Wana JF, ni halali kweli UDOM kuitwa chuo cha kata?

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Ndugu zangu ma GREAT THINKERS
naomba niwaulize swali moja tu leo juu ya uhalali wa baadhi ya wapinga maendeleo ya kielimu ktk JF kukiita chuo kikuu cha dodoma kuwa ni CHUO CHA KATA,ningependa kutambuwa ni vigezo vipi wapinga maendeleo ya kielimu hapa JF wanavitumia ktk ku grade UDOM kama chuo kikuu cha kata?

mimi nadhani umefika wakati baadhi ya wapingamaendeleo ya kielimu hapa jf wakubali mchango mkubwa uliotolewa na serikali yetu ktk kukijenga hiki chuo,kwani tutambuwe kuwa ktk Dunia ya sasa bila elimu huwezi kuendelea

May be tubomoe chuo cha UDOM ili kuwaridhisha baadhi ya wana Jf wasiokubali kuwa UDOM ni chuo kikubwa pekee hapa TANZANIA na chenye msaada mkubwa ktk taifa letu kimaendeleo

Wana jf kuna uhalali kweli wa kukiita chuo chetu kikuu cha udom kuwa ni chuo cha kata? ama kwa sababu msingi wake ni CHIMWAGA jengo la mikutano ya CCM? hivyo inatufanya tuendelee kuwa na fikra zile zile za kila siku?

karibuni jamvini
MSEMA UKWELIIIIII HAPENDWIIIII DAIMAAAAAA

mapinduziiii daimaaaaaaaaaaa :target::target:
 
Elimu siyo siasa!!!! Ni chuo cha kata na sababu hizi hapa

1) Wanagraduate bila mafunzo ya vitendo
2) Walimu wao wengi wana bachelor au masters degree (Kawaida hawa ni tutorial assistants)
3) wanaoapply hapo wengi ni wasio na matumaini vyuo vizuri hapa TZ

Labda wewe unafikiri chuo ni majengo! La hasha! Chuo ni elimu bora.

Conclusion

UDOM ni chuo cha kata mpaka hapo kitakapokuwa na walimu wenye sifa na wanafunzi bora
 
nadhani mkuu ungejaribu kufuatilia cv za walimu waliopo pale kwanza then ndio uongee
kwani usemacho kinautofauti mkubwa sana,pili umefika wakati tutoe kutu tulizonazo ktk vichwa vyetu kwani malanyingi tunatumia maji ktk kufikilia na sio bongo

mapinduziiii daimaaaaa
 
Siyo nifuatilie nawajua kwa majina na wengi ni rafiki zangu.
 
1 ujenzi wake ulifanyika ndani ya muda mfupi
2 kilijengwa ili kukabiliana na wingi wa form 6 leavers waliotokana na mpango wa MMES
3 Ujenzi haujakamilika lakini chuo kimeanza kutumika
4 wengi wa wanafunzi wake ni kutoka familia duni
5 walimu /lecturers ni wachache na most of them ni wale wa voda fasta.
6 ni mojawapo ya mafanikio ya serikali ambayo hutajwa mara kwa mara kwenye sekta ya elimu.
Jaribu kulinganisha hayo mambo hapo juu na mwenendo mzima wa shule za kata,utapata jibu kuwa UDOM ni chuo cha kata!!
 
Sina uhakika na haya,kwani vigezo vipi umetumia kutambuwa uduni wa wanafunzi na familia zao? pia hakuna chuo chochote duniani kimeanza na kuwa na maprof kama walimu,ni lazima uajili then usomeshe,sasa mkuu mimi sikuelewi unapozungumzia vodafasta,sijui wapi wanatowa degree za namna hiyo sijui tupe chuo kinacho andaa walimu wenye degree voda fasta

mapinduziiii daimaaaaaa
 
Hivi nyie mnaokiponda udom mnakunya akili au?
Hamfikirii kuwa kodi zenu mnazokatwa kwenye mishahara
yenu zimechangia kujenga pale?
Badala mjivunie angalau kodi zenu zimefanyia jambo la heri bado linalalamika.
 
Ni Chuo cha kata tu, no way out. Binafsi sikuwahi kuita jina hilo mpaka juzi rafiki ambaye anasoma pale aliponiambia yupo Chuo cha kata. Kuhusu sifa za Walimu wanaofundisha pale hakuna ubishi kwamba wanazo sifa zisizokidhi haja. hata wao wanajua hilo kama una rafiki yako anfundisha pale wasiliana naye kama yupo objective atakwambia ukweli. By the way wanoita Chuo cha kata sio wanaJF pekee ni jamii nzima yenye mashaka na elimu inayotolewa pale
 
ok tufanye nini sasa ukiwa ni mmoja wa wapingaelimu ndani ya JF SEMA nini kifanyike ili tuondokane na kauri yako isiyoweza kubalika daimaaa?

mapinduziiii daimaaaaa
 
Kwa mara nyingine nasema wanaoponda UDOM na Mataahira na inabidi wakapimwe akili, wanapelekwa na hisia na chuki na wivu vimewatawala,.

Nimejaribu kufanya utafiti nikaona wote wanaoponda UDOM ni vilaza especially wanaotoka katika vyuo flani flani ambavyo kwa sasa vinaonekana kufunikwa na UDOM.

Mdogo wangu amemaliza UDOM kwenye college ya I.T mwaka huu, na alipata multiple admission moja ya UDSM engineering, ila akaamua kwenda UDOM kusoma I.S na miaka yote aliyosoma pale alifanya field na sasa anafanya kazi kwenye kampuni flani kubwa hapa dsm inayotoa huduma za Internet (ISP), na yuko nondo zaidi hata ya dogo wangu mwingine aliyemaliza UDSM Computer Science mwaka jana.

Kwa kifupi ukiona mtu mwenye Bachelor kakabidhiwa course afundishe labda anafundisha watu wa Diploma au Certificate, lakini hakuna mtu mwenye Bachelor anayesimamia somo lolote UDOM, zaidi ya kusimamia semina.

Narudia tena nyie mnaoponda UDOM bila kufahamu ukweli ni wanafiki, mataahira, wapumbavu na wazandiki msiopenda maendeleo ya elimu katika nchi yetu.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki UDOM.

Ndugu zangu ma GREAT THINKERS
naomba niwaulize swali moja tu leo juu ya uhalali wa baadhi ya wapinga maendeleo ya kielimu ktk JF kukiita chuo kikuu cha dodoma kuwa ni CHUO CHA KATA,ningependa kutambuwa ni vigezo vipi wapinga maendeleo ya kielimu hapa JF wanavitumia ktk ku grade UDOM kama chuo kikuu cha kata?

mimi nadhani umefika wakati baadhi ya wapingamaendeleo ya kielimu hapa jf wakubali mchango mkubwa uliotolewa na serikali yetu ktk kukijenga hiki chuo,kwani tutambuwe kuwa ktk Dunia ya sasa bila elimu huwezi kuendelea

May be tubomoe chuo cha UDOM ili kuwaridhisha baadhi ya wana Jf wasiokubali kuwa UDOM ni chuo kikubwa pekee hapa TANZANIA na chenye msaada mkubwa ktk taifa letu kimaendeleo

Wana jf kuna uhalali kweli wa kukiita chuo chetu kikuu cha udom kuwa ni chuo cha kata? ama kwa sababu msingi wake ni CHIMWAGA jengo la mikutano ya CCM? hivyo inatufanya tuendelee kuwa na fikra zile zile za kila siku?

karibuni jamvini
MSEMA UKWELIIIIII HAPENDWIIIII DAIMAAAAAA

mapinduziiii daimaaaaaaaaaaa :target::target:

---------------

Mie nasapoti hili na nilishashtukia UDOM ni bomu lingine la elimu, hata hayo majengo yaliyojengwa na wachina kwa muda mfupi tuyape miaka mitano tujue kama ni imara. Kuna ripoti mbaya kuhusu sewage system iliyopo etc.

Kazi kweli kweli!
 
