Wanafunzi 4,000 wakosa mikopo elimu ya juu

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Wednesday, 19 September 2012 19:13


heslb-logo.jpg
Elizabeth Edward

WANAFUNZI 3,937 waliodahiliwa kuanza masomo ya elimu ya juu mwaka 2012/13 katika vyuo mbalimbali nchini, wamekosa mikopo kutokana na ufinyu wa bajeti.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Asangye Bangu alizungumza Dar es Salaam jana kuwa wanafunzi waliokidhi vigezo vya kupata mikopo hiyo ni 33,050 lakini waliopata ni 29,113.
Alisema kati ya wanafunzi hao waliofanikiwa kupata mikopo, wasichana ni asilimia 31.9 na wavulana asilimia 68.0.

“Jumla ya wanafunzi 49,895 walituma maombi Bodi mwaka huu. Waliokidhi vigezo na kustahili kupata mikopo ni 33,050. Wapo ambao hawatapata licha ya kukidhi viwango kutokana na ufinyu wa bajeti na masomo yao kutokuwa na kipaumbele,” alisema Bangu.

Alisema wanafunzi 28,454 tayari wameshapangiwa viwango vya mikopo na wengine 659 bado kupangiwa kutokana na kushindwa kukamilisha baadhi ya vitu ambavyo vinapaswa kuambatanishwa na fomu.

Bangu alisema vipaumbele vimewekwa kwa wanafunzi wenye uhitaji wa mikopo hiyo kutokana na uwezo sambamba na wanaochukua kozi za ualimu, uhandisi, sayansi ya kilimo, sayansi ya wanyama, sayansi ya tiba na hisabati.
“Tumezingatia zaidi uhitaji wa mwombaji na masomo yenye vipaumbele kwanza kabla ya masomo mengine. Vilevile wapo watakaokosa kutokana na ufinyu wa bajeti,” alisema Bangu na kuongeza:

Waliofanikiwa kupata mikopo kwa masomo ya ualimu ni 13,004. Fani nyingine na idadi ya wanafunzi waliopata mikopo kwenye mabano ni uhandisi (2,369), elimu - sayansi (2,146), sayansi ya kilimo (433), sayansi ya wanyama (91), elimu - hisabati (242), sayansi ya tiba (1,583) na wanafunzi 6,838 kwa kozi zisizo za kipaumbele.

Alisema takwimu za mwaka huu zinaonyesha kuwa idadi ya wanafunzi waliopata mikopo imeongezeka kwa asilimia 12 ikilinganishwa na mwaka jana ambao waliopata walikuwa 26,000... “Serikali imetenga Sh345 bilioni ikilinganishwa na mwaka jana ambapo zilikuwa Sh317 bilioni,” alisema.

Aliwataka wanafunzi 659 ambao fomu zao zina matatizo kufanya marekebisho ndani ya siku 14 kuanzia jana ili bodi iendelee na mchakato wa kuwapitishia mikopo... “Wale ambao watakuwa wana matatizo, majina yao yatakuwa kwenye tovuti ya bodi ni vyema wangekamilisha mapema ili kuondokana na usumbufu.”
 

Sasa hao Waliokosa Pamoja na FANI yao KUWA sio ya MAANA kwahiyo hawata weza kuendelea na MASOMO labda wajilipie

WENYEWE? au Watakaa na kusubiri labda BUDGET ya Mwaka Unaofuata ? sababu kama ni Watoto wa Wakulima ina Maana ELIMU

BASI Kwao? Na wengine wenye UWEZO Wamepata MIKOPO ?
 
Shimbo kasitaafu jana na trilion tatu zake kwa amani! Mwizi na fisadi huheshimiwa sana na serekali ya ccm. MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA CCM HOYEEE!
 
Shimbo kasitaafu jana na trilion tatu zake kwa amani! Mwizi na fisadi huheshimiwa sana na serekali ya ccm. MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA CCM HOYEEE!

chandarua oyeee,madawa ya kulevya china oyeeeeee
 
Back
Top Bottom