Wana JF, hebu tujadili hili pengine Kikwete hafahamu

NIMEKIMBIA CCM

Senior Member
Oct 4, 2011
193
26
Naamini kabsa wote tunafaham mh rais jins asivyo aminika na watz, naye mwenyewe analifaham hilo, na wananchi hawampendi kabsa jinsi siku zinavokwenda (angalia tofauti ya matokeo ya 2005 na 2010),

SASA NDUGU ZANGU HIVI NYIE MNAONA AFANYE NINI ILI JAPO IMANI HATA KIDOGO JUU YA RAIS WETU TUIRUDISHE? MAANA INAWEZEKENA MH KACHANGANYIKIWA kwa kuwa aliahidi mengi alishindwa kuyatimiza, je pamoja na kushindwa kutimiza je atufanyie angalau yapi ili arudishe heshma na uaminifu japo hata 45%?
 
Ajiuzulu kwa sababu sioni kama ana uwezo wa kufanya lolote lile katika kipindi cha kutoka sasa hadi 2015. Hii itasaidia kuwa na Serikali ya muda na hivyo kuwezesha uchaguzi mwingine labda baada ya miezi 12 au 24 tangu atakapojiuzulu mara tu baada ya kuwa na katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
 
Yapo mengi ya kufanya lakini yote ni maamuzi magumu kwake.

1. Awashughulikie mafisadi wote walioliingiza taifa katika mikataba mibovu kabisa ikiwemo Richmond.

2. Kuwachukulia hatua wote walioiba fedha katika EPA.

3. Akatae kuwalipa DOWANS.

4. Atekeleze kivitendo nadharia yake ya kijivua gamba.

5. Ashughulikie mfumuko wa bei, tatizo la kushuka kwa thamani ya Tshs yetu na kwa kadri uchumu ujavyokuwa awaangalie wafanyakazi.

6. Aongeze juhudi katika kukusanya kodi na kupunguza matumizi yasiyo ya msingi ya serikali.

7. Ahakikishe tatizo la umeme linapatiwa ufumbuzi wa ukweli na siyo usanii.
 
hii nchi ni yetu sote.
Apunguze bei vifaa vya ujenzi
bati-6000 Cement-5000
huduma kwa jamii maji vijijini
Waliofungwa kwa hila waach4we
 
Ajaribu kurekebisha maeneo machache yenye shida. Hasa kuongeza ajira kwa vijana hilo ni la msingi zaidi.
 
Naamini anatambua kua yeye ni tatizo... Hilo halitoshi, ajitahidi atatue mizizi ya matatizo ambayo ni wazi kabisa aweza yafanyia kazi lakini anadharau...
 
Amfunge LOWASSA ndiyo nitaanza kumuamini kwa mbaaaaaaaaaaaaaaaaali.
Ni heri Lowassa (mtazamo wangu) kuliko hawa wahindi (wa DOWANS na EPA) maana wao wanahamisha tu rasilimali zetu na kupeleka nje na bado si tu wanaaminika ndani ya CCM bali wanaabudiwa (ni swala la wakati tu ndugu zangu yana mwisho haya)
 
Tuache matani, kama angekuwa na washauri wazuri na wakamshauri KULIVALIA NJUGA suala la KUBADILISHA KATIBA ninakuhakikishieni Mhe JK angejitengenezea LEGACY ambayo itadumu hadi siku Bwana Yesu au Mtume Mohammed (SAW) atakaporejea duniani. Hiyo nafasi anayo, asilimia kubwa ya umma inasapoti suala hilo - na hicho ndio kitakuwa chanzo cha kuikomboa Tanzania bila kumwaga damu. KATIBAAAAAAAAAAAAAAA baba na utajengewa mnara wa kumbukumbu.:lol:
 
Ajaribu kurekebisha maeneo machache yenye shida. Hasa kuongeza ajira kwa vijana hilo ni la msingi zaidi.
Penye red sijakuelewa
  • AJARIBU kwani uwezo hana hali ile ni taasisi yenye zana zote
  • MACHACHE halafu mengine iwenje kwanza kwa nini machache
 
kama haumpendi sio rahisi kumuondoa sasa ni kheri tu uvulimie hakuna jinsi kwa katiba iliyopo ndiye rais hadi 2015 kama hatutashirikiana naye nchi itayumba. tusipoteze muda kumjadili kikwete hadi 2015 tutakuwa tumeacha kujadili mambo ya kwa miaka minne ijayo.
 
kikwete kikwete wimbo huu tumechoka nao tangu 2004 hebu tujadili issues, mathalan changamoto za chuo alichojenga cha Dodoma ili watanzania wenzetu waweze kufaidika japo na machqche ambayo huyo kikwete amefanya sisi tuboresha utendaji katika maeneo hayo. miminaona hii inaweza kutusaidia kuliko kuimba wimbo wa simpendi kila siki na vibwagizo vyako
 
1. Katiba Mpya (Pamoja Na Mambo yote impunguzie rais mamlaka, kama za uteuzi nk).

2. Amfukuze Ngeleja Na atatue shida ya umeme.

3. Wafungwa waloonewa waachiwe, na kesi ziende haraka na kwa haki.

4. Arudishe thamani ya pesa yetu na ailinde.

5. Ataifishe mali zote zilizopatikana kifisadi, na pesa zitakazopatikana awakopeshe kaka na dada zetu wasome vyuo.

6. Aache usela na kazi

7. Dhana ya maisha bora iwe kweli

8. Ajira na fursa sawa ziwe kweli

9. Awapunguze polisi viburi, (wanawaonea sana wananchi wa kawaida).

10. Kodi itozwe kihalali na matumizi ya mapato yaonekane mpaka kwa mwananchi wa kawaida.

11. .......


Fanya hayo machache kwa mwaka huu na watanzania watakukumbuka Daima
 
Back
Top Bottom