Wanafunzi, Vijana na Wananchi Tukutane Mnazi Mmoja Ijumaa Tarehe 02/04/2011

Maandamano ni ya amani na twendeni February 4, 2011 kutaka serikali ya CCM kuondoka Tanzania. Hakuna kitu tunategemea toka CCM, tumewapa miaka 50 na inatosha.
 
Du mtoa mada ungeanza kwanza kwa kujiunga na maandamano ya CUF 07/02/2011 hukohuko DSM, kwani mnapotengana na kung'ang'ania eti vijana na wananchi tuandamane 02/04/2011 ni mbali kwani malipo ya dowans ndiyo yatakayowasha moto bila kusubiri maandalizi yako.
Hata hivyo BRAVO sana kwa kampeni zako tutakusaidia lakini sio kwenye mtandao, lazima tuongeze na matangazo mengine yanayowafikia walengwa wote wanaoumia
 
Nachanganyikiwa na baadhi ya mambo hapa hivi ni kwa nini watu hawataki kujifunza na kuchukua hatua?

Mgaya wa TUCTA ameandaa ya kwake na hataki wanasiasa waingilie anadi wasije kuingiza mambo ya siasa kupitia wao na maandamano yake yanashonewa sare kabisa wakati wanaoteseka ni wananchi wengi tuseme karibu wote swali kwani nchi inaongozwa na nani kama siyo wanasiasa ambao watu hujiunga nao kutokana na hoja na sera zao na siyo kundi fulani kama wengine wanavyotumia fimbo ya udini.

Wanavyuo nao hawataki wanasiasa waingile mambo yao na wao wanataka kuandamana kivyuovyuo na kupigwa na kuuawa kama kule dodoma na mambo yanaishia chinichini' nini kwani chuo si cha kwao mtawafanya nini mnasoma kwa msaada (nashindwa kuamini)

CUF nayo wanaandaa ya kwao kuanzia buguruni kama kawaida na nimemsikia Mtatiro amesema na yeye ana intelijensia yake na ana uhakika maandamano yatakuwa ya Amani na polisi wasilete intl.zao za kizushi maana ya kwake ni ya uhakika zaidi hii ni kama nimeitamani lakini hawa jamaa hawaaminiki kabisa inajulikana kama ccm b. Na wanatafuta kazi zaidi kama aliyopatiwa maalim Seif (samahani hivi Zanzibar kuna rais?)

Viongozi wa dini na wao wameganyika kidini ambao viongozi wa dini ndiyo waliohakikishaga kuwa Yesu Kristo anasulubiwa hawa wengi ni wanafiki wakubwa sana na wavurugaji wa kwa kutumia nafasi zao maana watu wengi wanawaamini sana kuwa wanaweza kuwapatia maisha bora ya umilele lakini wanaingiza siasa kulingana na ushabiki wao na kutumiwa vibaya na wanasiasa huku maisha magumu yakiwaadhibu kila mtu bila kujali aina ya dini yake na chama chake maana hata hao VILAZA WANAOJIITA WANA CCM. Wamechakaa na maisha na huku wamevaa kofia na vilemba vya uchaguzi wa 2005 akidai hicho chama kinamfaa. Hapohapo waisilamu wameshaingia mtegoni wakiamini kwamba mabadiliko yanayotakiwa na CDM.ni ya kikristo zaidi na waisilamu wao maisha yao yako sawa.

Nimesikia tena CDM. Wao wameandaa ya kwao Tarehe 28 na kila karibu watu wote hawa kilio chao ni kimoja lakini tatizo hatujajipanga kwa mtindo ambao utabadilisha sura ya kisiasa kama tunayoyaona Tunisia Misri na kwingineko ninachokiaona hapa zaidi ni ubinafsi zaidi na wachache wanaojitafutia umaarufu wa kisiasa.

Kwa haya ya CDM. Nitakwenda hayajaonyesha kuwa ni ya kwao wenyewe bali ni ya watanzania wote hayana sare na hayajasema ni ya watu wa dini gani wala wao hawatafuti kazi kama maalim Seif na kundi lake maana Lipumba ameshatoswa ila pamoja na kuwa Prof. Hajastuka tu na mashaka gorofani kwake yukoje.

Tuache mambo ya ushabiki hapa hebu tuangalie ukweli halisi kuwa ni chama gani kwa wakati huu kina nguvu ya kuweza kuwakusanya wananchi kona zote za Tanzania na kinasikilizwa na aina nyingi ya jamii na kuungwa mkono then kwa pamoja twendeni kwenye maandamano kwa HOJA ZA KITAIFA NA SIYO KICHAMA NA KIDINI KI TUCTA NK.

Na Polisi ambao wao ni kama maroboti wakae mbali maana hata wao wamechoka mbaya kama hawatasikia kuna Jeshi ambalo linajua mipaka ya kazi yake na yatawakuta yale ya Misri.

