Wanafunzi 15 UDSM wafutiwa kesi

mwinukai

JF-Expert Member
May 3, 2011
1,447
630
Na Asha Bani

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dar es Salaam, imewaachia huru wanafunzi 51 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya kufanya mkusanyiko na maandamano kinyume cha sheria.

Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Waliarwande Lema, alisema ameamua kuifuta kesi hiyo kutokana na kupitia mwenendo mzima na kujiridhisha kutokana na upande wa mashtaka kushindwa kupeleka hata shahidi mmoja hadi leo.

Alisema awali mashahidi walitakiwa kufika mahakamani hapo Septemba 8 mwaka huu, lakini upande wa mashtaka unaoongozwa na wakili wa serikali Ladslaus Komanya, ulidai kuwa askari waliotakiwa kutoa ushaidi huo walikuwa na kazi ya kusimamia mgomo wa madaktari.

Baada ya kutoa sababu hizo, hakimu alitoa tarehe ya ahirisho la mwisho ambalo ni jana na mashahidi walishindwa kufika tena na wakili wa serikali kuieleza mahakama kuwa wako katika kusimamia sensa.

Kutokana na sababu hiyo, Lema alisema upande wa mashtaka umeidharau mahakama kutokana na kuwepo na taratibu za kuomba ruhusa ingawa sensa ina umuhimu wake na kesi hiyo ina umuhimu wake pia.

Alisema kwa mujibu wa kifungu cha 225 (4) kifungu cha makosa ya jinai kulikuwa na utaratibu wake ambao wakili wa upande wa serikali alitakiwa kufanya kuliko hivyo alivyofanya.

Kutokana na hali hiyo Hakimu Lema alisema hana sababu ya kuendelea tena na kesi, hivyo ni bora kuwaachia huru kwa maana shauri zima halitakuwa na sababu ya kuendelea nalo.

"Kwa mujibu wa kifungu cha 225(5) sura ya 20 nawaachia huru washtakiwa wote kwa kuwa kesi hii haina haja tena ya kuendelea nayo," alisema Lema.

Awali walipokuwa wanasomewa maelezo ya awali watuhumiwa hao walidaiwa kuwa pamoja na kupewa ishara ya kusitisha maandamano na askari polisi walikiuka na kuwashambulia kwa mawe.

Komanya alidai kuwa Novemba 11, 2011 wanafunzi hao walifanya mkusanyiko katika Uwanja wa Revolution lililopo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadaye waliandamana kuelekea eneo la Ubungo Maji huku wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe unaoilaumu Serikali na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kuwa haiwatendei haki.

Novemba 14 mwaka jana, wanafunzi hao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza wakidaiwa kufanya mkusanyiko usio wa halali na kusababisha uvunjifu wa amani katika eneo la UDSM.

Nje ya mahakama, nderemo na vifijo vilitawala ambapo wanafunzi hao walikuwa na furaha huku wakishangilia na kuelekea katika Barabara kuu ya Bibi Titi Mohamed kutokana na kuachiwa huko.


SERIKALI INAPOFANYA HUJUMA HATA KWA WANAFUNZI KWA KUWABAMBIKIA KESI NA KUSHINDWA KUSIMAMIA JE HII INAMAANISHA NINI?
 
Chuo kiliwafukuza kutokana na madhila hayo, ni nani anawajibika kuwalipa fidia yao?
 
Hapa sijui sasa baada ya kuwafutia kesi mahaka ilipaswa iseme watarudi chuoni au? na fidia ya kupoteza muda ni nani atalipa? Je Hawa walioidharau mahakama je sheria gani inapaswa kuchukuliwa? Kweli serikali inaidharau mahakama. Hivi ndivyo wanyonge wanavyoonewa.
 
Hapa sijui sasa baada ya kuwafutia kesi mahaka ilipaswa iseme watarudi chuoni au? na fidia ya kupoteza muda ni nani atalipa? Je Hawa walioidharau mahakama je sheria gani inapaswa kuchukuliwa? Kweli serikali inaidharau mahakama. Hivi ndivyo wanyonge wanavyoonewa.
wanatakiwa kufungua kesi ya madai ili kurudushiwa stahili zao zote
 
Siyo wanafunzi 15 bali 51. Hawakuwa na kesi zaidi yakuzungushwa na kutaka kunyamazishwa tu na uhuni wa serikali yetu ya kipuuzi. Wakamateni mafisadi badala ya wanafunzi.
 
Moja ya changamoto inayokabiliana nazo serikali kwenye kesi km hiz ni kukosa ushahid,hivyo mara nyingi watuhumiwa uishiwa kuachiwa. ndio maana mimi siogopi kuandamana wala kufanya mkusanyiko usio halali.
 
Sheria za Vyuo ya Mwaka 2007 ni kwamba ukiwa na kesi mahakamani unapaswa kusimamishwa masomo mpaka hapo kesi itakapoisha ukikutwa na makosa basi unafukuzwa chuo.

Kwa wa UDSM wengine walikua tayari wanaendelea na masomo, wengine watarudi chuoni mwezi wa kumi na wengine walifukuzwa kabisa.
 
Sheria za Vyuo ya Mwaka 2007 ni kwamba ukiwa na kesi mahakamani unapaswa kusimamishwa masomo mpaka hapo kesi itakapoisha ukikutwa na makosa basi unafukuzwa chuo.

Kwa wa UDSM wengine walikua tayari wanaendelea na masomo, wengine watarudi chuoni mwezi wa kumi na wengine walifukuzwa kabisa.

Chalii unaimply nini?
 
Back
Top Bottom