Wana-JF: Ujumbe Mzito Toka Serikali!

Status
Not open for further replies.
Ujumbe kutoka serikalini naona umejichanganya mno, nasema umejichanganya kwa sababu serikali yenyewe haijui serikali ni nini au ni nani.....

Tahadhari za ni lugha ipi ni matusi au sio matusi haiko bayana, ni sawa na mtu kuogopa kivuli chake mwenyewe au mkono wako wa kushoto unakuwa na siri ambayo mkono wa kulia haupaswi kujua! Mambo haya ni uhayawani.

Wana JF, huyu Field Marshal namtilia mashaka kama aliwahi hata kutumia manati utotoni achilia mbali kuwinda sungura.. ameleta ujumbe kutoka serikalini ktuonya na kututahadharisha lugha ipungue makali.

Field Marshal asome posting ya BRAZAMENI ya kwanza ambayo inaongea mengi mno yaliyo halisi na yanayogusa, awapelekee hao wanaojiona ni untouchable.

BRAZAMENI kazi nzuri unafanya.
 
Ni kweli matusi hapa si sehemu yake; ila what is matusi? Hivi kuelezea private life ya kiongozi ni matusi? Mbona hiyo pesa wanayotumia kwenye private life ndiyo hiyo hiyo wanayokuwa wameipata kwa njia za kifisadi? Ebu fikiria suala la jamaa aliyekuwa anahonga magari mekundu - si ni hela yetu ya BOT. Hivi tukijadili matumizi hayo eti tunaingilia private life yake? Kama wanataka tusiwajadili basi waache ufisadi.

Gazeti la serikali la Habari leo la Alhamisi Feb 21 2008, likiandika habari za wanaJF kukamatwa lilimnukuu IGP kama ifuatavyo "baadhi ya watu wanaojadiliwa kwenye mtandao huo ambao wanahusishwa na tuhuma za ufisadi, ndiyo walioulalamikia mtandao huo kuwa unatumika kuwakashifu na kuchochea hasira za wananchi dhidi yao"
Utaona basi kuwa walalamikaji ni hao hao watuhumiwa wa ufisadi; na je mtu akikashifiwa anaenda polisi au anaenda mahakamani direct maana hii ni civil case? Kama ni kuchochea hasira za wananchi ndiko kulifanya polisi kuingilia kati, je michango ya wabunge bungeni haiwezi kuwa imechochea hasira za wananchi zaidi tena live? Ebu tukumbuke mchango wa Mheshimiwa Ndesamburo "huko China, watu wa namna hii (mafisadi) wananyongwa tena hadharani". Kuna maneno yaliyotumiwa hapa JF anbayo ni makali kuliko hayo?
Tusikubali kuwekwa kapuni, tuwajadili hadi waache ufisadi, full stop.
UKWELI HATA SIKU MOJA HAUWEZI KUWA KASHFA
 
FMES,

Katika ujumbe wako nakubaliana na maneno yako mengi ingawaje mimi nitataka kutofautiana na wewe juu ya viongozi wa serikali na hasa mafisadi.

Hao watu hawazalishi kitu, wanalipwa na kodi ya wananchi ili watuongoze. Maisha yao ni fair game na kama kuna mambo wanafanya huko pembeni ni lazima wana JF wayaongee na tuyajadili.

Tutafanya makosa sana kama tutazuia kujadiliwa kwa maisha binafsi ya viongozi wetu maana vitu kama UFUKSA vina uhusiano na vitu kama UFISADI. Ukiidanganya familia yako waziwazi, je utashindwa kulidanganya taifa lako?
Ukimnyanyasa mfanyakazi wako wa ndani, je utashindwa kunyanyasa mfanyakazi wako wizarani?

Hata kama kiongozi ni mgonjwa basi tuseme bila kuficha. Kwani kama mtu ana UKIMWI nini cha ajabu hapo? Wao wenyewe wanawashauri watu wakapime, sasa kama wana ngoma basi wawataarifu wananchi, vinginevyo JF itawafanyia hiyo kazi.

Matusi yanayokatazwa kwanza ni juu ya sisi wenyewe wachangiaji na pia juu ya uzushi ambao hauna ushahidi kabisa kama ile habari iliyowahi kuweka hapa kuhusu ngono za rais. Nafikiri habari kama ile ilitoka nje ya mambo tunayoweza kujadili. Lakini kama rais anatembea na wafanyakazi chini yake, au kiongozi wa upinzani anatembea na wabunge wake, hizo habari lazima tuzijadili.

Tuwe makini sana juu ya hili na kuwe na uhuru wa kujadili kila kitu hasa kuhusu viongozi. Ila tu hii ya kuacha hoja iliyopo na kuanza kutukana na kuonyeshana umwamba naona ndio vitu vya kuacha. Muhimu ni kutumia lugha ya kiungwana kuwakilisha hoja. Maneno kama mjinga, hujaelemika, mshamba nafikiri yanaruhusiwa kabisa wakati maneno kama mpumbavu, kichaa nafikiri sio mazuri.
 
Yaani hata tusiongelee maisha binafsi ya Mkapa na Anna ati kwa kuogopa watagombana ama kuachana.
No, tutawaongelea mpaka watuambie ukweli, kugombana ama kuachana kwao si hasara kwa Tanzania bali biashara zao za ikulu.
 
Nina point to this topic

1. Hatupaswi kuingiliwa kabisa na zelikali, tuna uhuru wa kuchangia bila kuulizwa
2. Any public figure officer has to expect positive/negative reaction from the public, kwahuyo hata hashifa kama zinajenga ni sawa zikitolewa
3. Kuhusu kuweka magojwa na wakulu hadharani hilo naona sio sahihi, hata madaktari hawaruhusiwi kufanya hivyo, na hata dini zetu haziruhusu hilo.
 
Nina point tatu.
  1. Si sawa kupangiwa na serikali cha kujadili.
  2. Si sawa hata hivyo kutumia matusi hapa. Si sawa vile vile kusema vitu kama ugonjwa wa mtu. Hata daktari haruhusiwi kusema ugonjwa wa mtu, sembuse wana JF?
  3. Si kweli kwamba freedom ni absolute. We are free to do good; but no one is free to do evil. It is an axiom in Philosophy that freedom is not absolute. Truth is absolute but freedom is not.
Kwa hivyo basi, nakubali kwamba tuwe na standards hapa, lakini ziwe za kujipangia sisi wenyewe na sio kupangiwa na serikali.

Mkuu,
Standards za JF zipo na nashukuru moderators wamekuwa wakizikomalia sana. Haya masharti ya JF yamekuwa yakirudiwa mara kwa mara na moderators ili kutukumbusha kuwa katika msitari, Sema sasa kuna nyakati huwa wanazidiwa na wingi wa posts ambazo zina mushkeli, hivyo ni jukumu letu wote kama familia ya JF kuwashtua moderators iwapo tunaona mada iko nje ya msitari ama ina matusi. Mara nyingi hii huenda sehemu ya maoni/malalamiko. Hata jana nakumbuka kuna posti ya mmoja wa moderators ilikuwa na ujumbe huo wa masharti na kanuni za JF.
Nawasilisha
 
...mtu Ukishakubali Kuwa Kiongozi Ujue Your Life Is Up For Scrutiny ..including That Of Your Family Tena Nyumbani Tuko Fair Huku Nje Ni Balaa Watu Wanakuchambua Kweli ...kama Ulikuwa Kikojozi Utotoni Pia Watasema ..hawatasema Ni Personal..wataalamu Wa Pschology Wanaamini Tabia Za Utotoni Na Malezi Hu Influence Tabia Za Utu Uzima..

Yes Hata Kama Una Kisukari Au Ukimwi ..tutasema Kwa Kuwa Afya Yakoinagusa Usalama Wetu...na Wala Hakuna La Ajabu ..kwani Sera Ya Ukimwi Inasema Watu Wote Wana Haki Sawa..itakuwa Kosa Kama Mtu Atasema Kama Kebehi..hapo Atakuwa Amenyanyapaa....kama Umefiwa Na Wake Zako Tutasema....

Nafikiri Mkono Wa Serikali Unaweza Kuwasha Na Kuzima Tvt Au Rtd ..the Likes..lakini Mtandao Wa Computer Ni Moto Wa Nuclear Reactor Hauzimiki...[half Life..to Half...unavyowaka Ndio Unakolea ..moja Itaza Bilioni..ipo Siku Tutakuwa Wana Jf 15,000,000 Mtafanyaje!!!..basi Kwamisheni Maendelea Kama Mlivyochelewesha Tv Tanzania..mmezoea
 
Mkuu Brazameni, nimekusikia loud and clear mkuu kama nilivyosema mwanzoni kutofautiana ndio demokrasia yenyewe, na mkuu invisible, ahsante kwa kunielewa lakini I will go with maneno haya mazito hapa juu ya Mzee Mwalimu Moshi.

