Wana JF, ni halali kweli UDOM kuitwa chuo cha kata?

Acha kelele wewe kwanza hufai kuwa Jack Bauer, inabidi tukuite Charles Logan.
Kukufahamisha kuwa usi-connect post yangu na mimi kusoma UDOM ni kujidhalilisha?
Hizo school of thought zipo kibao kwenye management, economics, philosophy etc. Nilikuelewa vyema, but aim ni kukufahamisha mimi ni Mtanzania na sijasoma huko UDSM, UDOM wala MZUMBE, na so far sijaona tofauti yoyote kati ya graduates wa vyuo vya Kitanzania.

Vya nje ndio vina tofauti au sio? Kazi ipo
 
Sina uhakika na haya,kwani vigezo vipi umetumia kutambuwa uduni wa wanafunzi na familia zao? pia hakuna chuo chochote duniani kimeanza na kuwa na maprof kama walimu,ni lazima uajili then usomeshe,sasa mkuu mimi sikuelewi unapozungumzia vodafasta,sijui wapi wanatowa degree za namna hiyo sijui tupe chuo kinacho andaa walimu wenye degree voda fasta

mapinduziiii daimaaaaaa

wawili kati ya walimu muhimu sn udom ni kaka mmojaaliwahi kuwa katibu wa serikali ya wanafunzi Tumaini, huyu bwana alisoma Bachelor ya Tourism akamaliza mwaka 2008 na hadi sasa hajasoma masters anasubiri skolashipu. Mwingine ni mdada alisoma kozi kama ya huyo katibu sa serikali ya wanafunzi wa Tumaini, mbaya zaidi Curriculum ya hiyo tourism imekaa kimagumashi sana. UDOM ni chuo cha kata tu
 
wawili kati ya walimu muhimu sn udom ni kaka mmojaaliwahi kuwa katibu wa serikali ya wanafunzi Tumaini, huyu bwana alisoma Bachelor ya Tourism akamaliza mwaka 2008 na hadi sasa hajasoma masters anasubiri skolashipu. Mwingine ni mdada alisoma kozi kama ya huyo katibu sa serikali ya wanafunzi wa Tumaini, mbaya zaidi Curriculum ya hiyo tourism imekaa kimagumashi sana. UDOM ni chuo cha kata tu

Kuna watu wabishi tu kwa asili hawataki kuambiwa ukweli. Wanaoita Chuo cha kata ni wanafunzi wenyewe wa Udom sasa wengine huku wanapanic na kuanza kutukana wenzao mara umesoma wapi? sijui hujasoma? mara taahira? Lakini ukweli upo palepale hata kama ni mchungu UDOM ni Chuo cha Kata tu hakina jina jingine kwa sasa
 
Wana jf napenda tu kusema machache.
Chuo kikuu kinafikia hatua ya kuwa chuo bora baada ya mchakato na muda fulani kupita. Kwa chuo kikuu dodoma, ni mapema mno kukiita cha kata au vodafasta. Muda wahitajika kuamua ubora wake. Kuona kuwa ni duni baada ya kulinganisha na vyuo vingine vikongwe nchini kama udsm si sahihi. Ukiangalia historia, hata udsm kilianza kama school tu kabla ya kuwa affiliated na uea. Lakini hatua kwa hatua kimeimarika.

Pia muhimbili (muhas) kilikuwa kidogo sana wakati kinaanza. Maprof walikuwa wa kuhesabu, lakini sasa kimepiga hatua kubwa sana.

Ukija ardhi (aru), nacho mwanzoni hakikuwa na madokta, lakini wakajiwekea malengo kuwa baada ya miaka 10 wawe na madokta wa kutosha na hali imekuwa hivyo. Aru ina maprof na madokta wengi sana.
Vivyo hivyo mzumbe, na vyuo vingine vingi unavyo vifahamu.

Sasa tukija kwa udom, twahitaji muda kuanzaia miaka kumi na kuendelea ili kuwe na ubora unaohitajika kulingana na vigezo vilivyo wekwa na tuc. Huwezi leo leo ukajenga majengo, papo hapo ukawa na walimu wenye phd na maprof. Hayo ni mambo yanayo hitaji muda. Na bila shaka yatakuwepo kwenye mipango yao ya muda mrefu na wa kati. Hatimaye tutakuwa na udom iliyo na sura kama vyuo vingine ambavyo mnadhani ni bora.

Pia labda ushauri kwa udom, katika kipindi hiki cha shida ya walimu, ni bora kuajiri walimu toka nje ya nchi. Hiyo inasaidia sana kupata ujuzi wa watu toka sehemu nyingine ya dunia. Binafsi sipendelei kufundishwa na mwalimu aliyesoma degree ya kwanza tanzania, ya pili tz, phd tz. Nahisi nakosa stadi toka nchi zingine.

