Wanafunzi elfu tano waliofaulu hawajui kusoma na kuandika

Masabaja

Senior Member
Mar 4, 2012
139
23
Nimesoma katika gazeti la mwananchi la leo nimestushwa na taarifa kwamba wanafunzi elfu 5200 waliofaulu kuingia kidato cha kwanza hawajui kusoma wala kuandika. Ndugu wana JF tukiwa katika karne ya sayansi na technologia halafu una watoto wanahitimu elimu ya msingi kisha hawajui kusoma wala kuandika. Tunaenda wapi?

Naomba kuwasilisha

Source: Gazeti la Mwananchi la tarehe 10/04/2012
 
Nimesoma katika gazeti la mwananchi la leo nimestushwa na taarifa kwamba wanafunzi elfu 5200 waliofaulu kuingia kidato cha tanao hawajui kusoma wala kuandika. Ndugu wana JF tukiwa katika karne ya sayansi na technologia halafu una watoto wanahitimu elimu ya msingi kisha hawajui kusoma wala kuandika. Tunaenda wapi?

Naomba kuwasilisha

Source: Gazeti la Mwananchi la tarehe 10/04/2012

Huu ndio msiba wa kitaifa kama Watanzania tukiamua kuwa serious! m.k.w.e.r.e na wenzake wa-take note!
 
Kwa mtindo huo utegemee Dr Ndalichako atatangaza matokeo ya aina gani kwa mwaka 2015?
 
Kwani haya hatukuyajua?!!!! Matatizo tuliyatengeneza wenyewe, tumeyalea, na sasa tunavuna tulichopanda, cha ajabu nini?
 
wizara ya elimu yote leo wamekwenda kumzika MZINIFU kanumba unategemea nini?halafu watanzania hawataki kuambiwa ukweli.
 
Nimesoma katika gazeti la mwananchi la leo nimestushwa na taarifa kwamba wanafunzi elfu 5200 waliofaulu kuingia kidato cha kwanza hawajui kusoma wala kuandika. Ndugu wana JF tukiwa katika karne ya sayansi na technologia halafu una watoto wanahitimu elimu ya msingi kisha hawajui kusoma wala kuandika. Tunaenda wapi?

Naomba kuwasilisha

Source: Gazeti la Mwananchi la tarehe 10/04/2012

Jamani hii bado haingii akilin kwangu....huyu mtu hajui kusoma wala kuandika kajibu vp mtihani?
 
Wakuu inakuwaje mnashangaa wakati vihiyo wapo hadi kwenye baraza la mawaziri? wengi tumesikia kuwa tuna mawaziri ambao Phd zao ni bandia, na hata uwezo wao unoanesha kuwa ni wa form six leaver. Labda hao wanafunzi wamepata honorary kufaulu, who knows.
 
Lakini hao walifaulu vipi mtihani wa taifa?

Nani alisahihisha hiyo mitihani yao?
 
Hili nalo ni janga la kitaifa hili. Tatizo hii nchi there is no body who is serious. Hivi kwa mfano huyu mwanafunzi amefika sekondary, mnakuta hajui kusoma na kuandika, mnashindwaje kwenda kumkamata mwalimu mkuu wa shule husika aseme ilikuwaje huyo mtoto akafaulu? Yaani hili lingefanyika mwaka mmoja tu, tungesahau huu uhuni. Lakini viongozi wetu hovyoo, hawajui wajibu wao ni nini hawa jamaa. kula kulala tu kazi yao.
 
Hilo suala la kufaulu shule ya msingi halipo watoto wanachaguliwa.Sasa naona wamechagua maboya mengi safari hii.
 
Mtu unafaulu vipi mtihani kama hujui kusoma na kuandika?

Au msahihishaji naye anakuwa hajui kusoma na kuandika?
 
Mtu unafaulu vipi mtihani kama hujui kusoma na kuandika?

Au msahihishaji naye anakuwa hajui kusoma na kuandika?

Msahihishaji ana malimbikizi ya mshahara miezi mitano hata uwezo wake wa kusoma na kuandika(kuweka tick au cross) unaweza kuwa impaired na mawazo.
 
Utashindwaje kufaulu mtihani ambao hauhitaji kufikiri. Maswali yote ni ya kuchagua. Muhimu ni mwanafunzi kuweza kujua kuandika harufi A,B,C,D na E.
 
Sasa kama hawajui kusoma na kuandika walifaulu vipi?

Mkuu NN,

Nakumbuka haya ni matokeo ya utafiti ulioamuliwa kufanywa baada ya kubainika kuwa wanafunzi elfu 9 na ushehe walijihusisha na udanganyifu na hivyo kukawa na wasiwasi kuwa huenda kuna waliopenya hivyo wakatakiwa wote waliofaulu wafanye mitihani watakapoingia kidato cha kwanza. Yawezekana kabisa hawa watoto "walifaulu" kwenye karatasi zao kwakuwa sio wao waliofanya hiyo mitihani au walipewa majibu.... Sijui kama jamii tunaelekea wapi....
 
Twende taratibu mmoja mmoja tutumie watu makini kwa uwazi. Tuwahoji vizuri wanafunzi wenyewe, walimu, wazazi na wasahihishaji tutapata sababu kabla ya ku-generalize.
 
Back
Top Bottom