Ahsante Bros!
 
Inawezekana Mzee ES amevuka msatri kwa kusema "ujumbe kutoka serikalini". Labda angepunguza hilo neno serikalini, lakini the message is very clear.Kweli kuna wakati tunateleza na tunakuwa too personal badala ya kuangalia broader issues. For sure hakuna mwenye haki ya kusema kuseme nini, lakini pia tusipojiwekea mipaka kwa kuwa too personal, kweli credibility ya kijiwe hiki itachukuliwa na wengine. Freedom and openneess without some kind of limitations siku zote inakuwa na matatizo fulani, hakuna wa ku-tumilit tunatakiwa kujilimit wenyewe.
Tunaipenda nchi yetu, kwa hiyo tulinde credibility ya JF.
 
hao watoto wamespend 12hrs ulifanya juhudi gani kuwasaidia......msiwe mnakuja na matusi bila ya sababu.......we toa maoni yako tutaona kama yanaleta sense tutakuambia lakini sio kwa matusi


Mkuu Ogah,

Respect mkuu, maneno mazito haya juu!
 
Jamani na nyie tusijidhalilishe hivyo. Yaani ukisoma point za watu wengine hapa ni kama vile sisi ni watoto wadogo kiasi cha kutokujua matusi ni nini. Hili ni tatizo la muda mrefu na la kihistoria katika nchi yetu. Tulikuzwa kwa kuaminishwa kwamba viongozi wa serikali wana akili zaidi kuliko mtu mwingine na kwamba ni wao tu wanaojua chema na kibaya. Lakini ukweli ni kwamba huu ni uongo. Kuna wengi wana akili zao na hawapo serikalini. Na ukweli zaidi ni kwamba viongozi wengi waliopo katika serikali yetu hawana moral authority ya kutuambia kipi kizuri na kipi kibaya maana wameshajichafau mno.

Sasa sisi siku zote hapa tumekuwa makini mno na karibu kila mtu hapa ni moderator. Tumekuwa tukionyana mapema na hata kuwakemea baadhi yetu pale wanapoleta lugha ya matusi au kuzusha jambo ambalo halipo. Tena ni mara nyingi tu hapa mada zimefutwa baada ya kugundulika kilichokuwa kinajadiliwa hakikuwa na ukweli wowote.

Kimsingi JF hii ya leo ni makini zaidi kuliko serikali ya CCM. Sisi ndio tunaopaswa kutoa somo kwa serikali hii jinsi ya kuendesha mambo. Narudia tena serikali hii ya JK na CCM haina moral authority ya kutoa lecture kuhusu what is evil and what is good because itself does more evil than good. Kwa hiyo ujumbe tumeusikia lakini tunapaswa kuukata mara moja. Kuukubali ujumbe huu ni kukubali kuwa serikali hii ilikuwa sawa kuwakamata wenzetu!

Mwisho, when you become a public figure your life also becomes public. Sasa kama watu hawataki tuwasema mambo yao ya nyumba ndogo na kuvunja ndoa za watu dawa ni kuacha hizo nyumba ndogo na kuheshimu ndoa za watu na wala sio kutuwaambia sisi tusiwaseme. Tulikuwa na haki sana tu ya kumkemea aliyekuwa waziri katika serikali ya JK kumnyanganya mke mkuu wa wilaya mkoani Kigoma. Tena tulikasirishwa na tunaendelea kukasirishwa sana na kitendo hiki na tunaendelea kukilaani kwa nguvu zetu zote.

Mimi nasema madamu naendelea kuwa mjumbe wa JF nitaendelea kumwaga na kuunga mkono kumwagwa kwa madhira yote wanayoyanya viongozi wetu. Asiyetaka shauri yake.
 
Quote: Lunyungu

Kidogo nina maswali mengi kwenye siri uliyo tupa lakini mimi ni Mzee hapa I read between the lines.[/SIZE]


Mkuu Lunyungu,

Heshima mbele kaka, na ahsante kwa ujumbe wako mzito hapo juu!
 


