Wanachama 3 wa chadema wafungwa mika 3 jela.

Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
11,450
8,241
Wanachama 3 wa cdm wamefungwa miaka 3 jela ktk mah ya mwanzo ya kijiji cha iyula wilayani mbozi.baada ya kuzuliwa kesi na mwenyekiti wa kijiji cha ichesa wilayani mbozi kuwa walitaka kumuua.kabla ya hapo mwenyekiti alikuwa ametangaza kuwa atahakikisha vyama vya upinzani havipati nafasi ya kujiimarisha ktk eneo lake.vijana hao walikamatwa waliopokuwa wanatangaza sera za chama chao ilikujaribu kukitwaa kiti cha udiwani wa kata ya ichesa pindi uchaguzi utakapoitishwa baada ya kifo cha diwani wa ccm. hivyo mwenyekiti kuingiwa na wasiwasi kuwa huenda kata hiyo isitwaliwe tena na ccm.viongozi wa wilaya cdm wamekata rufaa na itasikilizwa 20 07 2012 baada ya kutumikia kifungo cha mwezi 1.
 
Siwezi sana kushangaa kwani mahakama nyingi hapa nchini wazee wa mahakama wengi ni makada wa CCM wa kudumu kwa hiyo kesi nyingi ambazo zitahusu vijana wa CDM lazima sheria zitapindishwa na kutoa hukumu za uonevu, tujiulize kule Iringa yule mwenyekiti aliye mtishia maisha Mh. Msigwa amekwisha hukumiwa au ndiyo imepotezewa kiaina, lakini mwisho wao hupo karibu kwani mungu hamtupi mja wake ukombozi utapatikana.
 
Hii habari uongozi makao makuu haukuwa na hii habari kabla ya hukumu?
Swali lako linamaanisha nini? kwani hata makao makuu wangekuwa wanajua wana uwezo wa kuzuia hukumu? fikiria kidogo kule Arusha taarifa zilikuwepo za hukumu itakayo tolewa niambie walibadirisha hukumu? usipende kuuliza maswali ambayo hayana msingi kama huna cha kuandika soma na pita tu.
 
Poleni sana wajenzi wane, umwene wa maha, irufaa yinyu kutimpote! Amayimba mwenzo.
 
Hii habari uongozi makao makuu haukuwa na hii habari kabla ya hukumu?

Kwani hao waliofungwa nao wanatoka kule?
Call your enemy what you are, and always tell exact opposite of the truth.
 
Udhalimu huu ni dalili ya ukombozi,hakika nauona!!!!Tusife moyo makamanda wote,ALUTA CONTUNE!!!
 
Hii habari makao makuu wanapaswa kuingilia kama mkoa wameshindwa.

Huyu mwenyekiti ni mtu mwenye uwezo mkubwa sana kifedha kwa sehemu kubwa ndie mfadhili wa kijiji hiki. ndio maana kachaguliwa kuwa mwenyekiti.kesi yenyewe imeendeshwa kiaina. nakala yenyewe ya hukumu ilikuwa ngoma nzito kuipata mpaka walipojulishwa makao makuu cdm kupitia kwa mgombea ubunge alieshindwa kupitia tiketi ya cdm ndugu mwampamba ndipo walipofanikiwa kuipata.kwa kweli makao makuu cdm wamesaidia sana.
 
Indaji tee bhantu mwii, Ungulubhi abhavwe bhana bhitu, tubhaputila tee, tuli palushimo, munganasaje!
 
Wanachama 3 wa cdm wamefungwa miaka 3 jela ktk mah ya mwanzo ya kijiji cha iyula wilayani mbozi.baada ya kuzuliwa kesi na mwenyekiti wa kijiji cha ichesa wilayani mbozi kuwa walitaka kumuua.kabla ya hapo mwenyekiti alikuwa ametangaza kuwa atahakikisha vyama vya upinzani havipati nafasi ya kujiimarisha ktk eneo lake.vijana hao walikamatwa waliopokuwa wanatangaza sera za chama chao ilikujaribu kukitwaa kiti cha udiwani wa kata ya ichesa pindi uchaguzi utakapoitishwa baada ya kifo cha diwani wa ccm. hivyo mwenyekiti kuingiwa na wasiwasi kuwa huenda kata hiyo isitwaliwe tena na ccm.viongozi wa wilaya cdm wamekata rufaa na itasikilizwa 20 07 2012 baada ya kutumikia kifungo cha mwezi 1.
Hongera mkuu fuatlia kwa makini na hakikisha haki inatendeka!!usibakie kutoa taarifa fuatilia na utoe taarifa!!
 
Ndiyo mnasema mahakama ni mhimili huru? Nafuu watanzania wengi wafahamu manyanyaso yanayofanywa na ccm kupitia vyombo vya dola vilivyo chini yake.
 
hata Mandela alikaa jela miaka 27 na mwisho akawa Rais.CCM ya leo ni makaburu weusi wa wa TZ
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom