RedDevil
JF-Expert Member
- Apr 30, 2009
- 2,367
- 1,519
WanaJF, kuna tetesi kuwa, mpaka sasa ni wiki ya tano inaingia tokea mhura wa pili ulipoanza lakini bodi ya mikopo haijaweza kuwapa wanafunzi fedha za kujikimu, na hali ni mbaya haswa kwa dada zetu na wale watoto wa masikini wasiokuwa na ndugu hapo dar. Wanafunzi sasa hawawezi kusema kwani wanaogopa kufukuzwa tena. Hebu nisaidieni ni kweli jamani, serikali pamoja na uongozi wa chuo haujui kuwa hawa ni binadamu kama wao wanahitaji kujikimu ikiwa ni maradhi pamoja na mahitaji mengine ya kibinadamu. kazi kwenu wanaJF najua mnajibu zuriii, ambalo laweza hata kuwasaidia hawa wenzetu. Ikiwezekana, kama kunamwanaJF mpiganaji huru atembelee kimya kimya aulize atupe habari kamili ili tujue hatuna serikali siku hizi. Karibuni kwenye mjadala huu.