Wanafunzi UDSM kuishtaki serikali. Wataka kiswahili kiwe lugha ya kufundishia.

Hao wanafunzi waache kupoteza muda, kama wana kipenda sana kiswahili basi wote wakafanye PhD za kiwahili.
Kwanza ni waongo china kupata ajira safi ni mpaka uwe unaongea kiingereza. Universities kwa bachelor wanafanya CET4 college engilish test tena 4 credits na CET6 also 4 credit ukilinganisha na masomo mengine 1-3 credits na it is a compalsory subject. kuingia master na phD pamoja na masomo mengine lazima ufanye mtihani wa kiingereza na ufahulu. kwa sababu lazima waelewe research na technologia za nchi zilizoendelea maake uko ndo wanakoiga.hapa mtu anadanganya kwamba wachina wameendelea kwa kutumia lugha yao. lazima ujue maendeleo ya wachina imeletwa na watu wachache hawa wanatumwa na comunist party kusomea technologia ulaya na america. wakirudi technologia waliosomea inatekelezwa jinsi ilivyo.
 
kigugumizi;

Of course, hoja zao ni nzuri ila wanajifananasha na nchi ambazo zilianza kutumia lugha yao tangu mwanzo. Sisi siyo hivyo na kubadili mfumo huu kwa sasa utatugharimu sana. 'Programmes' nyingi (au zote) za kufundishia bado ziko kwenye Kiingereza na hatujawa na msamiati wa kutosha. Hebu angalia tu Kamusi yetu ya Kiswahili ilivyo ukilinganisha na 'dictionaries' za Kiingereza au lugha nyingine. Tungekuwa na Kamusi inayojitosheleza hapo ingekuwa hatua nzuri.

Mimi nadhani tungeenda taratibu. Mfano, vitabu vya Kiswahili viwe vingi kwanza, tukuze msamiati wa Kiswahili, nk. Mabadiliko mengi yanakuja kutokana na mahitaji na uwezekano wake. Bado tuna kazi kubwa ya kufanya ila sisi tunataka njia za mkato tu.

Nchi wanazozitaja kama China, Urusi, Uturuki, Sweden, Uingereza, Norway na Ubelgiji zina uwezo mkubwa wa kufanya mambo yao wanavyopenda wenyewe. Sisi bado ni taifa tegemezi. Kwani ni nchi gani kati ya hizo imeshakuja kuomba msaada au mkopo kutoka kwetu? Lakini sisi kila siku utasikia tumepata mkopo huu, tumesaidiwa hiki nk.

Kwa hiyo, huwezi kujilinganisha na nchi ambazo zina uwezo wa kupanga na kutekeleza malengo yao jinsi wanavyotaka. 'Programmes' zote za masomo na vitabu ziko katika lugha zao. Karibu kila kitu kwetu kiko kwenye lugha ya Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani nk. Kweli tuna kitu hapo?
 
Last edited by a moderator:
Mzee2000;

China walianza kutumia lugha yao kwenye elimu tangu mwanzo na sisi sivyo. Halafu kuelewa 'concept' ya kitu hakutegemei kujifunza kwa Kiswahili, inategemea zaidi ulivyofundishwa na kuelewa. Sisi tuna matatizo mengi sana.

Na si tatizo la lugha tu, bali pia tunafundishwa kijuujuu sana. Mimi ningefurahi kama Watz wangependa kujiendeleza. Lakini Watz wengi wanataka mafanikio bila shida (bila mbinu nzuri za kutafuta mafanikio). Tatizo ninaloliona ni kwamba kwenye jumuiya ya Afrika Mashariki, Watanzania tutakuwa vibarua.

Kazi nzuri zitafanywa na Wakenya, Waganda, Wanyarwanda na Warundi. Nilisikia Kenya imeanzisha mfumo wa kutoa elimu ya sekondari bure. Sisi hatuna mkakati mzuri wa kuwawezesha Watz wengi wasome na wawe wabunifu. Viongozi wetu wanafuja mali ya umma kwa mambo binafsi!

Halafu pia tunatumia fedha nyingi kwa mambo ya anasa ili tupate heshima na hivyo kushindwa kufanya yale ambayo yangetuletea maendeleo. Ndiyo maana (kwa mfano) jiji la Dar es Salaamu linanuka kama limeoza, utaratibu wa usafiri ni mbovu sana, takataka kila sehemu nk wakati tuna wataalamu wanaoweza kutushauri kuboresha mazingira na huduma za kijamii.