Halafu lingine ni kuwazoeza wanafunzi wetu kusoma vitabu. Hilo ni tatizo sana. Wanafunzi wetu wengi hawazoezwi kusoma vitabu. Vitabu vinakufanya hata kama umesoma chuo duni namna gani, unakuwa na stadi, uelewa na ujuzi wa hali ya juu na kujiamini pia. Elimu yetu ya tz inatupa shida sana mara unapokwenda kusoma ulaya na marekani ambako wanafunzi na jamii yao na kwa ujumla ina utamaduni wa kusoma vitabu. Unakuta wenzako wanasoma vitabu mulivyogawiwa kwenye kozi kama wanacheza vile, na mukienda kwenye semina wanakuwa fiti, huku wewe vinakutesa mno kuvisoma.

Hivyo udom ni chuo kichanga sana, chahitaji muda ili kiwe bora. Kufuata mipango waliojiwekea ndiyo msingi wa maendeleo ya chuo hicho.
 
nina mdogo wangu anasoma hapo ila nilikuwa sijui ila kwa haraka haraka nimekubali kuwa ni chuo cha kata.... maana hadi ilipofikia ni zimamoto kama ratiba za ligi kuu kipindi cha Ndolanaga na FAT
 
Ni chuo pekee ambacho adi walimu wa shule ya msingi nao ni ma lectures, sasa ni kwa nini kisiwe chuo cha kata
 
Wanaosoma udsm wanaita udom chuo cha kata kwa sababu wazijuazo wao wenyewe.

Na waliosoma vyuo katika nchi zilizoendelea wanaita udsm chuo cha manzese, kwa sababu hizohizo. Hii ni tabia tuu katika nyanja za elimu. Haina maana kwamba muhitimu wa udsm ana kiwango kizuri cha elimu kuliko yule wa udom.
 
wanaosoma udsm wanaita udom chuo cha kata kwa sababu wazijuazo wao wenyewe.

Na waliosoma vyuo katika nchi zilizoendelea wanaita udsm chuo cha manzese, kwa sababu hizohizo. Hii ni tabia tuu katika nyanja za elimu. Haina maana kwamba muhitimu wa udsm ana kiwango kizuri cha elimu kuliko yule wa udom.

kweli kabisa, udsm wana tabia ya kuwaona vyuo vingine kuwa yebo yebo, hata mimi mwenyewe nilikuwa nafikiria kuwa udsm ni bora. Lakini kumbe zilikuwa fikra mgando kama za ccm na vyama vya upinzani. Tulizoea chuo kikuu kimoja miaka nenda rudi. Mpaka ikafikia kuwa ukisema nasoma chuo kikuu watu walijua tu ni mlimani - udms. Kwa hiyo ilikuwa chuo kikuu maana yake mlimani - udsm. Lakini sasa vyuo ni vingi. Ukisema nasoma chuo kikuu mpaka wakuulize chuo gani.

Kwa hili la udom naipongeza serikali, maana baada ya miaka kumi hakitakuwa tena kama kilivyo sasa, kitakuwa bora zaidi. Siku zote mwanzo huwa mgumu. Hivyo udom lazima ipite kipindi kigumu.
 
JAMANI MI SIMO..........ILA ETI NIMESIKIA SOCIALOGY inafundishwa na MHINDI....!

SASA NAJIULIZA ANAFUNDISHA SOCIALOGY YA WAPI?.........INDIA AU TZ?

MI SIMO....
 
Mdogo wangu amemaliza UDOM kwenye college ya I.T mwaka huu, na alipata multiple admission moja ya UDSM engineering, ila akaamua kwenda UDOM kusoma I.S na miaka yote aliyosoma pale alifanya field na sasa anafanya kazi kwenye kampuni flani kubwa hapa dsm inayotoa huduma za Internet (ISP), na yuko nondo zaidi hata ya dogo wangu mwingine aliyemaliza UDSM Computer Science mwaka jana.
Huko kwenye nyekundu ndiko kunakoonyesha kabisa hiki ni chuo cha kata. Nani anamaliza chuo cha ukweli anaenda kufanya cazi internet cafe? Hii haihitaji elimu kubwa...ni uwezo wa kuwasha na kuzima pc na kufungua email-moja kwa moja elimu ya shule za kata inatosha.

Labda utoe maelezo mengine yakumaanisha ulichokisema but kwa ufasaha....
 
Nafikiri tusifanye kama tuna piga kelele tuweke hoja zetu vizuri. Kama JF ni kitovu cha mawazo basi hili suala la chuo gani ni chuo cha wilaya, kijiiji, kitongoji, mkoa au kata tuvitolee hoja zinazokubalika na pia tutoe mapendekezo mbadala ya kutatua matatizo haya. Maana mwisho wa siku yatatuhusu watanzania wote.

Sikubaliani na anayetoa hoja ya kujengwa majengo haraka hii si hoja, vile vile suala la walimu wa masters kama wanafundisha, bado hata huyu nafikiri hajui vyuo vikuu hawa wanaweza kusaidia kufundisha au kufundisha kabisa na ndio maana baadhi ya nchi unakuta Assistant Leactures/Professors jina tu linajieleza.

katika ulimwengu wa leo ambapo vyuo vimekuwa vingi na pia siasa zimetawala dunia, hili la kukosekana kwa walimu katika field fulani fulani halikwepeki. Hata nchi zilizo endelea hata marekani suala la walimu wa kufundisha vyuo vikuu ni suala ambalo lipo. Ndio maana utaona wahindi takribani dunia nzima katika vyuo mbali mbali.

Nafikiri hata chuo kikongwe kama UDSM bado watu wenye masters ndio muhimili wa chuo, ndio wanaofundisha wakisaidiwa na T/As. Hivyo tukienda mbali kujadili kipi ni chuo cha Tarafa/Mkoa/kijiiji/Kitaifa na Kimataifa unaweza kukuta Tanzania tuna vyuo vinavyo fanana. Na tukienda uganda tunaweza kuwa na definition nyingine. Kama UDOM ni cha Kata na kidogo tuwajua walimu wanaofundisha pale UDOM na waadhiri angalau kutoka nchi za mbali na wanaojulikana katika taaluma zao kimataifa, je vyuo ambazo hakuna mwadhiri hata mmoja anayejulikana hata katka Tanzania tuviiteje?

Tusiite vyuo kwa majina kwa kuchukia wanasiasa fulani fulani(chuki binafsi) tutumie hoja za kisomi zenye mwelekeo wa kubainisha tatizo na kulitafutia ufumbuzi. Sijabahatika kufika UDOM hila watu wengi niliyokutana nao wamenielezea na nimeridhika nagalau kidogo pamoja na challenges wanazokumbana nazo ambazo ziko kote duniani.
 
Msishangae hao ndio walivyo ,wana msongo wa mawazo kila lifanywalo na baba riziwani kwao donge.kusingekuwa na chuo wangesema saaana na matusi juu,sasa kuna chuo wanakejeli. tuwaache ,sisi tuipe nguvu Udom ,itoe huduma bora sana.

Maana hwa ni product ya maprofesa wa kizamani wa Kitanzania ambao ilikuwa inawauma sana kuona wenzao wanaelekea kupata uprofessa, ndio maana tunamapungufu yote haya.wanafelisha wanafunzi kwa chuki na mara nyingine ngono inakuwa ndio muamuzi wa nani akae nani apite.

Hawa wamerithi wivu, uchoyo na roho mbaya, wameona chuo kipya kikubwa kimeanzishwa wakaona duh ,Sasa kila kona ya tanzania kutakuwa na wasomi na hakuna tena kutunatuna , roho inawauma saaana kwa wivu wa Watanzania wenzao kupata elimu kwa wingi. Be carefull UDom is coming and is comming with high power hakuna tena kibri

Poleni samaki
 
Wakuu tufanye kauchabuzi kidogo.

Concept ya chuo cha kata ningeni sana, chimbuko lake ni mwaka 2006/07 ambapo ujenzi wa secondary za kata nchini ulianza. Hivyo kabla ya malamiko nivyema kuchambua concept husika. Je kwanini secondary za serikali zilizojengwa kuanzia 2006/2007 zinaitwa za kata. Pili, Secondary hizi zina sifa (characteristic features) zipi?, tatu, je Chuo kikuu cha Dodoma kinashiriki (Share) features zozote katika hizo? Nadhani mpaka hapo majadala utaongozwa na hoja kuliko jazba nilizoziona hapo juu.
 
Didia acha ubembuzi wa kibabaishaji. ndio maana wasomi wetu wanashindwa kuwa compitent kimataifa kwasababu wamejaa maubishi siku zote,so once employed or assigned to international posts wanashindwa kuwa compitent.sekondari za kata ni mpango wa serikali kuhakikisha kwamba kila kata ina sekondari ,full stop.

Je, unalinganisha nini na Udom. Kile ni chuo cha kiTaifa. You know what, kama taifa letu linategemea kizazi kinachozungumza humu JF then we are lost.kwa sababu wengi wana msongo wa mawazo nadhani ni hang over za uchaguzi, i know its not easy to take off the pain . Tujaribu kuzoea this is politics.

