Wanachama 1,938 wa CCM, Wenyeviti Watano wahamia CHADEMA

Nimemsikia Zitto akitoa hoja hiyo ya kukusanya sahihi 70 za wabunge, kwa ajili ya kupeleka hoja Bungeni ya kutokuwa na imani na waziri Mkuu. Kweli sasa mambo yanazidi kunoga. Madudu yanayofanyika serikalini yanasikitisha na yanatia uchungu.
 
.............Wote hao walikuwa mizigo isiyobebeka......

Tafsiri ya mizigo isiyo bebeka ni ipi?
Mi nadhani uko sahihi kabisa,hela mlizokuwa mnawapa,wamekula na bado hawaridhi,hiyo ndio mizigo isiyo bebeka
Sasa wamekuja cdm ambako wanatakiwa wachangie walichonacho hata kama ni tshs50,inauma hiyo.
 
Wanachama wa ccm wakiwemo wenyeviti wa vitongoji vitano wilayani ngorongoro, wametangaza kukihama chama hicho na kujiunga na chadema,na tayari wamebwaga kadi zao za ccm katika ofisi za chadema zilizopo wilayani humo na kukabidhiwa za chadema.

Tarifa hiyo imetolewa na katibu wa CHADEMA mkoa wa Arusha Amani Golugwa.


Hapa njia imeanza kuwa nyeupe yani Chadema inakuja speed 120 na hakuna cha nini wala nini bumps tunafukia break ni kuchukua dola na kupaki basi ikulu.
 
Nashauri wananchi wenye nia njema na Tanzania sehemu yoyote waliopo kuimalisha ulinzi, na kuhakikisha mafisadi wote ambao watakuwa kwa sasa wanapanga kuikimbia nchi wanazuiwa kwa nguvu zote. Maana upepo wa kuirudisha Tanzania katika mikono sahihi yaani watanzania wenyewe unazidi kushika kasi.

Tukiwaachia mafisadi wakakimbia,itakula kwetu, maana watatoroka na mali walizotuibia.

Hima hima watanzania !
 
Dah, hizo ni siku 7 tu, je akifunga miezi 3 itakuaje? Si mpaka Nape atarudisha kadi..
 
Dah, hizo ni siku 7 tu, je akifunga miezi 3 itakuaje? Si mpaka Nape atarudisha kadi..

Daaah! Hizo nyingi sana na itakuwa batili na kufuru. Nashauri (Lema) asiwazidi manabii na mitume. Amezidi sana (kama akitaka) isiwe zaidi ya 28, 29, au 30 kama akiamua kufunga kiislam au 40 kama akitaka kikristo. Asizidi hapo.
 
Back
Top Bottom