Yaani, inaonekana hakuna tunaloliweza na hata kama tutatumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia bado watu wataghushi vyeti, wanafunzi wataibia mitihani nk... Kwa nini? Kwa sababu tunataka kutumia njia za mkato kupata mafanikio!
 
Magobe T;

Tafadhari kama mtu unabisha hapa toa mfano wa nchi afrika iliyopata manufaa ya kisayansi kwa kutumia lugha za kigeni, jibu, hakuna. Miaka ishirini inayokuja uchumi wa China utazidi wa Marekani (this is fact) which means kiingereza kitashuka chati, je itabidi wabongo turukie tena kichina tuache kiingereza?

Haitawezekana, lazima tujijenge kwanza kwenye lugha zetu kabla hatujaanza kuparamia lugha za watu wengine.Brazil vilevile inakuja juu sana, na ni miaka michache tu ijayo watawazidi waingereza, je itabidi tuache kiingereza na kuanza kujifunza kireno?


Angalia wamalawi, wanajua kiingereza lakini wapo wapi? Nakumbuka Bongo kiingereza kimewasaidia wamalawi kuwa ma houseboy kwenye nyumba za wazungu (nakumbuka wamalawi walikuwa wanapendwa sana na wazungu) na nasikitika kuona wapo wasomi hawalioni hili (inabidi akili zenu zenu zisafishwe kwanza na mental slavery) kila kitu mnachofikiria mna direct kwa wazungu tu …

Jamani tufikirie mbali, tatizo letu sisi tuko short sited, vitu havi vinafanywa pole pole tunaanza kidogokidogo mwishowe tutaweza.Ni wataalamu wangapi ambao kiingereza ni secod language?

Halafu don't say we are too late we are not late! Imewachukua wachina miaka hamsini tu wakitumia lugha yao kufika pale walipo, na sisi inawezekana kabisa, kimombo sio elimu ! Tukiondoa rushwa na kujiamini mambo yanawezekana.

Mendeleo sasa yanahama kutoka kwenye nchi zinazoongea kiingereza (uingereza na marekani) na yanaenda Asia kwa hiyo kiingereza kitaisha chati muda si mrefu.

Angalia Msomi mmoja aliyefanya utafiti kuhusu suala hili na conclusion yake someni hapa chini.

Bearing in mind that language influences the thought process of the learner, this understanding of his environment and thus the learning of science, deliberate efforts should be made to enable students learn science in their mother tongue as much as possible. The idea of forcing students to think in the foreign language as advocated by Dikshit (1974) is unproductive. It does not help students to be creative but reduces them to "robot" who merely memorize the notes given to them by their teachers and reproduce same when required without demonstrating appreciable degree of understanding of the scientific and technological information and process under consideration. If students merely memorize facts, principles and generalizations only to be regurgitated during examination, they will not be in a position to use the knowledge acquired since it has not been intemalized.
The lack of internalization of scientific knowledge, process and skills by Nigerian students seems to have been largely responsible for Nigeria's inability to make a major breakthrough in scientific and technological development. The situation is unacceptable and needs urgent redress.
 
Last edited by a moderator:
Jamani uongo mbaya kiswahili hakitupeleki popote,bora hata kiingereza kingekuwa lugha ya kufundishia tokea primary school.
 
Mwalimu Gervas Zombe kateta vizuri hapa,

English vs Kiswahili: Tanzania at Crossroads



- ADVERTISEMENT -
spacer.gif
spacer.gif
spacer.gif
spacer.gif
lg.php

spacer.gif
spacer.gif
spacer.gif
spacer.gif
The recent thinking in Tanzania that instructing by means of Kiswahili in secondary schools and colleges diminishes learners’ ability to acquire jobs is a fallacy. If thinking and innovation are pegged on the knowledge of English language, why are the Chinese and Japanese, for example, influencing the world in spite of their deficiency in English? Why is Ronaldo - a Brazilian footballer who has no knowledge of English - feted in the world?
A country that frowns upon meaningful education will never prosper. ‘Education’ is not the mere hoarding of certificates and knowledge of numerous languages. Meaningful education should give rise to creativity, sound thinking, self awareness and productivity.
In Tanzania, the government recognizes that far from education aiming at inculcating writing, numeracy and communication skills, it is supposed to spur creative thinking; innovation; self awareness; work ethics and good character. In addition, it is out to make the learner relate the interconnection between the past, present and future; harness natural resources for progress as well as preserve and perpetuate culture.
Do any of these objectives state that the aim of education in Tanzania is to make Tanzanians know how to speak English? Tanzanians are at liberty to learn any language they desire. That's why many of them understand French, Latin, Russian, Germany and Arabic among others. My main bone of contention is why Tanzanians should give preeminence to English at the expense of Kiswahili in which many citizens are proficient.
Tanzania’s problems don't stem from lack of English knowledge or any other language. Many Tanzanians have lived in Europe. They understand a lot of English. However, this has not stopped them from being key obstacles to the country's prosperity. They are lazy and have no element of creativity. They copy that which is European and paste it on Tanzania. They don't believe in themselves. They value big titles and long prefixes to their names but can't think. Don't we see them? Most of them hold big positions in the government but offer no homegrown solutions to Tanzania's challenges. Their ‘imported’ solutions are mixing up the economy. Don't we see this?
Tanzania does not need multilinguists. It needs people who think. People who are innovative. People who are able to create opportunities. People who are not satisfied with the status quo but are always working at bettering themselves and the nation in line with the aims of education.
What are our leaders doing with available resources? Are the resources being harnessed for progress as stated in the aims of education? Aren’t the country’s resources being used to enslave Tanzanians instead of empowering them? While Tanzanians have been reduced to beggars, foreign nations on the other hand, by virtue of their ability to ‘think’ and ‘perceive’ opportunities, are profiting from the country’s resources.
Tanzania has highly educated people. It has professors who have more than three degrees in engineering- but they can't even build a simple bridge to enable their own cattle to cross! We have left this to the Chinese- the Chinese who neither know English nor Kiswahili, but are skillful, hardworking and creative. You will not find the Chinese in the office. They are always on the construction site. What about our engineers? Aren't they glued in air conditioned offices, perched on revolving seats? Is that what education should prepare us for?
Many highly educated Tanzanians are lamenting that they are unemployed. Why- when the country’s forests, wildlife, fish, minerals and fertile land are yet to be exploited? They have too many certificates but can't think. They can’t solve problems surrounding them. They can’t create job opportunities. They can't even ‘smell’ opportunities. They are not productive in their places of work.
Knowledge of English or amassing numerous education certificates does not spur development. Development is brought about by people who think soundly. Innovative people. Creative persons. Does repairing a vehicle, for example, call for English? If it were so, the Japanese would not have dominated the world in car and electronics manufacture. All functional items we use are products of the mind and innovativeness. A doctor is handy not by virtue of his ability to speak a foreign language but his skill to treat. Tanzanians are taking their heart patients to doctors in India who don't understand English but are experts in heart operations.
A language, in itself is never employed but rather, someone's ability and competitiveness to perform a given task. That is why the Chinese are being awarded contracts to build stadiums while our professors, with their English, are being bypassed.
The growing emphasis of a foreign language at the expense of the country’s national language is inhibiting learning in Tanzania. This mistake has been condoned for a long time in several African countries which were under colonialism. In Mali and Niger for example, by the time a learner reaches college level, he will have studied in more than three languages. This creates confusion. No wonder, Mali and Niger are plagued with poverty to an extent that to them, development is a mirage. Should Tanzania walk the same path?
English ought to be treated like any other subject. Education should lay emphasis on skills, creativity and solving problems. Kiswahili is our language, our culture, our gift and pillar for development. God bless Tanzania. God bless Kiswahili.


By Gervas Zombwe
Mr. Zombwe is a Tanzanian based Teacher
 
VERY FAKE!hoja za ma-akademishians!practikalle kwa dunia hii kuna lugha ambazo GLOBALLY HAZIKWEPEKI!badilisheni lugha muone kama hata hilo box mtabeba
 
Jamani uongo mbaya kiswahili hakitupeleki popote,bora hata kiingereza kingekuwa lugha ya kufundishia tokea primary school.

Umewahi kusoma insha za Kiingereza wanazoandika wanafunzi wa Ualimu Chuo Kikuu? Kawaombe maprofesa wakuonyeshe. Utakutana na sentensi kama hii: 'I was cutting the road when the pik pik came'! Sasa hao watafundishaje kuhusu kuvuka barabara kwa kutumia Kiingereza?

Jamani naomba tutofautishe matumizi ya Kiingereza kama lugha ya mawasiliano na matumizi ya Kiingereza kama lugha ya kufundishia. Tuwekeze kwenye hilo la kwanza ili tukijue vizuri Kiingereza kama wenzetu wanavyowekeza huko Mashariki ya mbali. Katika hili unapaswa kuwa na mtaalamu anayejua kuifundisha lugha hiyo kwa mtu ambaye haijui. Hilo la pili tuliache maana halijatufikisha popote na halitatupeleka popote. Tufundishie kwa Kiswahili ili watu waweze kuelewa na kujifunza wenyewe kisha wavumbue 'shokomzoba' huko mitaani alafu Kiingereza wafundishwe pia ili waweze kuwasiliana na kukitumia kwa masuala mbalimbali.
 
Good poin companera

Angalia mwalimu huyu anavyosema

Tanzania has highly educated people. It has professors who have more than three degrees in engineering- but they can't even build a simple bridge to enable their own cattle to cross! We have left this to the Chinese- the Chinese who neither know English nor Kiswahili, but are skillful, hardworking and creative. You will not find the Chinese in the office. They are always on the construction site. What about our engineers? Aren't they glued in air conditioned offices, perched on revolving seats? Is that what education should prepare us for?

Many highly educated Tanzanians are lamenting that they are unemployed. Why- when the country’s forests, wildlife, fish, minerals and fertile land are yet to be exploited? They have too many certificates but can't think. They can’t solve problems surrounding them. They can’t create job opportunities. They can't even ‘smell’ opportunities. They are not productive in their places of work.

Knowledge of English or amassing numerous education certificates does not spur development. Development is brought about by people who think soundly. Innovative people. Creative persons. Does repairing a vehicle, for example, call for English? If it were so, the Japanese would not have dominated the world in car and electronics manufacture. All functional items we use are products of the mind and innovativeness. A doctor is handy not by virtue of his ability to speak a foreign language but his skill to treat. Tanzanians are taking their heart patients to doctors in India who don't understand English but are experts in heart operations.

A language, in itself is never employed but rather, someone's ability and competitiveness to perform a given task. That is why the Chinese are being awarded contracts to build stadiums while our professors, with their English, are being bypassed.

The growing emphasis of a foreign language at the expense of the country’s national language is inhibiting learning in Tanzania. This mistake has been condoned for a long time in several African countries which were under colonialism. In Mali and Niger for example, by the time a learner reaches college level, he will have studied in more than three languages. This creates confusion. No wonder, Mali and Niger are plagued with poverty to an extent that to them, development is a mirage. Should Tanzania walk the same path?
 
Mimi nawashangaa sana wanaobeza lugha ya kiswahili eti Kenya wanapata kazi kwa sababu wanaongea kienglish, this is not true. Ni nchi ngapi wakenya wanapata kazi kama sio hapa tu kwa WaTz tuliolala??????? Hata wewe unayependelea kienglish, ebu jifikirie kwenye discussions zenu chuo lugha gani iliyokuwa inatawala???? Njoo ofisini, ni lugha ipi inatumika???, njoo kwenye mawasiliano ya kawaida ni lugha ipi inatumika???? Njoo hata hapa JF ni lugha ipi imepamba website yetu, soma wanaochangia wataandika kienglish lakini lazima wachanganye na Kiswahihili. Narudi, hakuna nchi iliyoendelea kwa kutumia lugha isiyo yao. Eti utahesabika umesoma kama utaongea kiinglish kizuri upuuuuuuuuzi mtupuuuuuuuuuuuu pamoja na fikra finyu. English ibaki kama lugha ya kuwasiliana kimataifa tu lakini sio kufundishia
 
maendeleo, well in a context of maisha bora kwa kila mtanzania si lugha, na wala si rocket-type- scientific innovations. Wagiriki walianza uvumbuzi wa mambo long time ago, same as to Arabs, Egyptians, Wareno. Leo wako wapi how are they ranked?

If all that we need is the so called maendeleo. Kuna mambo mengi sana tunayotakiwa kufanya kabla hata ya kuingia huko kwenye mabadiliko ya lugha ya kufundishia!!!!!!!

Anyway swali langu sijajibiwa mpaka sasa. Je matokeo ya mthani kidato cha nne somo linaloongoza kila mwaka ni kiswahili?
 
Mzee2000;

Naamini tatizo la Tanzania siyo lugha ni elimu duni na uvivu wa kujiendeleza. Kelele kuhusu lugha ni kisingizio tu. Baadaye itakuja hoja kutufundisha Hisababi na masomo ya sayansi kwa vile wanafunzi wengi hawafanyi vizuri katika masomo hayo.

Wewe angalia tu hata mambo ambayo hayahitaji lugha Kiingereza, 'performance' yetu iko chini.

Hata tukitumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia bado kuna matatizo mengi tu ya kimfumo na moyo wa utekelezaji wake.
 
Mzee2000;

Poland now is encouraging students to study more languages so that they can fairly compete and get employment in other European countries also. Formely, the majority learnt Polish. They study, for instance, Russian, English, French, Germany etc and are able to get employemnt in those countries. 'Should Tanzania also walk the same path?'

A few months ago, I read in a newspaper that ICTR needed a lawyer who speaks and uses well English and French. That made me start studying French! Let's not be parochial, we'll remain backward if we don't open up... We must study and speak good Kiswahili but only that will not make us develop. We need to communicate with other people who do not use Kiswahili.
 
Mzee2000;

Huyu "mwalimu" unayemquote mbona anarukia conclusions bila kuweka ground work yoyote? Relationship ya kusoma kwa Kiingereza na hiyo poverty iko wapi?

Kukaa ofisini kwa Engineer kunasababishwa na kusoma kwa Kiingereza kweli? Tuwe critical na hizi opinion jamani.

Tatizo lipo kwenye mfumo wa elimu kama nilivyosema mwanzo, haijengi creativity na out of the box thinking. Na culture ya kutothamini manual labour, ukikaa ofisini ndo unaonekana wa maana, ukipiga gazi "mbeba box".

Kaamua kulaumu poverty ya Naigeria kwa sababu ya lugha! Rushwa hajaiona? Ufisadi wa viongozi wao hajauona? Matatizo ya udini hajayaona? Vita wanavyopigana na waasi kwenye Delta hajaviona? Lugha is the least of their problems.
 
Mzee2000;

mwaka huu wanafunzi wa darasa la saba wamefeli hesabu kwa 79% ambao walifundishwa kwa kiswahili na hawa ndiyo watakaosoma physics baadaye unategemea nini? kwa hiyo tatizo ya elimu ya Tanzania siyo lugha unatumika but the way it is taught.
 
Hii nchi nyinyi hamuijui?

kila mara watu wanapojifanya wazalendo ujue kuna maslahi binafsi nyuma yake, watu walipigania Richmond na hata Raisi kuingia mkenge wa kui-suport kumbe wana maslahi yao, hao wanafuzi wa uzamili nahisi wanaona kuna fursa ya wao kupewa "dili" la kutafsiri mitaala, vitabu naa kila aina ya viandiko iwapo kiswahili kitapitishwa kama lugha ya kufundishia,

ni maslahi binafsi yanayopiganiwa hapo na si kingine. Naungana na wachangiaji wengine wote wanaosema kuwa kwa sasa tumechelewa kutumia kiswahili kama medium of instruction na kwa kufanya hivyo ni kutengeneza loophole nyingine ya ufisadi, hela zitaliwa hapo na umaskini wetu utabaki palepale.

Cha msingi ni kuhakikisha tunaimarisha mfumo uliopo, hao watu wanaong'ang'ania kiswahili wengine watoto zao ama wameshasoma kwa kingereza au wanasomesha nje kwa hiyo wanapigia debe kiswahili watoto zetu watakao soma pale vumbini wasiweze kushindana kimataifa.

I SAY NO TO THE USE OF KISWAHILI AS A MEDIUM OF INSTRUCTION!
 
Hao wanafunzi wanachotakiwa kufanya ni kufanya kazi kuikuza kiswahili kimataifa na si kufikiria theories zilizoshindwa kama hizo.
Tanzania hatuitaji kutafiti kutengeneza baiskeli ya mbao bali kutumia teknologia iliopo duniani kutengeneza ndege. Hii ndiyo maana ya kukimbia wakati wenzetu walioendelea wanatembea, na hatuwezi kukimbia kwa kutumia kiswahili!

Kama tuko makini na maendeleo ya Tanzania hatuwezi kupoteza muda kufanya tafiti za kiteknologia katika mazingira yetu, bali kutafiti namna ya kutumia teknologia zilizoko tayari duniani ili tuzihamishie kwenye mazingira yetu tuendelee, na tujue teknologia uhama na lugha yake ya asili, hivyo hatuna namna ya kukwepa lugha ya kingereza.
 
Hao wanafunzi wanachotakiwa kufanya ni kufanya kazi kuikuza kiswahili kimataifa na si kufikiria theories zilizoshindwa kama hizo.
Tanzania hatuitaji kutafiti kutengeneza baiskeli ya mbao bali kutumia teknologia iliopo duniani kutengeneza ndege. Hii ndiyo maana ya kukimbia wakati wenzetu walioendelea wanatembea, na hatuwezi kukimbia kwa kutumia kiswahili!
Kama tuko makini na maendeleo ya Tanzania hatuwezi kupoteza muda kufanya tafiti za kiteknologia katika mazingira yetu, bali kutafiti namna ya kutumia teknologia zilizoko tayari duniani ili tuzihamishie kwenye mazingira yetu tuendelee, na tujue teknologia uhama na lugha yake ya asili, hivyo hatuna namna ya kukwepa lugha ya kingereza.

Huwezi kuzihamisha hizo tekonolojia bila lugha ya mawasiliano - nenda kwa fundi gari umuulize kama anajua tofauti ya 'shokomzoba' na 'shock absorber' utaelewa namaanisha nini. Amefundishwa kwa Kiswahili kuhusu kutengeneza 'shokomzoba' na anaweza. Ila hajui kuwa hiyo ni 'shock absorber' japo anajua kazi yake ni nini kwa Kiswahili. Sijui kwa nini hamtaki kuamini kuwa wenzetu wanaendelea kwa kuwa wana uwezo wa kuhusianisha kile wanachojifunza na mazingira yao ndio maana wanaweza kuvumbua na kutengeneza kwa kutumia lugha zao wenyewe!

PS: Nobody is saying we should throw away English, we are simply saying let us use it strategically alongside Kiswahili and not pathetically as it is now!
 
Cha msingi ni kuhakikisha tunaimarisha mfumo uliopo, hao watu wanaong'ang'ania kiswahili wengine watoto zao ama wameshasoma kwa kingereza au wanasomesha nje kwa hiyo wanapigia debe kiswahili watoto zetu watakao soma pale vumbini wasiweze kushindana kimataifa. I SAY NO TO THE USE OF KISWAHILI AS A MEDIUM OF INSTRUCTION!

Hivi ndivyo wanavyoshindana kimataifa hapo vumbini:

T: What do you stand when we say animals of the forest?
T: What the meaning of decided?
P: Decided means to ask others
T: Who can use in a good sentence a word decided?
P: Our teacher decided all children come in the morning to school?
T: Good. What the meaning of a well?
P: A place which water are not walking.
T: The word clapped (pronounced /krapt/). It is the past tense of which word?
T: Understood class?
T: Quiet please (pronounced /kwait pliis/).
P: Clapped is the past tense of clap (pronounced /krap/)
(Source: Mlama and Matteru 1978:19) (Quoted in Qorro - HakiElimu WP)

----------------

T: When you go home put some water in a jar, leave it direct on sun rays and observe the decrease of the amount of water. Have you understood?
SS: (silence)
T: Nasema, chukua chombo, uweke maji na kiache kwenye jua, maji yatakuwaje? (I say take a container with water and leave it in the sun, what will happen to the water?)
SS: Yatapungua (it will decrease)
T: Kwa nini? (Why)
SS: Yatafyonzwa na mionzi ya jua (it will be evaporated by the sun's rays)
(Rubagumya, Jones and Mwansoko 1998:17) (Quoted in Qorro - HakiElimu WP)
-------------------------------

Jamani acheni masihara, hatuwezi kufundisha kwa Kiingereza!
 
Back
Top Bottom