Wanafunzi kadhaa wa mwaka wa tano udaktari (medicine) Muhimbili University wamekuwa discontinued

bado wanaishi tu maana mi naona kama ni ngumu yaani kwa walichokuwa wanasomea hiyo bila cheti ni useless
ila inauma
 
Ndugu uliyepost habari hii umekosea sana. kwanza ujafatilia habari kwa kina yaani haujui kinachoendelea yaani umekulupuka. pili umewachafulia majina watu kwa kwa kueneza habari kuwa wamedisco wakati haujafatilia habari kwa kina. tatu inakichafua chuo kwa kukulupuka

Msaidie kwa kueleza nini kilichotukia kwa usawia. Vinginevyo sisi tutamwamini. Uongo haushindwi kwa kuuficha ukweli bali kwa kuuweka wazi.

Alizona tususaidie kwa kutujuza ukweli.
 
Hii freedom sasa imezidi:
1.Huwezi ku-post majina kiholela namna hiyo
2.Hujui chanzo ni nini hadi kupewa barua za kuwa discontinued ni nini
3.Ume post thread yako kishabiki na kwa kuficha ukweli(Either kwa kujua ili kupata public sympathy au kwa kutokujua na hivyo kukurupuka)
4.Hujui idadi halisi ni ipi(Umesema wako 10) lakini umeweka majina ya watu tisa(ambayo hayakutakiwa kuwepo)...Kwani kutaja majina hakuongezi chochote katika thread yako..kama wewe ndiye wa kumi kwanini hujitaji??

Ukweli ni kwamba Hawaku-submit Elective report ambayo hupaswa kufanywa ktk likizo ya mwaka wa nne, na deadline huwa kabla ya kumaliza masomo yaani mwaka wa tano, hivyo mwanafunzi huwa na mwaka mzima wa kukusanya data, kuandika report...
-Je, walifanya?..walimaliza?..kama kulikuwa na shida kati ya Supervisors wao, walitoa taarifa? Taarifa ilitoka ktk muda sahihi?

-Kati ya darasa lenye wanafunzi zaidi ya 150 ni wanafunzi 10 tu ndiyo ambao hawaku-submit elective report zao, au unataka kusema kuna kosa/makosa common to all ten candidates??

-Ustaarabu na heshima haihitaji kwenda shule..jifunze namna ya kusitiri taarifa fulani(personally SIDHANI KAMA NI STAHA kabisa ulivyo andika majina yao hapo-watu wana heshima zao, familia, na mahusiano mengine) na kama unadhani ni sahihi kuweka majina hapo kwanini jina la kumi halionekani??..kwangu mimi ninatafsiri WEWE ndiye wa kumi(AMBAYE JINA LAKO LINAJULIKANA PIA) na ninasema hivyo kwani uandisihi wako umekaa kishabiki au emotions zaidi..if,so kwanini hukuliweka? Au, jina lako liandikwe pia hapa?

-Kwa experience yangu ndogo wakti nikiwa mwanafunzi pale, MUHAS SENATE ikishapitisha ..that's the finals say..ingekuwa kuna wepesi kama maamuzi bado yapo katika MUHAS BOARD..So,ningewashauri wanafunzi tajwa wa-appeal since it is out of Academic grounds instead it was WRONG DISCIPLINARY MEASURE by the MUHAS Administration.

-Mwisho, POLE kwa wanafunzi wote mliofikwa na huo mkasa.

Naungana mkono na wewe katika hili la kutaja majina...na siamini kama MUHAS wameweka majina coz always walikua wanaweka namba na sio majina...labda sikuhizi imebadilika..
Kwaupande mwingine kwakutumia common sense tu...huwezi kumsomesha mtu kwa gharama kubwa ya miaka mitano then simply unampotezea...especially tatizo likiwa si kufeli mitihani ambayo inachukua uzito mkubwa katika fani hii.Najua wanamakosa but bado kulikua na njia nyingi mbadala za kuwa bana wanafunzi hawa na kuokoa rasilimali za taifa.
He kumbe Karim mbulushi ndo kawa Dean,MUHAS kuna janga sasa hivi wakuu
 
Tunapokuwa wanafunzi mara nyingi tunajisahau sana kutimiza wajibu na kukimbilia kulaumu mfumo. Kama prospectus ipo kwa nini hao wanafunzi wamengoja mpaka ifikie huko? Ni lazima kukubali kuwa wanamatatizo hata kama wana uwezo katika masomo.
 
Second chance wapewe wote siyoo madaktari. Hivi kule chumba cha operesheni wanaweza kutoa second chance kwa aliyekufa? Acheni utani bwana. hao warudi nyumbani wakakazane na kilimo kwanza.

Nadhan hujui jinsi madaktari wanavyotayarishwa, elective much more of academics and less of practical ya kufanya operation. Na ili uruhusiwe kupractice unapaswa kufanya internship na kusajiliwa na baraza la madaktari. Ila naungana na wachangiaji wengine kuwa kuna aina fulani ya uzembe ya wadogo zetu vyuoni. Wanaanza kupoteza culture ya udaktari
 
Back
Top Bottom