaka huko kijijini kuhusu kodi zetu zinavyofujwa nina uhakika wangefeel the same... Na hii ni vita yetu wote wananchi wote wa Tanzania.., Sasa Mkuu ninakuomba kwa kutumia Platform yako ni vema tukawaambia wananchi wote jinsi pesa zao zinavyotumika..., kwa kila mmoja kutumia nguvu kwa uwezo wake.

Na wewe mkuu unaweza ukatumia platform yako ya kwenye gazeti kuweza kuelimisha wachache. Mkuu hii ni vita ya sisi wananchi wote na sio tabaka fulani, na hakuna mtu mmoja peke yake anayeweza kuikabili hii vita...
 
TUNATAKA MCHAKATO WA KATIBA MPYA NA TUME HURU
YA UCHAGUZI BUNGENI SASA HIVI!!!

Enyi Ndugu Waheshimiwa viongozi wetu

akina Kikwete, Dr Slaa, Prof Lipumba, Mbowe, Julius Mtatiro, Zitto Kabwe, Mbatia, Dr Mvungi, Prof Baregu, Prof Mukandala, Dr Bana, Dr Azaveli, Mama Nkya, Ndg Mgaya, Makwaia wa Kuhenga, Jenerali Ulimwengu, Reginald Mengi, Pius Msekwa, Fredrick Sumaye Fredrick Msuya, John Malecela, Mama Anna Makinda, Sheik Issa Bin Simba, Mhe Iddi Simba, Maaskofu na Wachungaji wote nchini, Denis Mwamnyange, Said Mwema, The Othma's, Tundu Lissu, Sitta, Mwakyembe, Mzee Mkapa, Mzee Salim Ahmed Salim, Mzee Sinde Warioba, Mzee Butiku, Prof Sarungi, Selasini, Ole Sendeka, Tido Mhando, Mama Maria Nyerere, Mama Karume, Selelii, Prof Bangu, Dr Matumaini, Bashe, Celina Kombani, Kafulila, Hamad Rashid, Regia, Lukuvi, Mama Maghimbi,Mama Anna Abdala, Pombe Magufuli, Mstaarabu wa Siasa Tanzania - Dr Mohammed Shein, Salmin Amour, Godbless Lema, Mzee Mwanakijiji, Maxence Melo, Candid Scope, Fareed, Mwakalebela, Mnyika, Halima Mdee, viongozi wote wa serikali za wanafunzi vyuoni ... na wengine wengi wengi wengi tu, sisi kama vijana wa nchi hii sasa hivi tunawaulizeni nyote kwa pamoja kwamba ...

... suala letu la michakato wa kujiandikia KATIBA MPYA na kuunda Tume Huru ya Uchaguzi ZINAANZA LINI BUNGENI???

Ndugu yangu sikusomi kabisa kila thread we unaibuka na hii post..hebu niweke sawa :coffee::coffee::roll::roll::roll:
 
haya fanyeni hima wabunge wa upinzani kupeleka hoja binafsi kupinga malipo ya mil 90 kwa ajili ya matumbo yenu ,kama kweli mnalitakia mema taifa hili lenye asilimia 80 ya watu wanaoishi chini ya dola moja, ukosefu mkubwa wa ajira na huduma mbaya za kijamii kama afya, elimu, maji,umeme na miundo mbinu mibovu.

am afraid, mhhhh. Unafikiri baba askofu Pengo alikosea. Watu wanapinga ufisadi si kwa sababu wao si mafisadi, bali hawamo ktk mzunguruko wa kifisadi. Lakini kama huo ufisadi unamgusa yeye anatuliza kimyaa.

Hakuna na chama mbadala tusidanganyane wajameni.
 
YES,
kwa sasa ngoja tukamilishe semester hii,hiyo inayo kuja naamini hoja yako ita fanyiwa kazi maana ni semester ya kudai haki kwa nguvu zote
 
Wabeja Ng'wanagwa
Nalebhona olena masala minge nho
Balebetela geko bamanile bale bana ba balemi!
[maoni yangu. hisia zangu. zenye harufu ya ukweli]

serikali ya tanzania inafanya makusudi kwa watoto hawa wa vyuo vikuu.

watawala wanajua kuwa wengi wa hawa wanafunzi ni watoto wa walalahoi.

watoto wa wakulima wa jembe la kupinda mgongo.

hizo kodi (P.A.Y.E) unazosema hawakatwi wazazi wao. hawana haki ya kudai kodi wanayokatwa vibopa wanaokurugenzi mashirika mbalimbali ya serikali (ambao kimsingi hawa ni watawala wenyewe au watoto wao).

au gunia mbili za mahindi anazovuna mzee Ng'wanidako kule kijijini zinakatwa P.A.Y.E? kama ni hivyo sawa. waendelee kudai. vinginevyo waingie kitaa kama Tunisia na Masri. au wanyamaze tu waendelee kupewa msaada (mkopo) kwa huruma.
 
Topic hii ndo inagusa tatizo letu kubwa na ndo maana imeonekana haina mvuto.wachangiaji wameingia mitini maana topic hii inagusa Wabunge wote wale wanaojita wapiganaji sijuhi watetezi sijuhi nini....wanagombana kwenye mambo ya ovyo
 
wangunge 45 wa chadema(sina hakika) x Tshs. 25 000 000 = Tshs. 1 125 000 000

wabunge wetu onesheni mfano. changisheneni kila mbunge m25. tafuteni mahala penye uhitaji mtoe mchango wenu. ama mubuni mradi endelevu wenye manufaa ya moja kwa moja kwa jamii.

Wabunge wa CHADEMA that is enough seed money for you to start on sustainable projects for the youths ambao hawana employment; hasa za kilimo...Hizo hela mkizifanyia project planning nzuri kwenye constituence zenu ni campaign tosha kubomoa ngome za chama tawala...

Wapinzani badala ya kuendelea na malumbano yakisiasa fanyeni kitu cha maana ku demonstrate capacity yenu katika good governance kwa any available resources.
 
hahaha...akili bado zimelala! Mtu akikwepa kulipa kodi ni kosa la jinai...lakini hataki kujua hiyo kodi yake imetumikaje!!
 
hizo kodi (P.A.Y.E) unazosema hawakatwi wazazi wao. hawana haki ya kudai kodi wanayokatwa vibopa wanaokurugenzi mashirika mbalimbali ya serikali (ambao kimsingi hawa ni watawala wenyewe au watoto wao).

au gunia mbili za mahindi anazovuna mzee Ng'wanidako kule kijijini zinakatwa P.A.Y.E? kama ni hivyo sawa. waendelee kudai. vinginevyo waingie kitaa kama Tunisia na Masri. au wanyamaze tu waendelee kupewa msaada (mkopo) kwa huruma.
Sahihisho. Kutolipa Kodi ya P.A.Y.E haina maana kwamba wewe si mlipa kodi. Kuna kodi ya V.A.T (ongezeko la thamani ). Hii inalipwa na kila mtu kwa kila kitu unachonunua dukani. Iwe sukari, chumvi, nguo, unga, vyote vina hiyo kodi ya V.A.T na ndiyo inayoingiza mapato mengi hazina kuliko hiyo P.A.Y.E. Kwa hiyo mkulima wa kijijini naye ni mlipa kodi.
 
Mimi nafikiri ni kuandaa mgomo wa kitaifa wa nchi nzima, mgomo huu usiwe wa chama chochote uwe wa wananchi wenyewe kupinga pamoja na hili la kwako mengine yafuatayo
1) Mfumuko wa bei na huduma duni za kijamii ( Hostpitali, Maji na Umeme)
2) Umaskini - matokeo ya matumizi mabaya ya fedha za umma
3) Kutaifisha mitambo ya Dowans sababu iliingia kitapeli tapeli
4) Makambi yote ya jeshi yaondolewe haraka kwenye makazi ya watu

Kwa sababu sisi wananchi tumeiweka serikali hii madarakani basi tunaweza kuiwajibisha maana inaonekana wabunge wetu wameshindwa kututetea inavyotakiwa
 
Back
Top Bottom