Maisha ya wanachuo kwa kweli yanasikitisha sana, lakini sidhani kama wakiongezewa posho watabadilika.
Makubaliana na wewe. UDSM na vyuo vingi vya elimu ya juu, kuna Culture fulani hivi ya ajabu sana na akina dada wengi hujihusisha nayo. Culture ya kushindana nani ana vitu vya bei mbaya na kuishi kama mtoto wa familia bora.
Huu utamaduni wa wanafunzi wa kike kuchukuliwa na mapedezee waliokubuhu kwenye ngono na kuishi na maambukizi ya kila aina maradi ya ngono pamoja na ukimwi kwa supply huduma za pesa kwa wanafunzi ipo siku nyingi sana. Hebu fika mabibo Hostel ujionee jinsi magari ya wazinzi wa mjini yanavyopishana. Zamani kabisa hali hii ilikuwa inaonekana Hall 3 na Hall 6 (Mabweni yaliyotengwa maalum kwa wanafunzi wa kike). Walikuwa na msemo kupigana 'EXILE' Yaani chumba cha watu wawili wanaambiana kuwa mmoja asirudi mpaka saa fulani kwa kuwa mwenzake atakuwa anampatia huduma pedezee wake.
Mbaya zaidi ni kwamba wazinzi wa mjini wanajitahidi sana kurubuni wanafunzi wa kike kwa kuwa tu mahitaji yao mara nyingi hupita pesa wanayopata kwa ajili ya show up kama (kutengeneza Nywele, kuvaa nguo na viatu vya kisasa kila vinapotoka, kununa simu za gharama, kujifanya hawaendi Cafeteria ya Manzese).
Ila kwa mwanafunzi anayejua lililompeleka anaweza kabisa kujiepusha na matumizi haya ya Ziada ambayo ndiyo chanzo cha kujiuza kwenye vyumba vyao, japo kwa wengi huwa na permanent suppliers of resources kama wanazo au hata kubadilisha kulingana na mahitaji.
Ukweli ni kwamba wanafunzi wa elimu ya juu ni watu wazima na wengi wanajua wanalofanya cha muhimu ni kuwapatia elimu ya UKIMWI badala kusingizia kuwa wanautafuta kwa kukosa hela ya kujikimu. Wengi wa wanafunzi hawa huingia kwenye biashara hii kwa tamaa na show up. Siku hizi mpaka wauza nyanya wa manzese kama wana hela wanafikiria kwenye kuonja wasomi wa mlimani, huku ni kujishusha sana.