Wana jamvi namleta kwenu kamanda Esther Wasira; naomba tumpe ushirikiano

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454
Kwa hesima na taadhima nawaomba wanajamvi tusichangie hili bandiko mpaka hapo atakapoanza yeye. Ameniahidi atakuwa hapa muda si mrefu, nawaomba tumpe ushirikiano wa kutosha , tuulize maswali yenye mantiki kwa muskakabali wa taifa letu, ni matumaini yangu mmenielewa karibu jembe,karibu dada yetu.
 
Habari Wana Jamvi,

Awali ya yote niombe radhi kwa kutofika mapema kuchangia thread hii, nilitumwa na mwajiri wangu nje ya eneo la kazi, sikuwa nimeona hii.

Asanteni sana kwa kunikaribisha kwa namna ya kipekee; I am truly humbled. Nimekuwa mfuatiliaji wa pembeni kwa muda mrefu lakini sasa hivi nipo humu miguu yote miwili.

Binafsi huwa nafurahishwa na uhuru wa kuchangia mawazo uliopo humu ndani, na nadhani kama kuna kiongozi anayetaka kujua anatakiwa abadilishe nini na wapi, awe anapita humu na anazingatia yote ya msingi yanayoongelewa na jamii yake. This is "Jamii Forums".

Ninashukuru kwa yote mema na mazuri yaliyosemwa juu yangu, maana yananipa nguvu za kusonga mbele, lakini pia nashukuru sana kwa yale ambayo hayaonekani kuwa mazuri au mema kwangu maana hayo hasa ndio yanayonijenga zaidi.

Thank you..
 
Tumjue huyu esther wasira ndo yule muimbaji alishirikigi mashindano flani hv? ndo baadae akaamua kuwa lawyer au ni mwingine? utangulizi tu mkuu usi-mind
 
Karibu JF dada hapa utakutana na mambo kibao maswali mazuri na ya ajabu na ya kizushi hata matusi but moderator watakuwa makini kuondosha yale ambayo hayastahili
 
Ndo nani huyo Ester had tumuulize maswali ya mustakabali wa taifa letu..... Sijakuelewa kabisa
 
Jamani tumeambiwa tusubiri aanze ndo tumuulize maswali...sasa mbona mmealianzisha kabla?

AANZE SASA KACHELEWA SANA ANGALIA WASOKUWA NA ADABU WANAANZA KUMUITA MNYAMA GANI, AU TUANZE MAANA KUNA NLOMSIKIA KT MDAHALO WA NKURUMA MAJUZI JE NDO UYO? O.W NAMI NTAULIZA NI MNYAMA GANi? SAMAHANI MH,..
 
There are currently 44 users browsing this thread. (18 members and 26 guests)

Kweli Ester Jembe, wote hao wanakusubiri.
 
Huyu namkumbuka alisomea Loyola.. Baada alikuja kua msanii wa Bongo flava.

Nimemkubali sana Esther kuingia kwenye siasa...
 
Estheeeeeeeeeeeeeer.. Habari yako bana!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Huyu dada ni jembe hile mbaya! Nimkubali sana ana jua kujenga hoja kwa kweli
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom