Wana Dar es Salaam tutoe maoni yetu, ili mkutano wa CDM Dar Urudiwe baada ya Bunge Bajeti

Naunga mkono hoja.

Inabidi baada ya Bunge la Bajeti Mkutano wa Dar es Salaam urudiwe. Tutachangia kama tulivyofanya Chadema Square kama tulivyofanya Jumamosi tarehe 26 Mei 2012. Nadhani ndugu Lema anakumbuka kwani naye alikuwa kati ya watu waliokuwa wanakusanya michngo siku ile pale Chadema Square.

Wakuu vilvile naomba mtukumbushe ile namba ya kutuma pesa kwa ajili ya M4C kwenye M-Pesa.

Najua namba ni 111333 lakini sijajua kwamba hii namba unatuma kama unamtumia wakala au kama unamtumia mtumiaji wa simu.

Naomba maelekezo zaidi na kwa watanzania wenzangu ambao hawajaelewa ili tuweze kuchangia UKOMBOZI WA NCHI YETU KUTOKA KWA MKOLONI MWEUSI CCM
 
wadau wako tayari kuchangia walau mkutano mmoja... Cha msingi tupate taarifa mapema tu..

Kweli baada ya bajeti ifanyie mikutano mingi sana Dar es Salaam sehemu mbalimbali, Kinondoni Biafra,Mwembe Yanga, Tanganyika Packers Kawe, Na sehemu nyinginezo zenye nafasi kwani pana wengine waliogopa vitisho vya polisi
 
Hili wazo la kurudiwa mkutano hapo cdm square libarikiwe sana, naomba lifanyike punde baada bunge la budget lakin pia kukiwepo na maandalizi bora zaidi na mda wakutosha. Nilikua pia nawazo 1 tusifanye maandamano yoyote, yani tusitangaze kufanya maandamano ili kupunguza hofu kwa wananchi kuhujumiwa kwa fujo na nyinyiem. Vinginevyo mchango wangu utawafikia kupitia mpesa kila mara niwapo na chochote, nawekeza katika ukombozi.
 
Maandamano yasiwepo ila kachopa katumike kiduchu kutangaza juu ya mkutano huo.
 
Back
Top Bottom