Poleni Samaki
 
Last edited by a moderator:
udsm just cant accept that there are other universities in this country,they are like ccm,the just dont want challenges,.KTK ULINGO WA ELIMU YA JUU UDSM KA CCM BADO WANAISHI KWENYE MFUMO WA CHAMA KIMOJA.
 
Huko kwenye nyekundu ndiko kunakoonyesha kabisa hiki ni chuo cha kata. Nani anamaliza chuo cha ukweli anaenda kufanya cazi internet cafe? Hii haihitaji elimu kubwa...ni uwezo wa kuwasha na kuzima pc na kufungua email-moja kwa moja elimu ya shule za kata inatosha.

Labda utoe maelezo mengine yakumaanisha ulichokisema but kwa ufasaha....

Mkuu kuna tofauti kati ya ISP na internet cafe, Unajua hivi ni vitu vya technologia. ISP ni internet Service Provider kama vile African Online, na wengine wote wanaounganisha wateja/watumiaji wa kawaida/mashirika katika mtandao wa Internet. Siyo kama pale internet Cafe za posta, hila hawa ndio wanaleta huduma ya mtandao katika sehemu za Internet cafes na makampuni mbali mbali. Kwa hilo unaombwa kufuta usemi wako.
 
MUHAS na ARDHI ni kati ya vyuo vilivyoanza na walimu wa kutosha.we unaishi dunia gani?

Wewe Jackbauer wacha kutudanganya Katika Chuo ambacho walimu wake wengi hawana sifa ni MUHAS.. kwani hao wanaojiita ma sn lecture wengi wao hawana PhD na hasa kwenye clinical medicine ma Pro ni wachache sana hivi juzi tu watu ndiyo wamepewa huo kuwa ma Ass pro lakini ukiangalia CV zao zinatia kichefu chefu kwani wengi wao publication 0.na walimu wenye master kwa clinical medicine ndiyo wanaotoa lecture na hao hao huwa wanawasimia wanafunzi wa master...na katika basic science wako wenye MD tu basi na wanasomesha je MUHAS pia chuo cha kata..
Na kuhusu jambo jengine ambalo huna hana idea nalo USA in general more 30% ya wananchi wake wana degree ya kwanza na kuendelea. na katika utafiti uliofanyika karibuni mji ambao una degree holder kidogo basi ni 19% ya population ya mji huo.kwa hivyo kijana kabla ya kusema kitu fanya utafiti wako.mimi nimeshafundisha MUHAS..
 
Sina uhakika na haya,kwani vigezo vipi umetumia kutambuwa uduni wa wanafunzi na familia zao? pia hakuna chuo chochote duniani kimeanza na kuwa na maprof kama walimu,ni lazima uajili then usomeshe,sasa mkuu mimi sikuelewi unapozungumzia vodafasta,sijui wapi wanatowa degree za namna hiyo sijui tupe chuo kinacho andaa walimu wenye degree voda fasta

mapinduziiii daimaaaaaa

Umeambiwa wengi ni rafiki zake na kusema eti uanze na walimu wa masters ili upate walio na uwezo haiwezekani inatakiwa upate professionals ndio uwatengeneze wengine proffessionals.

Kimsingi sipendi kuwasema chuo ni cha kata lakini nimekuwa naogopa kuiangalia mbele maana naona ni chuo kinachokuzwa kisiasa na naogopa na wanazuoni wake kujipa kifua kisiasa.
Sifahamu kama chuo hicho kimesheheni wajuzi wa kutosha lakini nadhani hawatoshi maana ukubwa wa chuo unaonyesha wazi haiwezekani kwa kipindi hiki kifupi kukawa na watu wa namna hiyo matokeo yake huwa kuna kanjia kamkato ka kupata malecturers wa part time ambao kamwe hawako makini katika usahihishaji na mwishowe watu hujisifia kwa GPA za juu wakijiriganisha na vyuo fulani wakati ukweli ni kwamba hakusahihishiwa vizuri kwa kuwa lecturer hana mda wa kutunga sup exams.

sifa za secondary za kata

Ni shule zinazotangazwa kama mafanikio ya kisiasa wakati sio kweli ni shule za wanancvhi na mimi nikiwa mmoja wao waliojenga kwa ajili ya watoto wao(UDOM ni chuo cha wafanyakazi maana pesa imetoka NSSF hiyo mimi kama mfanya kazi nimechangia kupitia michango yangu)
Shule za kata hazina walimu wa kutosha na waliopo hawana sifa (Sawa na UDOM lecturers wengi wana Degree or masters)
Shule nyingi za kata zilianza kufanya kazi wakati bado zinajkengwa =UDOM
UDOM=CCM
 
Back
Top Bottom