Wana JF, Hivi kuna tatizo gani kuoa mwanamke aliyekwisha zaa

KIFARU

Senior Member
Apr 6, 2009
172
14
Wakuu naomba nifahamisheni mazuri na mabaya ya kuoa mwanamke aliyezaa, kuna mwanamke naona tunaendana kila kitu sema yeye tayari ana uzao
 
cdhani kama kuna tatizo, ishu ni maelewano/makubaliano yenu kuhusu huyo mtoto kabla ya ndoa,.....jamii yetu nahic inaliangalia hili suala ki tofauti hasa mwanamke kuolewa akiwa na mtoto lakini kwa wanaume linachukuliwa kama jambo la kawaida tu....kama mnaenda sawa nakushauri songa mbele.
 
ooya inakuwaje?
sikupati hewani siku hizi,umebadilisha namba?
 
Sio ishu kabisa.
Mbona wao wanawake wanakubali kuolewa na wanaume ambao tayari walishazaa??(wenye watoto), hayo ni mambo ya mfumo dume tuu, cha muhimu maelewano tuu.
 
Baba wa huyo mtoto bado hajaachana na huyo binti, atakwambia kuwa wameachana lakini wakikutana we haupo wanakumbushia enzi hizo na matokeo yake wanaendelea kuongeza watoto kwenye kaya yako,

hachana naye tafuta mwingine
 
hiyo ni tatizo ambalo nalitegemea, lakini mkuu haiwezekani wazazi wawili uhusiano ukafa kabisa?mapenzi yasiwepo wakaangalia ulezi wa wanao tu?
 
ooya inakuwaje?
sikupati hewani siku hizi,umebadilisha namba?

hey hey hey nimeihack..watoto kama ninyi mlizidi kumwendea hewani ndo nimefungulia tu kidogo...mkicheza naiweka kabisa kibindoni! LOL:rolleyes:
 
Baba wa huyo mtoto bado hajaachana na huyo binti, atakwambia kuwa wameachana lakini wakikutana we haupo wanakumbushia enzi hizo na matokeo yake wanaendelea kuongeza watoto kwenye kaya yako,

hachana naye tafuta mwingine

Sasa umenifumbua macho, kwa hiyo hawa wakina baba wenye wana tunaokubali kufunga nao pingu huwa wanarudi kwa wazazi wenza wao? Usitoe macho, what you said here, its vice versa is true!

Ila kwa mtazamo wangu, sioni tatizo la kuoa mwanamke mwenye mwana, kwani wasiwasi uko wapi zaidi? Ni huko kulea mwana, au zoezi lenyewe la yeye kuzaa kuwa kachoka?
 
hiyo ni tatizo ambalo nalitegemea, lakini mkuu haiwezekani wazazi wawili uhusiano ukafa kabisa?mapenzi yasiwepo wakaangalia ulezi wa wanao tu?

Hilo huwa nahisi kama gumu hivi! hasa kwa upande wa mwanamke.....ila tu uwe tayari kukubali hali halisi pindi ikijionyesha!
 
Wakuu naomba nifahamisheni mazuri na mabaya ya kuoa mwanamke aliyezaa, kuna mwanamke naona tunaendana kila kitu sema yeye tayari ana uzao

Hakuna tatizo iwapo umekubaliana na hali hiyo na huyo mwanamke asimkumbuke tena mzazi mwenzaje wa kwa nza
 
Wakuu naomba nifahamisheni mazuri na mabaya ya kuoa mwanamke aliyezaa, kuna mwanamke naona tunaendana kila kitu sema yeye tayari ana uzao

Kwani shida yako ni kupanda gari jipya au kufika mwisho wa safari ukiwa comfortable...? Either ukipanda daladala jipya ambalo hajapanda mtu yeyote au ukipanda daladala lililotumika, mwisho wa siku utafika kwenye safari yako....!

Kama mashine ume-test mwenyewe umeikubali, habari ya kuzaa inakutatiza nini? La kama hujai-test, jaribu kutest kwanza uone, asikusimulie kwa mdomo...!
 
kuoa na mwanamke aliyezaa hana shida kwa sababu tayari yuko mature na anayo respobility kama yeye ni mama.......... nothing bad to have a child maana wototo ni malaika!!!!
 
Mkuu kifaru, kwa upande wangu sioni kama kuna tatizo lolote, chamsingi hapa ni maelewano tu. Kaka yangu kaoa mwanamke aliyekuwa na mtoto, lakini maisha yao ukiyaona yanaendelea na familia yao ina furaha kabisa.
 
Hilo huwa nahisi kama gumu hivi! hasa kwa upande wa mwanamke.....ila tu uwe tayari kukubali hali halisi pindi ikijionyesha!

mr linawezekana kabisa, nina mifano hai ya ma frnd zangu wa karibu, tena hata salamu hawapeani na hao baba watoto zao, inategemea kisa na mkasa mpaka wakatengana......
 
Baba wa huyo mtoto bado hajaachana na huyo binti, atakwambia kuwa wameachana lakini wakikutana we haupo wanakumbushia enzi hizo na matokeo yake wanaendelea kuongeza watoto kwenye kaya yako,

hachana naye tafuta mwingine

kwanini amdanganye, sio kila mtu ni muongo....ukiwa unajitambua/mcmamo kwenye lyfe hakunaga hiyo kitu kujikumbushia wala kukumbukia........
 
mr linawezekana kabisa, nina mifano hai ya ma frnd zangu wa karibu, tena hata salamu hawapeani na hao baba watoto zao, inategemea kisa na mkasa mpaka wakatengana......
there you are talking!.
mi niko tayari kuoa mwanamke aliye na mtoto aliyetelekezwa na babake, lakini sipo tayari kama baba yake yupo na waliachana na huyo mwanamke kwa sababu za ajabu kama kutokua na uaminifu kwa mmoja wao, ugomvi etc, coz iko siku wakarudia mahusiano yao kwa siri.
 
ewaa mrs apo ndo penyewe...kisa na mkasa ...ndo kusema kwamba kama walitengana kwa sababu nje ya uwezo wao kuna hatari wakakumbushiana ili mtoto asifananie upande mmoja tu lol

jingine ikitokea kuwa mi niliyekuoa tukakorofishana kidogo basi si itakuwa rahisi kwenda kwa 'baba mtoto' ! kupoza machungu! na mi niliyeoa nikijua kabisa possibility iyo ipo!
 
there you are talking!.
mi niko tayari kuoa mwanamke aliye na mtoto aliyetelekezwa na babake, lakini sipo tayari kama baba yake yupo na waliachana na huyo mwanamke kwa sababu za ajabu kama kutokua na uaminifu kwa mmoja wao, ugomvi etc, coz iko siku wakarudia mahusiano yao kwa siri.

enheee..Mpwa hapo ndo hoja yangu ilipo!
 
Kama manelewana nyie owaneni tena bora huyu aliyezaa kuna wengine wamefanya arbotion zaidi ya mara 10 na ukikutana naye wala hutafahamu, huyu anadhambi kubwa zaidi ya huyo aliyezaa na infact anadhihirisha yuko fertile issue ya kupata mtoto siku hizi nayo tete.

Nakutakia harusi njema.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom