Wanachama wa CCM waguswa na sera za upinzani wa CUF-200 wachoma moto kadi za CCM

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Wanachama wa CCM waguswa na sera za upinzani wa CUF,200 wachoma moto kadi za CCM
Na Kizitto Noya, Tandahimba

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Machano Khamis Ali, amegusa hisia za wakazi wa Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara na kusababisha zaidi ya watu 200 kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na CUF, baada ya kuwaeleza kuwa chama hicho tawala, kimewageuza kuku wa kienyeji.

Alisema, umaskini wa Mtanzania hautapungua na maendeleo kupatikana, endapo nchi itaendelea kuongozwa na CCM, kwa kuwa chama hicho hakiwathamini wananchi kama vile mfugaji asivyomthamini kuku wa kienyeji

"Viongozi wa CCM, wanawageuza kuku wa kienyeji ambaye hapewi chakula. Anapewa chakula na mfugaji siku ya kuchinjwa. Kwa akili yake mbovu anadhani siku hiyo anapendwa sana kumbe wanataka kumkamata na kumfanya kitowewo.

"Hii ndio CCM. Siku zote haijishughulishi na matatizo ya wanachi, lakini wakati wa uchaguzi wanakuja na ahadi nyingi nzuri kukuomba kura. Wanakuja na fedha na vishawishi vya misaada mbalimbali na baada ya kuwapigia kura hawaji tena kuwaona,” alisema Machano.

Machano alitoa kauli hiyo, kwa nyakati tofauti mwishoni mwa wiki wakati akihutubia mikutano ya hadhara wilayani Tandahimba katika sherehe za kumpongeza diwani pekee wa CUF Tanzania Bara, anayetoka katika Kata ya Manyawa, Rajab Nalinowa.

Kauli ya Machano imekuja baada ya wakazi hao kumwleza kuwa wilaya ya Tandahimba, ina matatizo mengi, ikiwamo ukosefu wa maji, matumizi mabaya ya fedha ya umma na ukosefu wa soko la uhakika la zao la korosho.

Walisema, matatizo hayo kwa namna moja ama nyingine yametokana na uzembe wa watendaji wa Serikali za vijiji, kata na halmashauri kwa kuwa wameshindwa kuweka mipango madhubuti kukabiliana nayo.

Kwa mujibu wa Machano, Wananchi wa Tandahimba, wasitegemee mabadiliko ya msingi katika maisha yao, chini ya uongozi wa CCM kwa kuwa mfumo unaotumia kuongoza, ni wa kugawana mali ya umma.

"Haya matatizo yenu hayataisha mpaka muiondoe CCM madarakani. Mhakikishe mwaka huu, mnashinda viti vyote vya uenyekiti wa vitongoji na vijiji, kata na halmashauri," alisema.

Akizungumza katika mkutano huo, diwani kata ya Manyawa (CUF) Rajab Nalinowa alisema, siri ya kuishinda CCM ni wananchi kuhifadhi vitambulisho vyao vya kupigia kura, kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuzilinda.
 
Hongera Bwan Mwiba. Lakini hivyo vitu vingekuwa vinatokea kule Kidoti au Makunduchi Zanzibar ningekupigia kofi. Huko huna la maana , unapuyanga tu.
 
Huko unakokusema hakuna jipya inajulikana wazi kuwa hakuna wafuasi wa CCM wa kuweza kuihangaisha CUF ,hilo halina mjadala unalielewa fika na unafahamu vizuri kabisa ninachokizungumza ,Zanzibar nzima ni wafuasi wa CUF ,si viongozi waliomo serikalini si wapita njia au umesahau mambo yalipozidi unga Karume akasikika kuwa kura yake na ya mkewe zitamuweka ikulu ,nyie pangu pakavu kusikia hivyo sijui mlikuwaje ,au sema kama hukusikia maana mtu mwenye akili timamu ambae ni CCM atakuwa na ari juu ya kauli.
Hivyo uelewa wako sijui unakupeleka wapi na wewe kama upo CCM basi si lolote si chochote kwa kauli aliyoitoa Karume ,kwamba wewe ukimpa kura usimpe Ikulu ataikaa ,sijui hata kama unafahamu maana ya kutoa kauli hiyo ya ubabe na ufedhuli ,hayo hakuambiwa aliekuwemo CCM bali wameambiwa CCM wanajilabu kuwa wao ndio wenye Chama wao au nyie ndie mnaemchagua nani wa kukaa Ikulu ,pole sana.
 
Yaani kuelekea 2010, mpaka vistationary vitakula sana pesa, vijitenda vya kuchapisha kadi feki za kuchoma ili kuvutia wanachama vitalipa sana. Kwa Tandahimba ninayoijua mimi, wanaCCM 200 wakuchoma kadi zao?!. Labda kama ingekuwa Pemba!.

Vyama vitachapisha sana cadi za wenzao ili kuzichoma!.
 
Back
Top Bottom