Wana ccm mpoo????

Matango

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
535
118
‘Chama Cha Mapinduzi, kwa sababu ya uzito wa historia yake, hadhi ya jina lake, mfumo wa wavu wake, mazoea ya watu, na ubovu wa vyama vya upinzani, kinaweza kuendelea kuchaguliwa na Watanzania, pamoja na kansa ya uongozi wake. Au watu wanaweza. wakachoka, wakasema, "potelea mbali:" wakachagua Chama chochote, ili mradi tu watokane na kansa ya uongozi wa CCM. Hainifurahishi kuyasema haya, lakini uhai wa nchi yetu unataka yasemwe. ‘J.K. Nyerere ; Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (1994)’.


..................... ‘Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa vyama vingi. Nilitumaini kuwa tunaweza kupata chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza nchi yetu badala CCM au ambacho kingekilazimisha Chama Cha Mapinduzi kusafisha uongozi wake kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao’ ; ‘J.K. Nyerere ; Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (1994)’.:plane:


 
Back
Top Bottom