Wana jf hili nalo ninalo!

Capitalist

Senior Member
Feb 3, 2011
164
27
Wadau nilikuwa na dada 1 ambaye nilimpenda sana nayeye alionesha kunipenda ila tulikuwa tunakaa sehemu tofauti mi nilikuwa nafanya kazi wilaya nyingi na yeye mkoani, nilipata likizo sept 2008 nikaspendi naye mwezi mzima, aliniambia kuwa anamimba nikamwambia poa usijali mi nitakuoa, niliondoka kurudi kazn mawasiliano yakawepo alijifungua mei 2009. Alinipa taarifa nikaenda nilimpatia mahitaji yote, nilikuta ameondoka kwao kudai kuondoa aibu kapanga nikalipa kodi ya nyumba, kitanda, chakula alidai mamake kampa. Kumbe yupo mwanaume mwingine ambaye ameambiwa hvyohvyo na anatunza, siku moja kanicall mtoto anaumwa nilifunga safari kwenda kumjulia mwanangu hali ndipo tulipogongana na jamaa tukaeleza na alikuwa ameshaanza kuishi naye, tukaelezana ukweli jamaa alichanganyikiwa mi nikachangayikiwa, mpaka sasa anaishi naye kang'ang'ania mtoto yule wake. je kama ww ungefanyaje?
 
Kacheki DNA yako na mtoto, baada ya hapo utajua moja. Kama mtoto wa kwako kamchukue. Kama si wako. Move on. Lakini achana na huyo dada:coffee:
 
Huyo mwanamke hafai kabisa nakushauri sahau kuhusu yeye.
Chakufanya jipinde ufanye dna test kujua kama mtoto ni wako au la then utajua chakufanya, kama sio wako its ok, kama wako ufanye mchakato umri sahihi ukifika mchukue
 
Kwa mtazamo tu yule dogo ni mm photocopy na yule dada mpaka leo anakiri ni wangu nikimwuliza ilikuwaje akafanya hvyo anakiri ni tamaa zilimshawishi, zote pesa na nani hii maana yule jamaa ana kakibanda.
 
Hii naifananisha na moja ya hadith za shigongo. Muendelezo wa hapo ulipo ishia....wanaume wakashauriana wakaona hata wakipigana hawata haitawasaidia ika bidi wamuache huyo mwanamke.mwanamke alilia sana huku akijutia ujinga wake.
 
Hii naifananisha na moja ya hadith za shigongo. Muendelezo wa hapo ulipo ishia....wanaume wakashauriana wakaona hata wakipigana hawata haitawasaidia ika bidi wamuache huyo mwanamke.mwanamke alilia sana huku akijutia ujinga wake.

Ila huyu dada mpaka sasa bado yuko pamoja na yule man alafu huwa ananipigia simu ati mwanao anakusalimia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom