Wanafunzi UDSM kuishtaki serikali. Wataka kiswahili kiwe lugha ya kufundishia.

Huyu "mwalimu" unayemquote mbona anarukia conclusions bila kuweka ground work yoyote? Relationship ya kusoma kwa Kiingereza na hiyo poverty iko wapi?

Kukaa ofisini kwa Engineer kunasababishwa na kusoma kwa Kiingereza kweli? Tuwe critical na hizi opinion jamani.

Tatizo lipo kwenye mfumo wa elimu kama nilivyosema mwanzo, haijengi creativity na out of the box thinking. Na culture ya kutothamini manual labour, ukikaa ofisini ndo unaonekana wa maana, ukipiga gazi "mbeba box".

Kaamua kulaumu poverty ya Naigeria kwa sababu ya lugha! Rushwa hajaiona? Ufisadi wa viongozi wao hajauona? Matatizo ya udini hajayaona? Vita wanavyopigana na waasi kwenye Delta hajaviona? Lugha is the least of their problems.

Sisemi umasikini hauchangiwi na kitu kimoja.Unachangiwa na vitu vingi.
Kitu ambacho ni common katika udhaifu wetu ni kwamba elimu yetu haitusaidii kudumisha mazingara yetu.Kuna sababu nyingi kwa hii sababu moja ni kwamba walimu hawafundishi vizuri, vilevile mfumo wa elimu ni duni,lakini ukweli ni kwamba lugha inachangia sana.Nimekuuliza angalia nchi zinazotumia lugha za kigeni Afrika zimefika wapi? Jibu kwanza hilo swali.Hizo nchi zimetumia English au French kwa miaka zaidi ya sitini sasa, sisi matumizi ya lugha zetu ni makubwa zaidi lakini manufaa yanaonekana katika amani na mambo mengine.

Ndio tuna uongozi mbaya pamoja na mafisadi umesdaidia kuleta umasikini lakini underlying reason ya kuwa duni katika sayansi na kushindwa uvumbuzi ni kuchukulia elimu kama kitu kigeni lakini tukiifanya ya kwetu na kusoima katika lugha zetu hata watu wa kijijini wataelewa na kufaidika zaidi.Kiingereza sio kitu.Jamaica na Haiti wana lugha zao za kigeni, kiingereza na kifaransa lakini wako wapi?

Mikaka ishirini ijayo tutafanya biashara zaidi ya China na vilevile brazil kuliko uingereza.Je itabidi tubadilishe lugha kwenda kireno au kichina?

Fikirieni zaidi!!
 
Companero;

Point nzuri hivi ndivyo tunavyofundishwa, sasa mnashangaa elimu yetu ni kama ya kasuku?
Kiswahili mpaka chuo kikuu na kiingereza pembeni ni wazo zuri sana!!
 
Sidhani kama ni akili ya wanafunzi wa UD lazima kuna FISADI PAPA amechungulia dili ya kubadilisha vitabu kotoka english to swahil coz to me its sound nonsense kwenye zama hizi ya uwekezaj ambao post zote zinazotoka qualification lazima uwe fluent kwenye english sa kiswahil ikipewa kipaombele??????????? labda kama serikali itachukua wahitimu wote kwenye kilimo kwanza hapo sawa.Au kuna malecturer wa kibongo lugha inawapa shida wanaamua kurahisisha kazi yao????
Na ni aibu kwa taifa kutoa wakufunzi wasioweza hata kujieleza kwa kiingerza its real shame.
 
Mzee2000;

Ushahidi kuwa lugha ndo inakwamisha hizo nchi zinazoongea Kiingereza au Kifaransa uko wapi?

Mbona Eritrea na Sudan hawatumii English lakini bado hawapati maendeleo?

Tena kuna Waafrika wengi wanaongea French kama first language, yaani kama Watanzania tunavyoonge Kiswahili, na bado maendeleo hakuna.
Sasa hapo tatizo ni nini? Kwani ubongo wa Mwafrika hauwezi kuelewa lugha kasoro za asili? Hakuna mtu anayezaliwa anajua lugha yoyote.

Hiyo ya miaka ishirini ni mawazo yako tu, hakuna mwenye uwezo wa kuona mbali hivyo. Na hao wachina ndo wako mstari wa mbele kujifunza Kiingereza so usiwe na wasiwasi.
 
Kang;

Kama mfano alioutoa componera kingereza sio lugha ya mama(mother tongue) kwa watanzania wengi na sio lugha ya kibantu kama lugha nyingine za kikabila za watanzania kwa hiyo ni logical tujifunze kwa kiswahili(lugha tunayoielewa) na kiingereza iwe lugha ya pembeni.

What is complicated about this?
 
Mzee2000;

Point ni kuwa hata Waafrika ambao Kifaransa kwao ni lugha mama bado wamekosa maendeleo, kwa hiyo kutomia au kutotumia lugha mama sio kitu kinacholeta maendeleo.

Hakuna kitu kama lugha tunayoielewa, tuna uwezo kama binadamu kuelewa lugha yoyote tukifundishwa vizuri.
 
Point ni kuwa hata Waafrika ambao Kifaransa kwao ni lugha mama bado wamekosa maendeleo, kwa hiyo kutomia au kutotumia lugha mama sio kitu kinacholeta maendeleo.

Hakuna kitu kama lugha tunayoielewa, tuna uwezo kama binadamu kuelewa lugha yoyote tukifundishwa vizuri.

Umuhimu wa kutumia Kiswahili elimu ya juu ni huu.


1) Kiswahili ndio lugha inayoongelewa karibu na watanzania wote.Tukifundishia Kiswahili na kufanya kiingereza kama lugha ya pili elimu itakua kwa kuwa vijana na waalimu wataelewa zaidi wanachofundishwa/ kufundisha.


2) Vijana karibu wote Tanzania wanatumia Kiswahili madarasani tu, wakitoka hawaongei tena.Tukitumia Kiswahili e elimu itakuwa internalized kwa kuwa wanafunzi watajifunza kukabili matatizo yao kwa lugha yao sio kama ilivyo sasa hivi.

3) Nchi zinazoongea kiingereza kama first language sasa hivi, kwa mfano marekani na uingereza uchumi wao unakuja chini na muda si mrefu superpowers zitakuwa asia na south amerika.Kwa maana hiyo tutakuwa tunafanya zaidi biashara na wa asia.Je itabidi tubadilishe tuongee kichina.


4) Je asilimia 90 ya wananchi walioko vijijini kiingereza kinawasaidiaje?Hawa watu wanapampana na mazingara yao kutumia local knowledge,Kiswahili ndio lugha inayowasaidia kukuza kilimo kwa kuwa wataalamu wetu wote wanaongea lugha hiyo.Hivi hujui lugha inaendana na tamaduni?Je mtu wa kijijini anajua snow ni kitu gani? Uoni kuwa Kiswahili kinaendana na tamaduni na mazingira yetu kuliko kiingereza.


5) Kwa sasa asilimia isiyozidi nafikiri tano ya watu (tena hawa wako mjini) ndio wanafanya kazi ambazo wanatumia kiingereza mara kwa mara(hasa kwenye NGO na kampuni za kigeni na mahouseboy wa wazungu).Je hizi sekta wanazofanyia kazi zimechangia uchumi Tanzania kiasi gain?Je unaweza kulinganisha na asilimia tisini ya watu ambao hawatumii kiingereza wanavyozalisha chakula cha watanzania n.k?


6) Tukianza kutumia Kiswahili zaidi ya asilimia tisini ya watanzania ambao wanakijua watapata matumaini ya kujifunza vitu ambavyo otherwise wasingevijua.Je itachukua muda gani kuwafundisha hawa watu kwa kiingereza wakati wataalamu wa kiingereza hatuna?


7) Tatizo la taifa letu sasa hivi ni nini?Tunahitaji kilimo bora pamoja na uchumi unaoweza kufanya manufacturing. Hawa wakulima kiingereza kitawasaidiaje?Tujenge na tuendeleze pale tulipo, manufacturing inahitaji basic science.

1) Kujifunza kiingereza mpaka chuo kikuu kitatupa taifa na watu wetu elimu ambayo itakaa kichwani(darasani na nje ya darasani which is sustainable) na kutupa confidence ya kugundua na kusustain teknologia yetu wenyewe.Tutaondokana na mawazo ya kikoloni ya kufikiria kuwa mtanzania ili aendelee lazima afanye kazi kwenye kampuni ya mzungu.Wewill develop our own solutions based on our own problems.We will look less to the west since we will have our own knowledge which is based on our own language.

Mnaosema kiingereza mnafikiria short term solutions ehh tujue kiingereza ili tufanye kwenye kampuni Fulani ya wazungu why not create our own industries.kiingereza ni lugha tu, mtu kama unajua concepts na ujasoma kiingereza utabrush lugha miezi mitatu tu na utaweza kuongea.But scientific concepts are the hardest to grasp.

Kwa hiyo ninachosema ni kwamba tuanze kuintroduce Kiswahili kwenye elimu ya juu polepole,na sisemi kwamba kiingereza tukiache NO.kitumike pempeni kama zinazofanya MAJORITY ya nchi zilizoenda. Otherwise in the longer run we are damned, and I tell you this for sure!!!
 
Point nzuri hivi ndivyo tunavyofundishwa, sasa mnashangaa elimu yetu ni kama ya kasuku?
Kiswahili mpaka chuo kikuu na kiingereza pembeni ni wazo zuri sana!!
Alafu ukitoka hapo unategemea kufanya kazi wapi? na waswahili?...
 
