Midavudavu
JF-Expert Member
- Jan 23, 2012
- 287
- 59
Jamani mwenzeni nimeota wanachama wa jamiiforums tumeitwa kupewa zawadi kila mmoja kutokana na mchango wake aliotoa katika jukwaa hili. Zawadi zilikuwa zinatolewa katika uwanja wa Taifa Dar. Kila mwanachama alikuja na familia yake ili ashangiliwe wakati anapewa zawadi. Msherehereshaji akawa anasoma jina moja moja pamoja na kusoma jokes zote zilizotumwa na mhusika. Jamani ilikuwa kimbembe, tumegoma wote kwenda kuchukua zawadi wengine wakaomba tupewe tukiwa peke yetu, wengine hata hilo hawakulipenda wakataka tuingiziwe ktk simu zete kwa m-pesa. Nilipata manufaa sana kupitia ndoto hii maana nilikutana na wanachama wenzangu wa JMF physically hasa Professors wa vyuo mbalimbali, wanasiasa mashuhuri na viongozi wengine maarufu wa Serikali. Yaani nyie acheni tuu jamani, sijaona jukwaa lenye watu maarufu kama hili.