Wana JF,Tujulishane Viwanda vilivyo uliwa na Serikali ya CCM Tangu uhuru

MMMT- Mang'ula Mechanical Machine Tools- mitambo midogo midogo baadae kingeweza kutengeneza hata silaha za kivita.
Sungura Textiles, Dar- nguo
Kilitex, Dar- nguo
Tanganyika Packers - Nyama za kopo
Moro Shoe - Raba mtoni za ukweli
NABICO-National Bicycle Compan
TAMCO- ku-assemble magari aina ya scania
 
Mkuu ilivikuta vingapi na kuviua?

Labda ungesema tujulishane viwanda vilivyoanzishwa na kisha kuuliwa na Serikali ya CCM tangu Uhuru.

naomba umsamehe bure, nadhani swala linaeleweka.
Ccm inayokera watu sio kile chama maarufu kilichopendwa sana, kilichosimamia mapinduzi mbalimbali, kuleta usawa kwa wananchi wote, elimu kwa watoto wa masikini, kujenga viwanda nchi nzima, kusimamia maadili ya viongozi. Chama kile kinakumbukwa na wengi, na ni pride ya tanzania hadi sasa.
Ccm anayozungumzia ni hii tunayoiona sasa, iliobadili kimya kimya maadili ya chama iliokosa uelekeo,inayochefua, isiosafishika, inayotufanya tufiche kadi zetu mbali sana. Hii ndio iliouza viwanda migodi, na ardhi kwa wageni. Umeshajiuliza viwanda vyetu ya nguo ambavyo 'havijakufa' vinapata wapi vitambaa, imports zake za vitambaa inashangaza, kwanini hawatumii pamba yetu?
 
Machine tools-Moshi



Nikikumbuka mkoa mmoja tu ambao naufahamu vizuri sana maana nimekulia hapo ni Morogoro mkoa huu miaka hiyo ya 1994 kurudu nyuma ulikuwa na viwanda visivyo pungua 7 ambavyo vilikuwa muhimu sana kwa ustawi wa kiuchumi wa watu wa Morogoro, ajira haikuwa shida. Leo takribani vyote isipokuwa Tumbaku na Canvas( kinajikongoja) vimekufaa. Viwanda hivyo ni kama vifuatavyo .
1. Canvas Morogoro- kilikuwa kinaweza kuzalisha zaidi ya tani 200,000 za maturubai ya kuuza ndani na nje ya nchi, kilikuwa kinaweza kuajiri zaidi ya wafanyakazi 5000 (including vibarua)
2. Magunia Morogoro-kilikuwa kinaweza kuzalisha magunia tani nyingi sana takribani tani 150,000 kwa mwaka huku kikiwa na uwezo wa kuajiri wafanyakazi wasiopungua 4500
3. Kiwanda cha kutengeneza vyombo vya udongo- Celamic kilikuwa kinatoa ajira za kudumu sizizo pungua 3000
4. Kiwanda cha viatu vya "Bora" kilikuwa kinatengeneza viatu vizuri sana vya ngozi vikiitwa Bora.. kilikuwa kinaajiri zaidi ya watu 3800
5. Kiwanda cha Vitenge na Khanga cha Polyster kilikuwa kinatoa ajira nyingi sana kwa wakazi wa Morogoro wasiopungua 5400
6. KIwanda cha Ngozi Tanarees Morogoro kilikuwa kinachangia sana uchumi wa watu wa morogoro hasa wafugazi kwasababu soko la Ngozi za wanyama lilikuwa la uhakika zaidi ya watu 800 walikuwa wameajiriwa katika kiwanda hicho
7. Kiwanda cha Asante Moproko, kilichokuwa kikitengeneza sabuni za Komoa na mafuta ya kupikia ya asante Moproko kilikuwa kinatengeneza zaidi ya ajira 1500 kwa wakazi wa Morogoro
8. Kiwanda cha Tumbaku Morogoro kabla ya kubinafishwa kwa makaburu enzi hizo za Director Koreen kilikuwa kinaajiri zaidi ya wafantyakazi 3700
Kama kunamwenye kumukumbuku za viwanda vya Morogoro anisaidfie kuongezea leo zaidi ya winda 7 vimekufa mazima ukitoa kiwanda cha tumbaku, ambacho kinaendelea but watuwake wanalipwa ujira mdogo sana.. huku wakifanya kazi mpaka weekend na siku za sikuku rasimi kama 9 december na Krismas na sikuku za Idd.. watu wake wanalipwa kati ya 100,000 mpaka 130,000

Lakini ndio hivyo leo Morogoro ni moja wapo ya mikoa maskini sana hasa kiuchumi viwanda vimebinafsishwa na vimekufa takribani vyote, hicho Canvas ambacho kimechukuliwa na Abood (sasa Mbunge) ni sawa na hakuna kitu pale.. wafanyakazi hawafiki hata 500
Leo vyote ni magofu tu yamebaki, na hao wawekezaji uchwara wamekwapua na mashine zilizokuwepo awali.. daaha inasikitisha
 
NMC iliyokuwa na matawi nchini kote..you can imagin ilikuwa na waajiriwa wangapi
 
Back
Top Bottom