Nitahudhuria maandamano yaliyoandaliwa na Chadema maana ndiyo sauti ya wengi na sauti ya wengi ni sauti ya Mungu na ndiyo waliokurupua mambo mengi ya mabadiliko ya kisiasa hapa nchini.

Shime!!! shime!!! Hima!!! Hima!!! Watanzania tuuungane kona zote za nchi kuleta mabadiliko ya kweli na kuacha ubinafsi wa kimatabaka na tusitumiwe vibaya na watu wasiopenda maendeleo na mabadiliko ya kweli.

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA MUNGU WALAANI WOTE WENYE NIA MBAYA NA NCHI HII KWA UFISADI NA MATAKWA YAO BINAFSI. Amen
 
Tanzania ilipata uhuru wake kwa njia ya mazungumzo/ya amani na kumuondoa mkoloni nchini. Hali hii ndio imetujenga watanzania kutumia zaidi njia ya mazungumzo kupigania haki zetu. Ni njia hii ambayo tukiitumia itaondoa madhara mengi yatokananyo na maandamano. Kwa mfano, baada ya kuomba katiba mpya serikali imekubali kulifanyia kazi tofauti na nchi nyingine ambazo mpaka kutokee ghasia na vurugu ndipo hatua huchukuliwa. bado tuna nafasi ya mwisho ya kuishinikiza serikali kudai haki zetu kabla ya maandamano ingawa sipingi kuandamana kama ndio suluhisho la mwisho kabisa si suluhisho la kwanza.
 
uzoefu unaonyesha kwamba nchi za kusini mwa jangwa la sahara zinadai haki kwa njia tofauti na nchi za kasikazini mwa Afrika. Hii imejengwa katika historia. kuwakusanya watanzania nchi nzima leo sio rahisi kama ilivyo kwa nchi za kiarabu. Tunahitaji maandalizi ya kisakolojia zaidi kwa watanzania kuliko kushawishi kwa njia ya blogs pekee ambayo huwafikia watanzania wachache. Naaona kwa sasa tuahirishe maandamano haya hadi hapo baadaye.
 
Watanzania walioko nje ya nchi huchochea maandamano kwa sababu kwa nchi za ulaya ni sehemu ya utamaduni uliozoeleka kwa wengi lakini watanzania ndio wanajifunza kuandamana. Sura ya kuandamana kwa kila jambo haijaonyesha kufanikiwa kila wakati na hasa kama njia tofauti hazijafanyia majaribio kiasi cha kutosha.
 
Mmeomba kibali cha hayo maandamano maana isije ikawa intellijensia tena!

Hakuna kuomba kibala, kinachotakiwa ni kumpa taarifa tu mkuu wa wilaya kabla ya kufanya maandamano. Ni kazi ya mkuu wa wilaya kuhakikisha watu wanaoshiriki kwenye maandamano wanakuwa salama.
 
ni kweli hayo ni maandamano ya chadema. maandamano yanafanikiwa endapo tu yatabeba utaifa na hayatachochewa na itikadi za kisiasa bali utaifa. Kila chama kikiamua kuandamana wananchi watakosa umoja wa agenda za kitaifa hivyo maandamano hayo yaondoe mkono wa chadema ili yabebe utaifa, sisi wote tujumuike kuandamano bila kujali huyu ni CCM, CUF au CHADEMA
 
my worry is maandamano haya ni ya watanzania wote au ni ya wanachadema tu. yanaonekana kupangwa kichama chama ni kutuogopesha wengine
 
Niliposikia maandamano ya chuo kikuu sehemu ya mlimani leo nikadhani ndio maandamano haya kumbe chadema wametoka kivingine kuibukia chuo kikuu. mmmmmh ni kama naota njozi mwaka huu watoto wa wakulima watafukuzwa vyuoni. kuandamana kunahitaji machache ya kulisoma jicho la serikali likikutazama kwa makengeza shule huna wewe mtoto wa maskini kule kijijini. Suluhisho ni kwa serikali kukaa kuangalia upya matatizo ya wanafunzi nchi nzima ili kuondoa malalamiko yasiyo ya lazima.
 
Ya Arusha hayajatokea tena leo? Tuombee maafa yasitokee vijana wetu waendelee na shule.
 
Kwanza asante saana kwa ujasiri ulionao lakin pili nafahamu kuwa yanayotokea pande nyingine za dunia yalianzishwa km hivi lakini hii tarehe 02/04/2011 nimeshindwa kuilewa kuwa ni tarehe mbili mwezi wa nne mwaka 2011 au ni tarehe nne mwezi wa pili mwaka 2011 kwa maana tarehe mbili mwezi wa nne itakuwa jumamosi na tarehe nne mwezi wa pili ni ijumaa, naomba ufafanuzi.
 
Kalagha baho............. nakuhakikishia kama agenda ndiyo hizo hupati mtu ngo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Hata huko misri na Tunisia hawajaweka agenda za maswala ya rushwa wala uchama. Wewe ukishaindoa CCM ndio katiba itaandikwa na watanzania au itaandikwa na CHADEMA, NCCR etc? Hujaona CUF waliandika yakwao huku wakisistiza kuwa ndiyo wananchi wanayoitaka? Ukitaka kuwaweka wananchi wote pamoja sema tu "hali ngumu ya maisha" hii ndiyo best agenda. Ninachoweza kusema hapa kwetu maadili hakuna kabisa na hivyo haa ishuke katiba au kiongozi kutoka mbinguni kama hatuta badilika tutaumia tu.

Mwisho natoa mwito kwa wananchi kutokubaliana na watu wachache ambao maslahi yao ya ungozi hasa CHADEMA wanaotaka kuwa viongozi kwa namna yoyote ile kama mbowe alivyosema anaandaa bajeti rasmi ya kuiadhabisha CCM bila kujali watakaokuwa wanateseka ni kina nani, watakaokufa ni kina nani. Namshangaa mtoa mtoa mada kusema Mauaji ya Arusha serikali inaficha ukweli lakini hasemi ukweli upi kwamba Dr. Slaa na Ndesamburo waliwahimiza wananchi kwenda kuwakomboa viongozi wao walioshikiliwa katika kituo cha kati?? Eti mbona siku ya maziko hakukua na fujo wakati polisi hawakuwepo? Ungejaribu kuafanya fujo uone cha mtemakuni, kwa taarifa yako tulikuwepo kiraia la kini tukiwa kamili na ingekua za moto tu!!!! pili siku ya mazishi kumbuka Mh. Lema wa Mh. Mbowe kila mara walikua wanawahimiza vijana kutulia ili waiabishe serikali ya CCM ikiwa na maana kama wangefanya hivyo siku ya tukia la vifo kusingetokea kilichotokea. Agenda ya CHADEMA tushaijua na wale viongozi wote wasiyowastaarabu wanaotumia mabavu kuliko akili na utashi na kuangalia maslahi ya wengi watakiona pamoja na wewe unayetaka kuleta uhuni hapa nchini.

Kumbuka hii nchi siyo ya CCM au CHADEMA ni ya watanzania wote na pia si nchi ya vyama viwili ni nchi ya vyama vingi. What is going on in Tunisa, Egypt and elsewhere will never happen in Tanzania nakuhakikishia.
Usiwe na fikra mgando ndugu yangu unafikir huko Tunisia na Egypt walianzia from no where. Matatizo wanayoyapa hasa hali ya uchumi kuwa mgum ndo kilichosababisha yote hayo je kwetu tanzania matatizo kama hayo hayapo
Ebu angalia bei za mafuta zilivyo juu kwa sasa ukilinganisha na mwaka 2005 kabla Kikwete hajaingia madarakani
Ebu angalia bei za umeme
Ebu angalia bei ya maji
Ebu angalia bei za usafiri
Ebu angalia bei gesi
Ebu angalia mfumuko wa bei ya vyakula
Ebu angalia shilingi yetu inavyopolomoka dhidi ya dola
Ebu angalia tatizo la ajira Tz
Ebu angalia migomo inavyolindima Tz
Kutokana na matatizo hapo juu ww unafikiri uelewa wa WaTz uko vile vile ukilinganisha na miaka ya nyuma acha mawazo mgando nakuambia ipo siku patachimbika hapa patakua padogo ebu tukae chini tujadiri vizuri mstakabari wa nchi yetu sio kuropoka tu.
Fikra zako ni duni sana ipo siku haya unayosasema hayawezekani yatawezekana tu.
 
Usiwe na fikra mgando ndugu yangu unafikir huko Tunisia na Egypt walianzia from no where. Matatizo wanayoyapa hasa hali ya uchumi kuwa mgum ndo kilichosababisha yote hayo je kwetu tanzania matatizo kama hayo hayapo
Ebu angalia bei za mafuta zilivyo juu kwa sasa ukilinganisha na mwaka 2005 kabla Kikwete hajaingia madarakani
Ebu angalia bei za umeme
Ebu angalia bei ya maji
Ebu angalia bei za usafiri
Ebu angalia bei gesi
Ebu angalia mfumuko wa bei ya vyakula
Ebu angalia shilingi yetu inavyopolomoka dhidi ya dola
Ebu angalia tatizo la ajira Tz
Ebu angalia migomo inavyolindima Tz
Kutokana na matatizo hapo juu ww unafikiri uelewa wa WaTz uko vile vile ukilinganisha na miaka ya nyuma acha mawazo mgando nakuambia ipo siku patachimbika hapa patakua padogo ebu tukae chini tujadiri vizuri mstakabari wa nchi yetu sio kuropoka tu.
Fikra zako ni duni sana ipo siku haya unayosasema hayawezekani yatawezekana tu.

Kati ya matatizo hayo katika ngazi ya familia umejaribu kutatua mangapi na mangapi yameshindika kwa sababu zipi?
 
Back
Top Bottom