Wana jf. Mtaji wa 5 million, nitaweza kuinuka kwa hii biashara

kwamtoro

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
4,922
3,234
Sina kazi ya kuajiriwa kwa sasa, nimeamua kuacha kwa sababu ya kutovulia kufanya kazi na ndugu zetu wa Asia.

Nina Million 5 katika account yangu. Nime plan kufungua Grocery pamoja na kibanda kama cha nusu jiko hivi maeneo ya Tabata.

Je nitaweza kutoka kweli kwa biashara hii.

Vitu vinavyo nichanganya ni gharama za uanzishaji

1 Pango
2 freezer
3 ujenzi wa kibanda cha chips
4 Viti & Meza
5 Usajili wa jina la biashara, licence
NK
Naombeni ushauri, nitaweza wekeza katika biashara hii?
 
kwa nini usifanye research mwenyewe na kujua gharama za hivyo vitu, nadhani itakua vizuri zaidi kuliko hata ushauri tutakao kupa hapa.
 
kwa nini usifanye research mwenyewe na kujua gharama za hivyo vitu, nadhani itakua vizuri zaidi kuliko hata ushauri tutakao kupa hapa.

Ndugu yangu humu ndani ya JFkuna wajasiria mali walio bobea. Wanaweza wakanipa njia ya kupunguza gharama nikabakiwa na hiyo pesa pia. Au mitazamo mingine
 
Mkuu unasikitisha jambo moja, tu, UNASHINDWA KABLA YA KUANZA, Mkuu hutakiwi kushindwa kabla ya kuanza na unatakiwa uamini kwamba utafanikiwa,

Kwa sababu umeisha jua sababu za kushindwa huna budi kupambana nazo mapema kabisa na kuzishinda

KUHUSU GHALAMA

1. Mkuu si razima uanze na vyote hivyo, mfano freeza, unaweza tafuta za mitumba zinazo uzwa, ukaongea na mtu aliye karibu na ulipo mwenye freeza ukawa unatumia ya kwake kwa muda na kumlipa kiasi fulani mpaka utakapo sima

2. Viti si razima ununue vipya, unaweza anza na mabenchi mkuu, kinacho waleta wateja si viti make hata nyumbani kwao vipo tena vikali sana na wameviacha, Mteja atakuwa mwenda wazimu kama atakuwa analetwa na viti, anza na mabenchi kwanza mkuu, kikubwa ni location nzuri na huduma nzuri

3, Hizo za usajiri ninavyo jua ni bure

Kwa hiyo mkuu hutakiwi kushindwa kabla ya kuanza, na ukianza ukiwa na mawazo ya kushindwa hakika utashindwa, ila unatakiwa kuwaza kufanikiwa daima,
 
Sina kazi ya kuajiriwa kwa sasa, nimeamua kuacha kwa sababu ya kutovulia kufanya kazi na ndugu zetu wa Asia.

Nina Million 5 katika account yangu. Nime plan kufungua Grocery pamoja na kibanda kama cha nusu jiko hivi maeneo ya Tabata.

Je nitaweza kutoka kweli kwa biashara hii.

Vitu vinavyo nichanganya ni gharama za uanzishaji

1 Pango
2 freezer
3 ujenzi wa kibanda cha chips
4 Viti & Meza
5 Usajili wa jina la biashara, licence
NK
Naombeni ushauri, nitaweza wekeza katika biashara hii?

ok ni wazo zuri mimi ni mjasiliamali wa miaka mitano sasa.
Nina ofic nzuri na inayolipa kama uko tayari uje nikueleze ukiwa tayar na kama ni mchakalikaji unaingia then tunakupa ownership.
Just nicheki kwenye
imamu.njama@yahoo.com
kama uko tayari tuongelee hili.
 
Je wewe upepanga au unaishi/kula kwa wazazi bado? (kifupi huyo 5M yako inaunganisha na gharama zako binafsi)
 
Je wewe upepanga au unaishi/kula kwa wazazi bado? (kifupi huyo 5M yako inaunganisha na gharama zako binafsi)

Mimi nimepanga pia nimeshalipa kodi ya mwaka mzima toka last month, pesa ya matumizi kwa miezi mitano mbele ninayo bila kugusa mtaji wa 5M
 
Mimi nimepanga pia nimeshalipa kodi ya mwaka mzima toka last month, pesa ya matumizi kwa miezi mitano mbele ninayo bila kugusa mtaji wa 5M

Umekwisha anza mkuu? au bado unasikilizia, Ukiona hiyo aidea yako haijakaa vizuri unaweza piga china na kuja na aidea nyingine
 
Back
Top Bottom