Kwa mara nyingine nasema wanaoponda UDOM na Mataahira na inabidi wakapimwe akili, wanapelekwa na hisia na chuki na wivu vimewatawala,
nimejaribu kufanya utafiti nikaona wote wanaoponda UDOM ni vilaza especially wanaotoka katika vyuo flani flani ambavyo kwa sasa vinaonekana kufunikwa na UDOM, mdogo wangu amemaliza UDOM kwenye college ya I.T mwaka huu, na alipata multiple admission moja ya UDSM engineering, ila akaamua kwenda UDOM kusoma I.S na miaka yote aliyosoma pale alifanya field na sasa anafanya kazi kwenye kampuni flani kubwa hapa dsm inayotoa huduma za Internet (ISP), na yuko nondo zaidi hata ya dogo wangu mwingine aliyemaliza UDSM Computer Science mwaka jana. Kwa kifupi ukiona mtu mwenye Bachelor kakabidhiwa course afundishe labda anafundisha watu wa Diploma au Certificate, lakini hakuna m2 mwenye Bachelor anayesimamia somo lolote UDOM, zaidi ya kusimamia semina.
Narudia tena nyie mnaoponda UDOM bila kufahamu ukweli ni wanafiki, mataahira, wapumbavu na wazandiki msiopenda maendeleo ya elimu katika nchi yetu.

Mungu ibariki Tanzania, mungu ibariki UDOM.

Unaoongozwa na jazba mkuu, polepole. mbona mimi nawafahamu T.A's waliopewa kozi wanafundisha? unaweza kushangaa wewe ndio umepitwa bna wakati. By the way kila mtu anao uhuru wake hapa habari ya kumwambia mtu sijui mpumbavu au taahira na konyesha usivyo mvumilivu wa kukosolewa. Kuwa mstaarabu kidogo
 
Hivi nyie mnaokiponda udom mnakunya akili au?
Hamfikirii kuwa kodi zenu mnazokatwa kwenye mishahara
yenu zimechangia kujenga pale?
Badala mjivunie angalau kodi zenu zimefanyia jambo la heri bado linalalamika.

hakuna la kujivunia!elimu sio majengo.
Tatizo letu tanzania tunataka kila mtu awe na 'White coller job'
vocational training ni muhimu kwa watoto wetu,haiwezekani na haitatokea watanzania wote tukawa na akili za kufika university hata tukiweka UDOM kila kata.lazima kuwe na wasomi werevu(wachache) na watu wenye elimu ya msingi level ya vocational training/fom 6 ya ukweli.wasomi hawa wapewe jukumu la kuiletea maendeleo nchi kwa kutumia vipaji vyao vya kiakili.hata marekani,UK na Kenya hakuna degree holders weengi kama tunavyohisi.nadhani ingekua jambo la msingi kuviboresha vyuo kama UDSM,SUA,MZUMBE,IFM,DIT... Kuliko kukurupuka na hiki chuo cha kata.
Najua ntawaumiza sana wale wanaopata marks za tia maji tia maji but i ll never hesitate kueleza ukweli unapohitajika.
 
unaoongozwa na jazba mkuu, polepole. Mbona mimi nawafahamu t.a's waliopewa kozi wanafundisha? unaweza kushangaa wewe ndio umepitwa bna wakati. By the way kila mtu anao uhuru wake hapa habari ya kumwambia mtu sijui mpumbavu au taahira na konyesha usivyo mvumilivu wa kukosolewa. Kuwa mstaarabu kidogo
Weka wazi, tutajie huyo mwenye bachelor na anafundisha tumjue na tujue anafundisha course gani?

Isijekuwa anafundisha certificate, acheni chuki nyie watu, mnaponda sana UDOM, chuo ndo kinaanza mnakuwa na chuki hivyo.

Umefanya utafiti UDSM, Mzumbe, SUA, Ardhi, Tumaini na kwingineko ukaona wao ni wasafi 100%?

Acheni ishu za ajabu nyie watu.
 
Hilo ndio swali la msingi. Tufanyeje? Hata hivyo mimi sio mpinga elimu nakosoa utaratibu mbovu uliopo udom na vyuo vingine hata udsm. Ningekuwa mpinga elimu nisingesoma basi. hata mdogo wangu yupo udom. Cha kufanya tusiwe na ulimbukeni, twende taratibu idadi ya wanafunzi iendane na hali halisi ya miundombinu. Walimu wenye hadhi ya kufundisha Chuo kikuu watafutwe, waliopo waendelezwe na uongozi wa juu wa chuo umulikwe sana
ok tufanye nini sasa ukiwa ni mmoja wa wapingaelimu ndani ya JF SEMA nini kifanyike ili tuondokane na kauri yako isiyoweza kubalika daimaaa?

mapinduziiii daimaaaaa
 
Sina uhakika na haya,kwani vigezo vipi umetumia kutambuwa uduni wa wanafunzi na familia zao? pia hakuna chuo chochote duniani kimeanza na kuwa na maprof kama walimu,ni lazima uajili then usomeshe,sasa mkuu mimi sikuelewi unapozungumzia vodafasta,sijui wapi wanatowa degree za namna hiyo sijui tupe chuo kinacho andaa walimu wenye degree voda fasta

mapinduziiii daimaaaaaa

MUHAS na ARDHI ni kati ya vyuo vilivyoanza na walimu wa kutosha.we unaishi dunia gani?
 
Mla Mbivu

Muulize mdogo atakutajia hao watu. Vinginevyo anza wewe kujianika jina lao halisi hapa nami nitakutajia au unataka twende kwenye PM nikupe facts? Kama Mzumbe, Udsm au Sua kuna watu wa aina hiyo sio sababu ya Udom kuwa hivyo pia. Huwezi kuiba kwa sababu jirani yako ni mwizi wewe vipi bwana?

Usidhani tuna chuki na UDOM, hata mimi nina wadogo zangu wapo pale ndio tunaowasemea hapa. Pointi yangu usimwite mtu taahira kwa sanbabu anwambia ukweli hata kama ukweli unauma.

Halafu unanidhalilisha kwamba sijui tofauti ya bachelor na certificate? Jamani ushabiki kitu kibaya sana
 
Last edited by a moderator:
Me pia huwa nashangaa iweje watu waseme udom ni chuo cha kata! Kiukwl chuo hiki cku zinavyokwenda kitakuwa bora sana,ni kwl vyuo vingi Tanzania (c udom pekee) kuna upungu mkubwa wa wahadhiri,ili kutatua tatizo hili udom huwaendeleza kielimu waliowaajiri.

Mwaka juzi nikiwa udsm nilimsikia prof. Tibaijuka (waziri wa makazi alishawi fundisha UDSM) wakati wa wiki ya Kigoda cha Mwalimu akisema hata UDSM ilipoanza haikuwa na waadhiri wenye sifa, watu wengi wakasomeshwa nje walau mambo yakabadilika..

Vivyo vivyo UDOM itakuwa nzuri its just the matter of tym..cha muhimu wazalendo msome kwa bidii mkiwa undergraduate ili muweze kupata gpa inayohitajika (3.8 and above) ili mkihitajika muweze kuajiriwa,wengi wagraduate mitaani hawana gpa hiyo that's why kuna upungufu mkubwa wa wahadhiri nchi nzima.
 
Elimu siyo siasa!!!! Ni chuo cha kata na sababu hizi hapa

1) Wanagraduate bila mafunzo ya vitendo
2) Walimu wao wengi wana bachelor au masters degree (Kawaida hawa ni tutorial assistants)
3) wanaoapply hapo wengi ni wasio na matumaini vyuo vizuri hapa TZ

Labda wewe unafikiri chuo ni majengo! La hasha! Chuo ni elimu bora.

Conclusion

UDOM ni chuo cha kata mpaka hapo kitakapokuwa na walimu wenye sifa na wanafunzi bora

Mkuu,
Kwanza labda niulize ni katika mfumo wa Chuo Kikuu gani duniani hakina Tutorial Assistants ambao wanafundishwa ili nao watakapohitimu waje kuwa maprofesa?

Ni taasisi ngapi za umma na binafsi zilizolalamika ubora wa graduates wa UDOM? Miezi 6 imepita tangu wengi wao waajiriwe

Wanafunzi zaidi 21,000/= waliopo UDOM sasa wangekuwa wapi baada ya kukosa nafasi UDSM, IFM, SUA, MZUMBE au MUCCOBS? Kama si kuongeza idadi ya vibaka na wavuta unga mitaani?

Tujifunze kuwa na shukrani.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom