Malcom the X
New Member
- Nov 11, 2016
- 3
- 8
Mpaka lini wanafunzi wa chuo tunaosoma nchini Algeria kwa udhamini wa serikali ya Tanzania tutaendelea kuteseka kwa kucheleweshewa fedha za mkopo ?
Tabia hii imekubuhu na inatunyong'onyeza sana na kuififisha imani yetu juu ya serikali ya nchi yetu na kutufanya tujiulize kama kweli serikali yetu inajali watu wake kwa kadri inavyopaswa au imekuwa ikisema inafanya hivyo kisiasa tu????
Sasa ni takribani miezi 3 imepita tangu muda rasmi wa kupewa mkopo na hakuna taarifa zozote za matumaini kutoka wizarani pia bodi ya mkopo ambao wanaonekana hawana mamlaka juu ya hili kwani kila wanapowasiliana na viongozi wetu wanawaambia wanasubiri waagizwe na uongozi wa juu.
Sasa tunapenda kuwataarifu wale wote wanaohusika kuwa tumechoka kuvumilia kwani hali ya kifedha ni mbaya sana, kuna watu wanaumwa lakini hawawezi kwenda kupata matibabu kwa sababu gharama ni kubwa, kuna wanafunzi shule karibu itawashinda kwa sababu hawana pesa za kufanya research( gharama za internet ni kubwa na pesa hakuna ) , vifaa vya shule hakuna pesa ya kununulia, hatuna pesa za kununulia mavazi ya kujikinga baridi , ulaji wetu ni wa tabu sana ( afya zetu zimedhoofika ) .
Kwa kifupi ni kwamba wanafunzi tulioletwa na serikali ya Tanzania nchini Algeria hatupo katika mazingira stahiki ya kimasomo kwa sababu ya kukosa pesa ambazo serikali kipitia bodi ya mikopo inapaswa kututumia.
Hivyo tunaomba serikali itume pesa upesi ili kunusuru janga hili kwa sababu tunaamini inaweza ama sivyo itume tiketi za ndege wanafunzi wote turudishwe nyumbani ili tusiendelee kuteseka bila sababu za msingi.
Wanafunzi walioalgeria wamejitolea kuja kusoma kwa ajili ya maendeleo ya taifa la Tanzania, hivyo wakiwa kama raia wema na wazalendo tunaomba haki zetu zizingatiwe na utu wetu usidhihakiwe .
Sisi pamoja na wengine wote walipolekwa nchi mbalimbali ni mashujaa wa taifa la Tanzania hivyo serikali itutendee inavyowapasa mashujaa na sio kama waomba misaada.
N.B
Tumeyasema haya si kwa hasira bali kwa kadri tulivyoguswa na hali yetu