Wana Tabora kumlilia Rostam na siyo Selelii! Wana nini?

Kwa hiyo ukiwa wewe unapita na wengine hawana uwezo wa kupita? Unanchekesha! huna hoja.
<br />
<br />
Lakini unapopasifia utafikiri pako juu sana, unavyosifia mtu anaweza akadhani pako kama uswisi vile kumbe hakuna kitu kama hicho, we jamaa watu wengi Tz walikuwa hawamkubali na hata baadhi ya magamba wengine kama nape walikuwa hawamkubali, lakini wewe unavyomkubali mpaka nashangaa, unanchekesha! Jamaa alikuwa ni kings maker!
 
Those who were crying for RA were crying for purely personal reasons and gains....

Katibu mwenezi wa chama Nape na wengineo wenye nyadhifa za juu ndani ya chama na serikali wamewataja mafisadi hao wa3 bila kificho...haihusu sana kwanini wasimlilie Selelii ambaye personally he was more talk than action but inahusu sana kwa wananchi wale wa Igunga kuwa wanamlilia mtu wa aina gani ?

Maendeleo aliyoiletea Igunga na matatizo aliyoicause Tanzania kwa ujumla wake hayapimiki chungu kimoja...
 
Nilisikitishwa na kufadhaika sana, kuona baadhi ya wananchi wa jimbo la Igunga wakiangua kilio na baadhi yao kupoteza fahamu kisa Mbunge wao Rostam Aziz kajiuzulu! Mbunge aligubikwa na tuhuma na kashfa lukuki,ambaye Tanzania nzima ilikuwa ikipaza sauti ya kumkataa wakiwemo wana CCM wenyewe! Mbunge ambaye Bungeni hachangii hata hoja moja kimya muda wote, alinukuliwa bunge lililopita kukaa kimya miaka yote! Najiuliza Wanyamwezi hawa wanaelewa haswa maana ya Mbunge?!

Au kwao wao ni MFADHILI anayegawa tu pesa na kugawa Mahindi na Vyerehani!!Bila kujua hizo gharama anazotumia pesa amezitoa wapi!! Anatoa hela mfukoni wakati bungeni anaachia mabilioni ya fedha zinazotokana na kodi walizotozwa wao wenyewe katika madini, mazao yao na ng'ombe wao yakipotea katika Bajeti mbovu!

Wanategemea maendeleo ya nchi yataletwa kwa fedha za mfuko wa mfanyabiashara mmoja na siyo Mbunge mwenye hoja nzito bungeni, anayehoji zinapokwenda fedha zinazotokana na madini yetu!! Wanatabora hao hao hatukuona wakilia walau tone moja kumlilia Mbunge GODWIN SELELEIII ambaye Watanzania wengi wenye fikra timamu walikuwa wakimpenda na kumtegemea kama mtetezi wao bila kujali ni wa chama gani!

Huu mkoa una tatizo wajiangalie upya.


Walio mlilia ni wana igunga, kawafanyia mambo mengi ambayo hakuna mbunge atakaye yafanya kuanzia bima ya afya, barabara vijiji vyote, mabwawa ya kunyweshea mifugo na kumwagilia. hawana njaa kama wilaya zingine za tabora na mikoa jirani kana shinyanga na singida ambayo imekua na mvua chache.
 
Kazi ya mbunge siyo kupiga gumzo bila kufikiria, wasemaji wazuri wengi sana wanakuwa ni wanasiasa na watendaji wabovu, mfano ni Nyerere. Rostam ni mtu wa action na ndio maana unaona mafanikio yake kwenye Ubunge na kwenye biashara zake binafsi.

Ni jimbo gani la Tanzania zaidi ya la Rostam lenye bima ya afya kila kata? hapo kishapiga teke adui maradhi kwenye jimbo lake. Jimnbolake lina shule nyingi zaidi ya wanafunzi, lina walimu wa kutosha kila shule, hapo kisha piga teke adui ujinga.

Bado hayakutoshi? Nipe mfano hai kama nnavyokupa mimi, Selelii kafanya nini kipindi chake jimboni kwake?

RA alikuwa mfadhili wa Igunga , na nina wasiwasi inawezekana ni mhisani tu coz trend inaonyesha wakiondoka , wanatoka na "misaada" yao yote .
Kazi ya MP si kutoa misaada dada angu ,hiyo ni wajibu wa mwananchi yeyote kuisaidia jamii yake, au ndo maana magamba wanang'ang'ania zile 70,000/= ili na wao wakatoe misaada, bac tuongeze sifa moja ili uwe MP , KUWA BILLIONEA , akili za magamba bwana.
 
Back
Top Bottom