Ama kweli mfa maji aachi kutapatapa...
Sasa imekuwa issue ya kutokuendelea ni kiswahili, Je hao wanafunzi wanafahamu hizo nchi walizozijata especially turkey wana insist english pia. Yani ktk sifa za muomba kazi anatakiwa kujua english - inglizce bilen.
Mwanafunzi akipata admission au akisoma dept ambayo 100% wanafundisha kwa kiingereza anaonekana wa maana na kazi anapata kirahisi zaidi. Tumesoma dept za kituruki lkn walimu wanakataza kusoma reference za kituruki maana translation inakuwa na mapungufu fulani. Angalia nchi kama Nigeria wanatumia english, Ghana pia. Nigeria ni mojawapo ya nchi zenye maendeleo barani africa.
Uwezi kuanza degree mpaka ufanye english exam. Wengi wao hawajui inglish but they are not happy about this. Wanatuonea wivu sisi wabongo na nchi za kiafrika maana straight tunaingia exams na kupasua.

Kwa kifupi english inatakiwa kwa sababu ni international language. Vile vile nchi yetu bado masikini sana yani issue ya maendeleo sio lugha.

Ufisadi umezidi.. viongozi wengi wazembe...yani tatizo ni serikali na viongozi wake. Lugha haina nafasi hapo.


Nafikiri ukifikia hatua ya kutokuwa tegemezi ndio unaweza kuanza kufikiri mambo ya lugha. Ikiwa hadi mchele to import ujue hali ni mbaya sana na ni better tuka focus kwenye mambo ya maana.
 
if i imagined myself studying physics in swahili i would have never understood as well..,kwa sampuli ya maneno kama mwendo kinyume kasi-decerelation,teknohama etc..,ni bora tuendelee kutumia kiingereza,kiswahili ni lugha changa kwenye dunia ya sasa,kila kitu kinabadilika kwa kasi ya ajabu,hata kiingereza chenyewe hakitoshi.

nyie mnaosema kiswahili kitumike mnafahamu watanzania wengi hawafahamu kiswahili fasaha?kwanza waanze na project kiswahili fasaha kwa watanzania wote,like to get to university kila mwanafunzi anatakiwa afahamu kiswahili fasaha(by passing swahili fasaha exam).wanaopasi wafundishwe kiswahili.

si vizuri kuanza na project muhimu kwa taifa kama hii kwa mkupuo.yaleyale ya shule za kata,kunatakiwa kuwe na trials za miaka 10 atleast kuanzia sekondari hadi university,zitengwe shule maalum za kiswahili full suit.from baiolojia to kemia.kila kitu kiwe kiswahili kwenye shule hizi.kiingereza kiwe kama somo..,hawa wakifaulu vizuri sana chuo kikuu,wakipelekwa makazini japo kwa niaka miwili wakiwa na perfomance nzuri basi tunaweza kukirithisha kiswahili kuwa lugha maalum ya kufundishia.

kwa nini nimesema hayo,kama mwanasayansi naamini katika sampling of specimens,huchukui watu wote duniani na kuwadunga virusi vya HIV na kuwapa a rial medicine eti unafanya majaribio ya dawa mpya usiyokuwa na uhakika wa uwezo wake.

Nakubaliana na uwepo wa kiswahili kwenye mitaala na vitabu vyetu,Lakini tuwe makini..,watanzania wengi hawafahamu kiswahili fasaha,tukiweka mitaala hiyo kwa nchi nzima watu watakuwa na mzigo wa kujifunza kiswahili na kingereza.

kama nilivyoandika huko juu,tuanze na sample schools.hizo kila kitu kiwe kiswahili fasaha,then niversity wachague kozi maalum kutoka kila kitivo ku-elimisha wanafunzi hao.naamini hata maprofesa wanatakiwa wapelekwe kozi za kiswahili pia.

tusifanye makosa ya shule za kata,wanafunzi wanajaa madarasani mwalimu ni vodafasta au hayupo kabisa.
 
One of the country developed without using its language is America, English wasn't an american language before the British invasion. Many young people in south Africa died becasue they wanted to be taught in English (International language). we are now in globalisation not in colonial era. we want our graduates to be internationally competitive in the job market. wakenya wanachukua vibarua vyetu just because of they speak English. anyway let them go we can know their nosense.

Bahati mbaya hakuna kitufe cha "dislike", vinginevyo ningebonyeza mara ishirini kwa lugha uliyotumia.

Kama "Dislike X 20!
 
Hapo kwenye lugha ya kufundishia.., Kuna sababu kwanini Latin ni lugha ya kisayansi...; vilevile kabla hatuaweka uzalendo mbele kabla ya uhalisia na kuangalia faida na hasara lazima tujiulize.., ni vitabu vingapi na volumes ngapi zinazoelezea mambo ya elimu katika lugha ya kiswahili ? Mtandao / Tovuti imeshakuwa ni sehemu ya kupata information kuliko hata kwenda maktaba, sasa kama kijana akitaka kujua kuhusu Newtons Laws of Motion je itakuwa rahisi kwake aki-google kwa kiswahili ili aweze kupata maelezo au akitumia Kingereza ambacho kuna maelezo zaidi ?
 
Bwa-ha-ha-ha-hah...!
Tumethubutu, tumejaribu, tumeshindwa.

Nukuu: UNESCO considers that "providing education in a child's mother tongue is indeed a critical issue"
 
Back
Top Bottom