Kwa hiyo ujumbe tumeusikia lakini tunapaswa kuukata mara moja. Kuukubali ujumbe huu ni kukubali kuwa serikali hii ilikuwa sawa kuwakamata wenzetu!

Kitila mimi bado sina hakika na sababu hasa za wana JF kukamatwa, for sure kama JF mambo yake ingekuwa ni kusema waziri kaiba mke, waziri kaiba mume au bongolander kaiba mchumba wa mtu, sidhani kama hata hiyo "serikali" isingekuwa na haja ya kuwasakama hao watu, na huenda ingefurahi sana. Kama ukiona hapa bongo magazeti yanayoungwa mkono zaidi ambayo hata kina-Kubenea wao hawasumbuliwi ni kama Kandanda kitandani, Kona ya fuska, lakini magazeti yenye real issues yanakumbwa na msukosuko sana. Sasa wanaotupa ushauri ni kwamba tusiwe na haya mambo ya udaku tuwe na issues za maana zenye maslahi ya taifa letu.
Hata hivyo kona ya udaku ipo........ukitaka kujua popularity yake uliza modertaors ni forum ipi inatembelewa zaidi, udaku ni one of the least visited, this tells it kwamba members wengi wa humu si wa udaku udaku!
 
Tumepokea ujumbe na mwenye uelewa amesikia na ahad ni kwamba tutajitahidi kutotukana, lakini wenye hasira kama ndugu zangu kadhaa wafanyeje, maana wao wakitukana hasira zao zinapungua kidogo. Labda tuwaruhusu kutukana kidogo kama vile shit, wajinga, wapumbavu, washenzi lakini si zaidi ya hapo. Mwasemaje waungwana, maana kwa hali halisi hayo siyo matusi
 
Hata kama ni kutoa muongozo si kwa wakati huu ambapo watu wanauguza kidonda.
Sijawahi kuona mtu anatoa muongozo kwa forum, i think hiyo ni kazi ya Moderators na ndio maana wakawepo kwani hata gazeti likianzishwa linakuwa na malengo na interest za upande fulani, lengo la JF ni kukosoa na kuelekeza pale Serikali inapopotoka sasa kwanini umpangie mtu cha kusema hapo?

Kesho utasikia wanawapangia na wanasiasa wa Upinzani cha kusema, hili ni jukwaa suala la matusi hakuna mtoto humu hilo linaeleweka lakini wakati mwingine mtu hutumia maneno hayo ya kisifa kutokana na jazba!! na kama si tusi basi mlengwa angekuwa hapo angepigwa hata makofi wkati mwingine "Mnayoita matusi" hutumika ku express hisia za mtu.

Wabillah Tawfiq
 
Nikuunge mkono Mwl Moshi kwa yote matatu kimsingi, lakini natofautiana nawe kuwa hata "truth" sio "absolute" ndio maana mambo mengi bado yako debatable. Mambo mengi yanayochukuliwa kuwa "truth" ni makubaliano tu ya jumuiya fulani (wanataaluma, jamii, nk) kuwa yachukuliwe hivyo, na siku ushahidi tofauti ukipatikana kilichokuwa "truth" chaweza kubadilika kuwa sivyo tena (na hivyo wanakubaliana juu ya "ukweli mpya"). Mifano iko mingi. Kwa hili peke yake, si sawa hata kidogo kuzuia watu wasijadili jambo fulani, kwa sababu hata hiyo dhana tu ya kuwa mjadala huo uwepo au usiwepo ni debatable. Kwa mfano tunapozungumzia maisha binafsi ya kiongozi, tunamaanisha nini, na kwa mujibu wa nani? Kujadili afya ya kiongozi ni sawa au si sawa? Kimsingi hakuna mwenye jibu ambalo tunaweza kulichukulia kama "absolute truth" kuhusu swali hili, wengine watasema ni sawa na watatoa sababu, wengine watasema si sawa, na sababu watakuwa nazo, na zote zinajadilika. Kinachopaswa zijadiliwe zote, hoja "nyonge" itajifia yenyewe, na zile zenye nguvu zitabakia.

Labda kama Field Marshal ES anataka kubadilisha slogan ya JF iwe kuwa "We no longer dare to talk openly!" lakini tukumbuke members wengi wako hapa kwa kuwa wanapata nafasi ya ku-ventilate. Jibu la kuwapa hao serikali ni sisi kuendelea kujadili hoja yoyote inayofika ukumbini humu, zile zenye udhaifu zitajifia zenyewe na zile zenye nguvu kimantiki zitadumu na kuleta impact kama ambavyo tayari imeshatokea huko serikalini na kwingineko zitakakogusa.

Kwa maneno mengine, Mkuu Kithuku, 'truth is socially constructed'.
 
Ujumbe mzito umetufikia, Ndani yake pana ukweli unaopaswa kuzingatiwa. Matusi yakizidi sana yanakera kwa pande zote mbili. Si mara moja si mara mbili, tena majukwaani, watumishi wa ummah pamoja na Rais mwenyewe, aliyopo na waliopita hutukana na kutoa maneno ya kashfa na kejeli kwa baadhi ya wananchi. Wafanyapo hivyo, wanategemea majibu ya namna gani? Tusi ni tusi si lazima liwe la nguoni. Dharau nayo ni tusi pia iwe kwa maneno au kwa vitendo. Si vibaya nao hao watumishi wa umma ndani ya vyama vya kisiasa na serikali wakajitazama na kujirekebisha, kama vile ambavyo nasi tukajitazama na kujirekebisha.

Tofauti nasi, watumishi wa umma, familia zao, mali zao na vitendo vyao ni lazima wa/zi/vi-chunguzwe na wa/zi/vi-jadiliwe na umma wakati wote. Lazima walitambue hilo na halikwepeki. Wenzetu wanamsemo wao. "kama huwezi kustahimili joto la jikoni, basi usiamue kuwa mpishi."
 
Sikujua kama hapa JF tuna mwalikilishi anae act as middleman btw JF na serikali, hii ni elimu mpya nimeipata leo.

Labda Mods or Invisible atatuwekea wazi ni lini/kikao kipi kilimchagua/mteua mwakilishi huyu ili tupate mwanga wa kuelewa vizuri, nachelea na na reserve my comments mpaka nitakapo pata mwanga juu ya hili. Isije ikiwa tunadili na self-proclaimed middleman na haya mambo ya u double agent yana madhara makubwa sana, mtu anataka apendeze kote kote nina smell tunakokwenda ni kubaya.

I would hope na ningeupa uzito ujumbe huu kama ungetoka kwa vijana wetu waliokuwa wanashikiliwa kule kwani ni wao ndio waliokuwa mikononi mwa "watawala" otherwise any attempt ya ku capitalise on this saga by huyu "self-proclaimed" mjumbe ni wa kupuuzwa tu....

Kama wana lolote wanaona linachupa mipaka Invisible amefanunua wazi kuwa milango yake ipo wazi na wapo tayari kulishughulikia. Sasa hawa wanaojitafutia umaarufu sijui "ujumbe mzito kutoka serikali" wameupata wapi watuambie ni nani huyo huku serikali "aliemtuma?" kwani serikali ina mkono mrefu hata mwenyekiti wa mtaa nae ni serikali.

JF is bigger than kuokota habari mitaani na kuzi sensationalise kwa vichwa vya habari vikubwa, tuna chambua pumba na mchele hapa.

Watu wengine bwana sijui tuwaweke kwenye fungu gani yaani ovyoooo...
 
[*]Si kweli kwamba freedom ni absolute. We are free to do good; but no one is free to do evil. It is an axiom in Philosophy that freedom is not absolute. Truth is absolute but freedom is not.[/LIST]Kwa hivyo basi, nakubali kwamba tuwe na standards hapa, lakini ziwe za kujipangia sisi wenyewe na sio kupangiwa na serikali.


....good point,na FM kuhusu ndoa za wakuu na familia zao kama hazina maadili na kuendelea kuhudumiwa na kodi zetu zitaendelea kuwa mali yetu hapa maana ufuska madarakani ndio mwanzo wa all evils,mimi break ni kwenye file za afya za watu tuu mengine yoyote halali,ila wakuu mkumbuke msumeno unakata pande zote kwa hiyo sitashangaa siku moja akatokea mjanja ambaye hatumii siasa akatutandika na lawsuit la nguvu na kuiacha JF chali kwa ajiri ya midomo yetu michafu,tujitahidi kuandika yaliyo ya kweli bila kupakaziana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom