Wana jf huyu mtoto ni malaika anahitaji msaada wetu, na amekataa kwenda loliondo

COMPLICATOR2011

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
253
35
[h=1]Mtoto huyu haendi Loliondo[/h]

Mtoto Cecilia Edward (14) (pichani), mkazi wa Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani, ambaye kwa sasa anaishi na mlezi wake, Mbagala jijini Dar es Salaam, bado anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo na amekuwa akihudhuria kliniki na hajapata mabadiliko.

Kwa mujibu wa mlezi huyo, Cecilia anasumbuliwa na ugonjwa huo, hali iliyosababisha tumbo kujaa maji mara kwa mara.

Imeelezwa na mlezi wake huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwamba tatizo hilo lilimuanza Cecilia baada ya wazazi wake wote kufariki dunia akiwa na umri wa miaka minne.

Hata hivyo, mlezi wake huyo alisema mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam kuwa hana niya ya kwenda kutibiwa Loliondo kama ilivyoripotiwa na gazeti hili siku za nyuma.

“Sina mpango wa kumpeleka mtoto huyu Loliondo na anaendelea na kliniki,” alisema.
Awali gazeti hili katika toleo namba 687 la Mei 31 liliandika kimakosa kuwa jina lake ni Khadija Ally na kuwa mtoto huyo anaomba msaada wa kwenda kutibiwa Loliondo kwa Babu.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.
 
Wandugu wapenda angalieni kiumbe huyu.....UKIMSAIDIA MMOJA WAPO WA WADOGO HAWA UMEMJUA MUNGU KWELI KWELI.....NA UKIMKATAA MMOJA WAPO WA WADOGO HAWA UMEMKATAA MUNGU KWELI KWELI....
 
Sasa kinachonishangaza mimi ni huyo mlezi wa mtoto huyo kukataa kutaja jina lake, au ndo chuma ulete wake?
 
mimi naomba contact za huyu mtoto au account number ya bank au je pesa nitakayo tuma tafikaje kwa mlengwa please naomba kama nitaweza kuwasiliana na mzazi wa huyu mtoto
 
Back
Top Bottom