Wanafunzi Muhimbili Waandamana hadi Wizara ya Afya

Goodrich

JF-Expert Member
Jan 29, 2012
2,091
1,177
Huku mgomo wa madaktari ukiwa umeshika kasi, Wanafunzi zaidi ya 1000 wa Muhimbili wameandamana hadi wizara ya Afya kudai fedha za Chakula.
Hii inanikumbusha hadithi ya Farao na wana wa Israeli
 
Sijuti kuzaliwa tanzania najuta kuishi katika serikali na mfumo wake wa uongozi mbovu. Leo ni siku ya tatu tangia wanafunzi diploma katika chuo kikuu muhimbili hakuna chakula leo wameamuwa kwenda wizarani kushinikiza.KWA UPANDE WA UNDERGRADUATE hawajaandama wala kugoma wametulia lakini nao hawajapata hela ya chakula na malazi tangia wafungue chuo
 
Tz imepoteza dira. Kila kukicha na vibweka. Wakubali yaishe kabla janga kulikumba taifa.
 
kwani pesa inaendaga wapi? hazina imekauka? kodi zote zinaishia kwenye mikono ya mafisadi sio?
 
tatizo ninaloliona kwa serikali ya kikwete ni kuwa imepanua mahitaji ya hela kuliko inavyoingiza. wanafunzi waliopo mashuleni/vyuoni ni zaidi ya mara 1000 ya waliokuwa kabla yake. mashule yaliyojengwa katika kipindi chake ni zaidi ya 1000%, bado mazahanati/vituo vya afya na kadhalika. hivi vitu vyote atavi-RUN vipi kwa ungezeko la 50% ya kipato cha awali kabla hajawa madarakani? Si kwamba na ponda kuwa haya anayofanya ni mabaya. NO. ila uwezo wa kuyahudumia yote kwa pamoja.
Mathalani, kikwete amejenga/anajenga barabara za km zaidi ya 6000 za lami. hizi ni zaidi ya barabara zote zilizojengwa kwa pamoja na nyerere, mwinyi na mkapa. how came all of these being done within this short time? Crazy.
 
Back
Top Bottom