Wanafunzi kutokariri kidato cha pili kwawagawa wabunge

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Wanafunzi kutokariri kidato cha pili kwawagawa wabunge
Mgaya Kingoba, Dodoma
Daily News; Wednesday,July 16, 2008 @00:03

Suala la wanafunzi wa darasa la nne na kidato cha pili kukariri au kutokariri madarasa limewagawa wabunge, baadhi wakitaka wakariri. Wakichangia mjadala wa hotuba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe juzi, pia wamekerwa na hatua ya Wizara kulimbikiza madeni, wakitaka ikomeshwe na kwamba maslahi ya walimu yanapaswa kuangaliwa kwa jicho la huruma.

Kuhusu kukariri madarasa, Mbunge wa Viti Maalumu, Benadetta Mushashu (CCM), alisema wafadhili wanaipeleka kubaya elimu, akitaka wanafunzi wanaoshindwa darasa la nne na kidato cha pili, wakariri madarasa badala ya kuendelea.

"Wasioshinda wasiendelee kukariri… hawa wafadhili watatupeleka pabaya," alisema Mushashu na kuongeza kuwa wizara hiyo inaongoza kwa kudai kuwa wanasubiri wakati wa kampeni ndipo walimu wanalipwa malimbikizo yao ya madeni.

Mbunge wa Viti Maalumu, Felister Bura (CCM), aliunga mkono wazo la wanafunzi wa darasa la nne na kidato cha pili kukariri madarasa badala ya kuwaswaga kama ng'ombe. Lakini Mbunge wa Ngara, Profesa Feetham Banyikwa (CCM), alipinga wazo la kuwapo kwa mitihani ya darasa la nne na kidato cha pili, akisema ilianzishwa na wakoloni kwa nia kuwazuia baadhi ya wanafunzi hasa Waafrika kusonga mbele katika madarasa mengine.

"Hili lililetwa na wakoloni kwa nia ya kuwazuia wanafunzi Waafrika wasiendelee na madarasa ya ngazi nyingine. Sisi tumeiga tu. Hivi hatuwezi kuondokana na ukoloni? Hali hii itaongeza mdondoko wa wanafunzi ambao sasa ni asilimia," alisema Banyikwa.

Waziri wa zamani wa Elimu, Jackson Makwetta ameonya kuwa hatua ya kutaka baadhi ya masuala ya elimu kusimamiwa na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), ni kuzua matatizo mapya na kuingiza siasa katika masuala ya msingi.

Makwetta, ambaye ni Mbunge wa Njombe Kaskazini (CCM), alisema amesikia kuwa Tamisemi inataka kupewa usimamizi wa baadhi ya masuala ya elimu ni kuzua matatizo mapya, na kwamba ni vyema kucheza na mambo mengine, lakini si elimu.

Mbunge wa Wete, Mwadini Abbas Jecha (CUF), mbali ya kuwatetea walimu, aliitaka Hazina ibebe madeni ya walimu; akawajia juu wanafunzi wanaowashambulia walimu; lakini akawageuzia kibao walimu wanaowapa mimba wanafunzi wao akisema ni uhasidi. Bunge jana lilitarajiwa kupitisha makadirio ya Wizara ya Elimu na Mafunzo baada ya michango mingine ya wabunge asubuhi. Leo ni zamu ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwasilisha makadirio yake.
 
Hii Ndio Tanzania Inapanga Sera Kutokana Na Uwiano Wa Wanafunzi Wanaofeli Na Kukimbia Mitihani Hiyo Sababu Za Mimba,ufugaji,na Uvuvi.........hizo Ndio Sababu Kubwa Zilizopelekea Jk Apange Mkakakati Mkali Hivyo Wa Kufuta Mitihani Hiyoo...si Vinginenvyo Subirini Akitoka Madarakani....mtaona Watamnyoshea Vidole.........na Kumuita Majina Yoteee.......hili Ni Suala Zito Ila Ndiko Lilikotoka.......kwa Museee Ya Nchiiiiiiii.naomba Kuwakilisha.
 


“Hili lililetwa na wakoloni kwa nia ya kuwazuia wanafunzi Waafrika wasiendelee na madarasa ya ngazi nyingine. Sisi tumeiga tu. Hivi hatuwezi kuondokana na ukoloni? Hali hii itaongeza mdondoko wa wanafunzi ambao sasa ni asilimia,” alisema Banyikwa.

Hivi huyu muheshimiwa naye ni Prefesa wa nini?.....Yaani kukariri madarasa ni kuwaiga wakoloni?
Naachia hapa....... maana yatakayofuata pengine nikafungiwa kuchangia hoja humu jamvini; na sitaki kupoteza nafasi hiyo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom