Wanafunzi 400 wajisaidia porini

Jun 13, 2010
22
1
Wanafunzi 400 wajisaidia porini


na Ambrose Wantaigwa, Tarime

Tanzania Daima, 17 January 2011, pg 6.
amka2.gif

SHULE ya msingi Nyairoma iliyoko katika kata ya Sirari wilayani Tarime yenye wanafunzi zaidi ya 400 inakabiliwa na upungufu wa vyoo na kusababisha wanafunzi kujisaidia porini.
Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki shuleni hapo, mwenyekiti wa kijiji cha Sirari, Nyangoko Paulo, alisema atalazimika kuitisha kikao cha dharura cha serikali ya kijiji, ili kuwanusuru watoto hao kukumbwa na magonjwa ya mlipuko.
“Wanafunzi wanalazimika kujisaidia vichakani ama katika vyoo vya shule jirani ya Sirari mita chache kutoka shuleni hapo hali inayowaweka katika hatari ya kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu,” alisema.
Alisema uamuzi wa kuitisha kikao cha dharura cha serikali ya kijiji umechukuliwa baada ya kamati ya shule hiyo kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo kutokana na ufinyu wa bajeti. Mmoja wa wazazi, Marwa Masese alitishia kuhamisha watoto wake wawili ikiwa shule hiyo haitachukua hatua za haraka kukabiliana na mazingira mabaya ya kiafya yaliyoko shuleni hapo ikiwa pamoja na kuchimbwa vyoo.
 
Back
Top Bottom