Wanachuo na DEC ni ujasiliamali au Ufisadi?

kasyabone tall

JF-Expert Member
Sep 13, 2009
254
59
Wanachuo na DEC ni ujasiliamali au Ufisadi?
Jamani kwa muda nimefanya research kujua ni wanachuo weangapi waliwekaza fedha za mikopo DEC. Nimegundua kuwa wanafunzi wengi walitumia pesa iliyotolewa kutoka kwenye kodi ya wananchi kwa ajili ya kuwasomeshea ikiwamo pamoja na kununua viandikwa na viandikio lakini wanachuo hawa walitumia pesa hio kuwekeza DEC, hatimaye zikapotea mpaka leo. Sasa maswali ambayo nilikuwa najiuliza ni mengi sana, achana na watu waliowekaza hela zao za mfukoni.
Je watu hawa ni wajasiliamali au mafisadi?
Kwa kutumia fedha za serikali kuwekeza hawajatumia ipasavyo inaonyesha ni uchu wa pesa wa hali ya juu, je mtu huyu akiajiliwa na kukawa na pesa ya ofisi isiyo na matumizi ya haraka je ataweza kuitunza au atawekeza? Baadaye ikiliwa kama ilivyo kwenye DEC je huyu mtu akashindwa kuirudisha huoni kuwa watakuwa wakinamramba?
Je mtu huyu anapaswa kuwa kiongozi katika taifa hili ambalo watu wengi hawajui pesa yao iko wapi na inafanya nini kwa wakati gani?
Kama ni ufisadi kwanini wasishitakiwe?
Hapa niliachilia mbali ni watu wangapi waliwekeza pesa ya walipa kodi kwenye DEC na hatima yao ni nini? (wanaowajua tumtonye slaa wasikae kimya)
nisaidieni huu ni ujasiliamali au ufisadi?
 
Back
Top Bottom